Biashara ya mashine za kusaga

Biashara ya mashine za kusaga

Naomba kujua motor nzuri ni aina gani, na vifaa vingine associated. Gharama ni kiasi gani, na duka gani ambalo halina vifaa fake na la kuaminika hizo mashine zinauzwa hasa Dar.
 
Na kwa sasa motor 20hp ni bei gan msaada jaman kwa anae jua nijarb kuona tathimin ya bajet kama iko vzuri nijarb kuwekeza na mm
 
Kamata mnyama Lister

TR-Generator-Engines-5.png
 
Na kwa sasa motor 20hp ni bei gan msaada jaman kwa anae jua nijarb kuona tathimin ya bajet kama iko vzuri nijarb kuwekeza na mm
Bei ya mota inategemea na mkoa ulipo mfano dar hp20 laki8
 
Biashara hii nimeifanya kwa miaka 3 sasa, nilianza na moja na sasa ziko mashine mbili.

Sehemu moja nimeweka Mota 2 zenye ukubwa wa 20hp kinu cha kukoboa na 25hp kinu cha kusaga nafaka..sehemu hii niliweka mota 2 kulingana na uwingi wa wateja nisije waweka foleni nikawaboa..goli la pili halina wateja wengi sana ambapo nimeweka mota moja 25hp inayohudumia vinu vyote viwili cha kukoboa na kusaga.

Kwa siku mashine moja huwa inaingiza wastani wa shilingi 30,000- 50,000 na ile yenye mota moja huniingizia si chini ya 25,000
Huwa naweka umeme wa shilingi 50,000 napewa units 130 ambapo katika usagaji na ukoboaji unit 1 huingiza wastani wa shilingi 1300 kwahyo umeme wa shilingi 50,000 huniingizia 169,000 na kwa kawaida umeme huo hutumika ndani ya siku 3-4. Kwahyo umeme wa shilingi 50,000 unakuingizia faida ya 119,000 ndani ya siku 3-4.

Pia kuna pumba za mahindi ambazo wateja wanaonenepeshea mifugo huweka oda, kwa mfano hapa kwangu nina wateja wawili wameweka oda ya gunia 200 na kwa bei ya oda ni shilingi 6,000 ambapo unapata 1.2m na kuendelea.

Kwa ujumla biashara hii ni nzuri kwa kupata hela ndogo ndogo za kuendeshea maisha, kulipa ada za watoto na vitu vingine. Biashara hii ni nzuri na haina kurupushani kama biashara nyingine. Nimeshanunua vinu 2 vingine ili nianzishe goli la 3
Karibuni
Biashara nzuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom