Short white
Senior Member
- Jan 6, 2011
- 124
- 32
Salaams JF,
Nilipata wazo la kuanzisha bakery maeneo ya Sinza. Products ni ; Mikate, Maandazi na cakes aina mbalimbali. Sikuomba au kutafuta ushauri kwa mtu yeyote. Pia sijafanya research ya uhakika kuhusu mahitaji halisi ya hizo bidhaa ninazotaka kuingiza sokoni. Pia sijafanya utafiti kuhusu ushindani wa hii biashara. Nimeamua kuchukua RISK 100% katika kuwekeza huko kwenye bakery. Kwahiyo bado sijaelewa / sijajua kama nipo njia sahihi au nimekosea. Naomba ushauri na uelewa wenu kwenu hii biashara.
Hadi sasa nimefanikiwa kupata vitu vifuatavyo;
- Machines- 3 Ovens ( moja kubwa inaingiza paltes 6 na nyingine mbili ni ndogo zinaingiza plates 2 kila moja); 1 Mixer aina ya B30; Shelf; 30 Oven Plates,
-Nimepanga Jengo na kulifanyia ukarabati kulingana na mahitaji ya kazi.
-Nimesajili jina la biashara
-Nimeshapata na TIN
-Nimeshapata leseni
Vitu vinavyohitajika kwa sasa ni;
-Connecting service line ( electricity) kwenye jengo ambalo nimeshafanya wiring
-TFDA authorization
-Source of more finance
-Hard working, knowledgeable and skilled person ( Baker) ambaye ataweza kutengeneza bidhaa mbalimbali
-Bread slicer
-Manager and cashier
-Marketing and sales person
-Distributor
Je mnaonaje wakuu? Je nipo sahihi? Nawakilisha
WADAU WENGINE WANAOHITAJI UFAHAMU WA BIASHARA HII
Ndg zangu wanaJF, kwanza poleni sana kwa msiba wa mwanaJF mwenzetu RM iliyotuchukua almost the whole week kuomboleza.
Napenda kusema yote ni mipango ya Mungu na tulio bado hai let us make this world a better place for US and next GENERATION.
Naomba wenye UELEWA na biashara ya BAKERY wanijuze if it is a good business to engage in (is it paying?), tayari ninayo OVEN yenye uwezo wa kutengeneza walau Mikate 20 at once.
Nashindwa kuanza bcoz nimeambiwa lazima niwe na TIN no, LESENI, TFDA, Mazingira masafi etc, so where can i get all these things guyz or is it possible nikaanza bila moja ya hivyo vitu?
Mie ningependa nianze polepole wakati biashara ikikuwa, walau hata nikianza atleast na mikate 50 per day i have NO PROBLEM with that.
Natanguliza shukrani zangu ndg zangu.
Nataka kufanya biashara ya bakery lakini sina hakika kama inalipa au la.
80% ya mikate na bishaa zitakuwa za brown hivyo hatutegemei volumes bali itakuwa ni quality kwenda kwa juu japo itakuwa na bei ya juu kidogo
Naskia kuna wazungu wa Denmark wako Dar wanafanya ila sina hakika jina la bakery yao na kama wanauza sana
Washindani wakubwa wangu ni wale jamaa pale shoppers plaza na pia jamaa wa pale jengo la mkapa. Lakini sisi tutawekeza zaidi kwenye quality, usafi, na niche market ya wasio kula mitake ya white
Je, italipa? na inahitaji kiasi gani?
Wadau habari za leo?
Natamani kufungua biashara ya mikate yaani Bakery hivi karibuni ila sina uelewa kuhusu biashara hii. Hivyo naomba wenye uzoefu mnielimishe gharama halisi zinazohitajika katika biashara hii ikiwa ni pamoja na vifaa/mashine na bei zake, sehemu zinakopatikana/zinakouzwa kwa hapa Tanzania, gharama nyingine za uendeshaji na jinsi ya kukokotoa faida/hasara katika biashara hii.
