Biashara ya kuuza genge

Haoa
Hapa umeandika kama anayeanza na 50K anapenda kumbe ndipo muscle yake ilipoishia.
 
Haoa

Hapa umeandika kama anayeanza na 50K anapenda kumbe ndipo muscle yake ilipoishia.
SIO kila anaeanza biashara na mtaji mdogo ni kweli "kakosa mtaji mkubwa au hana" kuna watu biashara ipo damuni (hata mimi siingiii),wanapenda anzia chini chini chini,hawa raia ndio hata mimi nawaogopa,hawa sio watu nawafananishaga na marobot

hela anayo ila anaishi kama hana,mtaji anao ila ukimwambia "upgrade" biashara yako (hataki) yani miaka na miaka utamuona anauza karanga kwenye ungo,au anauza kahawa kijiweni au ana genge lina vitu vya kuhesabika,nk nk..Hawa unaweza fikiri wanasindikiza wengine

ila "hapana" wakkupeleka wanapoishi,wana majumba,wanasomesha,maisha ya kawaida na mazuri tu,sema ndio hivyo ukimkuta kazini na biashara yake ina mtaji wa 50,000 unaweza hisi maskini ndio anaanza biashara huyu kumbe mtu yupo kwenye game huu mwaka wa 8 unaenda ila kaganda kama robot yupo vile vile.NO CHANGES. ukimchukulia poa SHAURI lako.
 
Nilichogundua Watanzania kuja kuondokana na adha ya Umasikini sio leo. Mtu hata atoe ushauri mzuri namna gani lkn bado atatukanwa au kupewa kejeri. Any way hii labda inatokana na stress ambazo tuko nazo asee....!!!
Ni kweli asee,, ht mi nimefuatilia madam nyingi nimeiona hili janga
 
Unajua ukiwa unazungumzia biashara unazungumzia numbers, hakuna kitu kinachoitwa "inalipa sana" au "biashara inafaida sana" ingawaje wafanyabiashara wengi tumekua tukitumia sana haya maneno.

Unachotakiwa kusema (mfano) kwa msimu mzuri nyanya tenga nanunua 30, 000/= nikiuza napata around 40,000/= mpaka 45,000/= so faida inakua 10k to 15k. Tenga moja linaisha after one week. Unaona sasa hesabu inavyoeleweka? Kwa mfano tu hivyo ndo mfanyabiashara anatakiwa kusema biashara inalipa or namna gani vepe!
 
Huyo anayesema mtaji zaidi ya laki 5 na huyu aliyesema ina faida mno wote maelezo yao hayafanani na genge la mama
 
Genge nyumbani kwako wakazi wa Dar tunakufikishia bidhaa zote za gengeni kwa Bei nafuu
 
Hongera sana kiongozi kwa mawazo yako mazuri,ila biashara hii haiko hivyo unavyozani,kiufupi ni biaharayenye changamoto nyingi sana na imejaa fitina/ushirikina wa kila aina,ukiweza kujipanga(kwa Mungu/miungu) hapo sawa.
 
Habari za wasaa huu wakuu naitaji msaada mwenye kujua vizuri biashara ya uuzaji genge.

ikiwemo mtaji,faida,hasara na pamoja na kuliendeleza zaidi na kuwa la kisasa kabisa Asante na nawasilisha.
 
Biashara nzuri sana mbali na location na mtaji, pia kama unaajiri mtu usimueke kijana wa kiume....

Mana kuna wanawake wanakuja na mia tano but watataka warudi na vitu vya buku...
 
Biashara ya genge jitahidi ujenge connection na wauzaji toka mkoan,hakika utafurahia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…