Biashara ya dagaa wa nyama

Biashara ya dagaa wa nyama

kinywanyuku

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2015
Posts
3,849
Reaction score
3,065
Wakuu habari za asubuhi,

Naomba kujua anayefanya biashara ya Dagaa wa Nyama wale wa Zanzibar. Vipi, hapa kwa Dar soko lipoje wanapendwa?

Nikitaka mzigo na chukulia wapi kwa jumla na je, mtaji wa laki mbili unatosha?

Nashukuru
 
ukitaka dagaa nyama Mimi nauza mkuu..... npo tanga mjini ila mikoani pia huwa nasafirisha kwa uaminifu mkubwa.... ndoo kubwa ya kg kumi Mimi nauza 55,000 tuu.... naweza pia nkakuelekeza jinsi ya kufunga Kama utapenda... karibu
 
Qurie, Unauzia wapi.. Na ww unaanika au unanua kwa wavuvi mana bei yako kubwa
 
Qurie, Nashukuru mkuu nikichukua ndoo moja mpaka dar je usafiri malipo juu ya nani maana me npo dar
 
Wakuu habari za asubuhi naomba kujua anayefanya biashara ya dagaa wa nyama wale wa Zanzibar vp hapa kwa dar soko lake je wanapendwa? Nikitaka mzigo na chukulia wapi kwa jumla, kwa mtaji wa laki mbili unatosha? Nashukuru
Mkuu hiyo biashara ina lipa lakini mtaji wako mdogo kule znz unanunua kila kg 4500 au 4600 ww huku dar utauza kg 6000
 
Unauzia wapi.. Na ww unaanika au unanua kwa wavuvi mana bei yako kubwa
Mimi nachukulia kwa wavuvi mkuu.... Na hi ndo Bei yake pia
Bei yake huwa inapanda na kushuka kutokana na upatikanaji
 
Nashukuru mkuu nikichukua ndoo moja mpaka dar je usafiri malipo juu ya nani maana me npo dar
Gharama za usafiri Ni juu ya mteja mkuu....
Ni TSH 5000 tuu huo mzigo kutoka tanga Hadi dar...
 
Gharama za usafiri Ni juu ya mteja mkuu....
Ni TSH 5000 tuu huo mzigo kutoka tanga Hadi dar...
Hivi mkuu hawa dagaa dar wanapendwa? Maana naona wanakula sana mchelemchele wale
 
Wanapendwa pia
Mkuu kuna tofauti kati ya dagaa wa nyama na Uduvi na je kwa Tanga gunia la Uduvi linaenda bei gani?Kama nikoTanga Uduvi wanapatikana wapi kwa wingi?
 
Mkuu hapo juu nimekuuliza swali kwa Tanga wapi nitapata Uduvi kwa bei nafuu?Msaada kidogo hapo naona kimya
Uduvi wa vidagaa vya kawaida au uduvi wa dagaa kamba?..taja bei ya vyote possible
 
Uduvi wa vidagaa vya kawaida au uduvi wa dagaa kamba?..taja bei ya vyote possible
Nilikua naulizia bei ya Uduvi wa vidagaa vya kawaida kwa Tanga inakuaje na wapi nitapata kwa wepesi zaidi?
 
Back
Top Bottom