Biashara ya Camp ya watalii

mzeemzima

Senior Member
Apr 14, 2010
122
78
Wadau heshima kwenu,

Nina wazo la kuanzisha camp ya watalii katika barabara kuu za nchi yetu , lengo ikiwa ni kuwa na eneo ambalo ambalo nomadic tourist (wale wanaotembea na magari masafa marefu) watapata mahali pa kupumzikia. Naomba kwa wale wenye uzoefu wa jambo hili wanisaidie ushauri wa vitu kama jinsi ya kupata ardhi , vibali vinavyohitajika , gharama mbalimbali za kuanzia n.k

Asanteni
 
Mkuu wazo zuri sana Sema linahitaji mtaji mkumbwa kidogo.. Kama upo tayari tukae Chini tuone tunaweza shirikiana vp.. Nina mtu anafanya hiyo biasha naamini anaweza akatusaidia..
 
Ni wazo zuri sana tafuta mtu ambaye yuko kwenye hiyo makitu hata matour guides huwa wanakuwaga na wateja.Mi namwona jamaaa yangu mmoja wazungu anawapelekaga kwake kwa hiyo jaribu.
 
Wazo sio baya,unajua Overland trucks ni watu waliojitoa saana.
Na wengi pumzika yao huwa kwenye Magari yao unless wameshuka kwa ajili ya shopping tu.
Fanya uchunguzi wa kutosha saana na wa kina saana.Na hali ya usalama kwa sasa sikushauri uanze hii biashara.
Maana idadi yao inapungua,maaana wengi wa South Africa na Wajerumani,ambapo usalama ukiwa duni basi wanatumia ndege.
So,fanya uchunguzi wa kutosha,usije kukuta unalipia kodi tuu bila biashara.Wale jamaa hata kuoga huwa hawataki,asiee wabishi saana wale Watalii wa kwenye Magari.Hahahaha
Wapo ambao smart,ila kuna kipindi ukute wajerumani waliopinda,aisee wavivu hadi kuoga.Sasa kwenye kutumia ndio kabisaa,wanajua hadi bei ya andazi
 
Mkuu sina uzoefu sana ila nimefanya kazi kwenye utalii wa kawaida na hunting safaris kidogo ,niligundua business opportunity moja ambayo wengi hawajaona .Wengi wanapenda kujenga maghorofa ya kifahari sana mjini kama hotels zinazowagharimu billions with payback period ya zaidi ya miaka 50 .Lakini cheap investment with high return .kuna uhaba mkubwa wa accommodation kwenye hifadhi zetu especially Nothern Circuit.Ukiweza kwenda TANAPA ukaongea nao wakakupa mwongozo jinsi ya kuweka semi-luxury camp itakua nzuri sana na utapata wageni wa kutosha.Unahitaji kama hema 10 (double beds) za wageni ambazo on average zinaweza kugharimu kama 4-6 millions/unit (including their poles),then utaweka na furnitures na kufanya plumbing ili liwe self,then ujenge mess ambayo inaweza kukugharimu kama 20 millions maana unaijenga juu ili wanyama waweze kupita chini na wageni waweze kupata park view nzuri.Unaweka na kitchen tent na hema za wafanyakazi.Utahitaji solar na standby generator na-resupply truck ambayo unaweza kukodi mwanzoni,halafu unanunua zile fridge zinazotumia gas . Tatzizo kubwa ni requirements za Tanapa na vibali vingine kama certificate of TFDA na other certifications na vitu vingine vidogo.Then unaweza ku expand biashara yako taratibu.Hii kitu watu wengi hawaijui na wala hawaioni.
Hizo 10 tents ukiweza rate za $60 /clients na ukawa na occupancy capacity ya 75% June-October,Dec-March, unaweza kutengeneza in that period around $200k ($60x 2pax per tentx 10tentsx 30daysxmonthsx 75% occupancy),ndani ya mwaka na nusu umesharudisha hela zako.Na low season unashusha bei ,and you still make money
Hii naona ni nzuri kuliko kujenga barabarani ambako huna uhakika na wageni
 
Hii pia ni nzuri kwa mazingira kuliko kujenga ma lodge ,na lazima uwe na environmental management plan ,na huwenda watu wa mazingira wakakuomba pia environmental impact assessment.Lakini vyote hakuna kigumu .Hawa wenzetu kutoka ulaya wameshasoma hii biashara muda mrefu wanakuja na dollar laki mbili wanaanza na hema 10,ndani ya miaka miwili anakua na tents 35.Na marketing ya hii kitu si ngumu sio kama na kua tour operator
 
Back
Top Bottom