Biashara ya mashine za kusaga

Biashara ya mashine za kusaga

Biashara hii nimeifanya kwa miaka 3 sasa, nilianza na moja na sasa ziko mashine mbili.

Sehemu moja nimeweka Mota 2 zenye ukubwa wa 20hp kinu cha kukoboa na 25hp kinu cha kusaga nafaka..sehemu hii niliweka mota 2 kulingana na uwingi wa wateja nisije waweka foleni nikawaboa..goli la pili halina wateja wengi sana ambapo nimeweka mota moja 25hp inayohudumia vinu vyote viwili cha kukoboa na kusaga.

Kwa siku mashine moja huwa inaingiza wastani wa shilingi 30,000- 50,000 na ile yenye mota moja huniingizia si chini ya 25,000
Huwa naweka umeme wa shilingi 50,000 napewa units 130 ambapo katika usagaji na ukoboaji unit 1 huingiza wastani wa shilingi 1300 kwahyo umeme wa shilingi 50,000 huniingizia 169,000 na kwa kawaida umeme huo hutumika ndani ya siku 3-4. Kwahyo umeme wa shilingi 50,000 unakuingizia faida ya 119,000 ndani ya siku 3-4.

Pia kuna pumba za mahindi ambazo wateja wanaonenepeshea mifugo huweka oda, kwa mfano hapa kwangu nina wateja wawili wameweka oda ya gunia 200 na kwa bei ya oda ni shilingi 6,000 ambapo unapata 1.2m na kuendelea.

Kwa ujumla biashara hii ni nzuri kwa kupata hela ndogo ndogo za kuendeshea maisha, kulipa ada za watoto na vitu vingine. Biashara hii ni nzuri na haina kurupushani kama biashara nyingine. Nimeshanunua vinu 2 vingine ili nianzishe goli la 3
Karibuni
 
Sehemu moja nimeweka Mota 2 zenye ukubwa wa 20hp kinu cha kukoboa na 25hp kinu cha kusaga nafaka..sehemu hii niliweka mota 2 kulingana na
Nimependa sana huu mchanganuo mkuu,

Mashine gharama yake ni kiasi gani zinauzwa??

Na pumba mtu akija kusaga si inakuwa sio Mali yake?
 
Unaifanyia wapi
 
Mashine ni muunganiko wa vitu vingi, vinu ni wastani wa 1.6m, mota hp 20 haizidi 1.3 halafu kuna wiring 3phases...nafikiri mashine moja mpaka inawaka yenye mota 2 inaweza kufika 6m, yenye mota moja ni around 5m makadirio hayo nje ya jengo
 
Pumba huwa wanaziacha.. Ni biashara nzuri sana
IMG-20201114-WA0045.jpeg
IMG-20201114-WA0045.jpeg
 
Mashine ni muunganiko wa vitu vingi, vinu ni wastani wa 1.6m, mota hp 20 haizidi 1.3 halafu kuna wiring 3phases...nafikiri mashine moja mpaka inawaka yenye mota 2 inaweza kufika 6m, yenye mota moja ni around 5m makadirio hayo nje ya jengo
Mashine moja inatakiwa kuwa na mota mbili??

Hiyo wiring naona ni kawaida.

Vipi hujawahi kufkilia kuhusu kuanzisha bidhaa yako mwenyewe,kama unga hivi au lishe?

Unaweza tumia mashine moja,ukakobolea na pia kusagia?
 
Wazo lipo lakini changamoto eneo zilipo hizi mashine ni sehemu ya wazalishaji wakubwa wa mahindi..kwahyo wateja wanakuja na mahindi yao,ukisaga unga labda uuze nje ya eneo hili ..tatizo mtaji bado
 
Biashara hii nimeifanya kwa miaka 3 sasa, nilianza na moja na sasa ziko mashine mbili.
Sehemu moja nimeweka Mota 2 zenye ukubwa wa 20hp kinu cha kukoboa na 25hp kinu cha kusaga nafaka..sehemu hii niliweka mota 2 kulingana na uwingi wa wateja nisije waweka foleni nikawaboa..goli la pili halina wateja wengi sana ambapo nimeweka mota moja 25hp inayohudumia vinu vyote viwili cha kukoboa na kusaga.
Kwa siku mashine moja huwa inaingiza wastani wa shilingi 30,000- 50,000 na ile yenye mota moja huniingizia si chini ya 25,000
Huwa naweka umeme wa shilingi 50,000 napewa units 130 ambapo katika usagaji na ukoboaji unit 1 huingiza wastani wa shilingi 1300 kwahyo umeme wa shilingi 50,000 huniingizia 169,000 na kwa kawaida umeme huo hutumika ndani ya siku 3-4. Kwahyo umeme wa shilingi 50,000 unakuingizia faida ya 119,000 ndani ya siku 3-4.
Pia kuna pumba za mahindi ambazo wateja wanaonenepeshea mifugo huweka oda, kwa mfano hapa kwangu nina wateja wawili wameweka oda ya gunia 200 na kwa bei ya oda ni shilingi 6,000 ambapo unapata 1.2m na kuendelea.
Kwa ujumla biashara hii ni nzuri kwa kupata hela ndogo ndogo za kuendeshea maisha, kulipa ada za watoto na vitu vingine. Biashara hii ni nzuri na haina kurupushani kama biashara nyingine. Nimeshanunua vinu 2 vingine ili nianzishe goli la 3
Karibuni
Duh! Una umri kama wakwangu ktk biashara hii Mkuu. Mchanganuo ulioutoa uko sahihi kwa maana ya kwamba umeendana na uhalisia wa kile ninachokifanya na matokeo yake yako vilevile.

Hongera Mkuu.
 
Karibu, kwakweli hata ukisafiri miezi 3 nje ya nyumbani familia hailali njaa huoni simu za kuombwa hela zaidi ya wewe kuomba utumiwe kwa halopesa ha ha ha ha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom