Biashara ya kusafirisha petroleum Tanzania

Malumbo wa ngullo

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
3,246
11,011
Habari maswahiba, sio jambo baya tukipeana mawili matatu kwenye fursa na ujuzi wa biashara ili endapo mmmoja wetu atahitaji kufanya biashara hiyo awe na mwanga kidogo.
twende moja kwa moja kwenye mada husika.

Hii ni biashara ninayofanya na inalipa vizuri, na ukiwa unatafuta fursa kwenye Tanzania's Petroleum Industry basi hii ni chaguo lako itakufaa. Kitu kizuri ni kuwa huna haja ya kuhifadhi products kwa ajili ya marketing, ni kuchuukua from depot you suppy to retailers on demand, cash your money and smile to the bank.

FAIDA YA BIASHARA YA PETROL PRODUCTS SUPPLY.
Mahesabu huwaga ni per litre per tuck, ni kwamba.. Tuchukulie Dar es salaam to Mtwara ila bei inatofautiana inategemea na wapi unasambaza, lakini depots today ni 150 per litre, watakulipa Tzs 150 kwa litre 1 kusafirisha kutoka Dar es salaam to Mtwara. na kama utabeba 20,000 litres kwenye lori lako utakuwa una

150 x 20,000 = 3,000,000 Tzs.
ukitoa gharama zote faida ni 2,200,000.
hii ni kwa single trip na endapo ukipata trip 5 kwa mwezi
you earn 2,200,000 x 5 = 11,000,000 Tzs.
Mara nyingi mtaji unarudi ndani ya mwaka 1 hadi 2.

Swala la Tender za mafuta kwa hapa nchini.
Matumizi ya mafuta ya petroleum yanazidi kupanda kila baada ya siku, Na tender zipo nyingi tu hapa nchini kwa mfano mdogo.. Tanzania Kuna makampuni makubwa ya mafuta kama Oilcom, Kbfuel, Afroil, Total, Camel oil, Puma na vingine kibao pamoja na ma clients wao. Tatizo ni kuwa they have minimal trucks to transport petroleum products and satisfy all there stations kwa nchini na nje ya Tanzania na kusapply kwa clients wao hivyo they come out a head, and they pull out people with their own trucks to helps them distribute products .

VITU VYA KUANZIA KWENYE BIASHARA HII.
1).Tafuta Tanker.
Horse ina cost pound 7,000-10,000 = 27 mil + tra tax 23 = 50mil.
Tank atleast usd 10,000.
Kwakuanzia anza na Tank yenye kupakia 20,000 litre size minimum, to be come a large scale supplier get 37,000-50,000 litre tank size.

2). Tafuta Dereva.
Hapo ndo hatari madereva wetu wengi vichwa maji, hivyo kuwa makini chagua mtu mwenye uzoefu na kazi ya udereva angalia na umri pia.

CHANGAMOTO ZA BIASHARA HII YA USAFIRISHAJI MAFUTA.

1).Gari kuanguka/kudondoka.
Kutokana na uzembe wa madereva wetu, rough driving ni bora kutafuta derva mwenye busara ili kukwepa hili.

2). Gari kuwaka moto.
Gari inaweza kuungua kwasababu bidhaa za Petroleum ni rahisi kushika moto,so its better to ensure a trucks and petrol products with a reputable insurance company.

BUDGET YA KUANZA BIASHARA HII KWA GARI 1
Scania/Iveco/Daf/volvo is around 60,000,000.

Tank is around usd 10.000-50,000.= 23,000,000.

Mshahara wa driver............................ 250,000.

Pesa ya matumizi njiani .....................200,000.

Misclleneous...................................... 600,000.

Jumla 83,160,000.00

Ni biashara nzuri sana.. inalipa hope u understand well.
 
biashara nzuri sema mtaji wake mkubwa sana, kwa Mtanzania wa kawaida ni ngumu sana kupata hizo milioni 85. Lakini pia nasikia madereva wanayadondosha malori ya mafuta makusudi baada ya kuuza shehena ya mafuta.
 
Asante mkuu, nasikia biashara ya kusafirisha mafuta huwa hailipwi kwa tripu moja , kwa maana kwamba mmiliki anatakiwa kuwa na cash ya kujisafirisha kwa maana ya kuwa malipo hufanywa baada ya kupiga trip kadhaa,
Kuna u kweli wowote kwenye hilo?
 
biashara nzuri sema mtaji wake mkubwa sana, kwa Mtanzania wa kawaida ni ngumu sana kupata hizo milioni 85. Lakini pia nasikia madereva wanayadondosha malori ya mafuta makusudi baada ya kuuza shehena ya mafuta.
Madereva ni changamoto sana, tatizo ni kuwa wafanyabiashara wwengi hawko fair na madereva wao,lakni ukiishi nao vizuri kama ndugu hawawezi kukufanyia hivyo.
 
Asante mkuu, nasikia biashara ya kusafirisha mafuta huwa hailipwi kwa tripu moja , kwa maana kwamba mmiliki anatakiwa kuwa na cash ya kujisafirisha kwa maana ya kuwa malipo hufanywa baada ya kupiga trip kadhaa,
Kuna u kweli wowote kwenye hilo?
Inategemea una depot Petrol products wapi na unazipeleka wapi na kwa makubaliano ya malipo yapi? pia kuna wengine wana mikataba mara nyingine mkataba unalipwa baada ya miezi 3 kutokana na idadi ya gari zako zilizopiga trip kwenye kampuni husika
 
Back
Top Bottom