Asanteni
MICHANGO YA WADAU
Mkuu Hongera sana kwa jitihada zako, mkuu hizi ndo moja ya aidia ambazo zinamshiko mkuu.
- Labuda mimi nikushauri kitu kimoja mkuu,
1. Hii biashara kama ziilivyo biashara nyingine ni lazima ziww zinatambulika na serikari yetu, hii ni pamoja na kuwa na
- TIN NO
- LESENI
- TFDA CHETI
Mkuu huwezi fanya hiyo viashara bila kuwa na hivi vitu na kitu kama TBS kupata nembo yao si kitu cha mchezo mkuu inaweza kukuchukua miaka kama usipo kuwa makini, make hawa jamaa wanataka
- ENEO LA KUOKEA LIWE SAFI
- VIFAA VISAFI
- NYUMBA AMBAYO IMEJITENGA YENYEWE NA HAISHI BINADAMU HUMO NA IWE NA MADIRISHA NA MWANGA WA KUTOSHA
- WAFANYA KAZI WAKO LAZIMA WAVAE MAVAZI MALUUMU
- NA MENGINEYO
Mkuu si kwamba ukitimiza haya ndo utapewa TBS, razima wakapime na hiyo mikate yako na watakuwa wakifanya ukaguzi wa kushitukiza kuona kama unafuata taratibu zote, na hawakuambii siku wanakuja, na wakikukuta umevunja baadhi ya masharti ndo sahau kabisa, itabidi uanze tena mwanzo
MKUU KUHUSU ENEO LA KUWEKA HII KITU,
- Mkuu naamini Dar, Arusha, Mwanza, Mbeya na miji mingine mikubwa kuna viwanda vya kutosha vya mikate, na ukisema uweke Dar, inakuchukua muda mrefu sana kuja kukopinti na watangulizi ambao wameisha kamata soko vya kutosha, na itakuhitaji kuwa na mtaji wa kutosha ili ufanye matangazo na lazima uwe na Distribution chanel za ukweli, so inahitaji capita ya uhakika.
- MKUU SASA UFANYE NINI?
- Mimi ningekushauri fanya utafiti wa kutosha katika miji mingine hapa Tanzania ambayo hakuna kiwanda cha hii kitu, na ukiona kuna demand fungua huko mkuu, ili uweze kukua vizuri, si razima Dar tu.
- Mkuu hata wawekezaji unao waona huku Africa wamekimbia stiff competition huko Ulaya, Marekani na Asia na kuja huku, mitaji yao haiwaruhusu kuendesha biashara huko kwao kwa sababu ya competition kubwa sana
- So hata sisi sometime ili kuepuka kutumia nguvu nyingi kufungua biashara kwenye miji mikubwa ambayo tiyali kuna business za aina hiyo nyingi tunaweza enda mikoani ambako tutatumia capital kidogo na ukisha kuwa unaweza rudi mjini kushindana na hao waliopo
DONDOO ZA MTAJI WA BAKERY NDOGOKuhusiana na Mtaji inategemeana unataka kutengeneza bidhaa gani na kwa kiwango gani kwa siku etc. Mfano kwa minimum hata 3 mill unaweza anaza kwa keki ndogo. Kwa kununua mixeer ya kg 5 kwa laki 9, Oven single deki ya 1.5 then laki sita ikawani pans na ingredients.
Vifaa vinavyohitajika kwa mradi wa bakery yaani unatengeneza wa keki, mikate, biscuits etc ni kama ifuatavyo commercial Oven, mixer mashine, slicer, improver, kabati, Pan/ filling, nozzels and mashine, decorations accesories, neckbag na vingine vidogo vidogo.
Maduka ya vifaa nayafahamu baadhi yako ambayo ni ya vifaa bei rahisi na mengine juu kidogo:
1. Maduka ya vifaa expensive ila vifaa vyao vina ubora wa hali ya juu. Duka la kwanza liko mtaa wa samora avenue inatazamana na PPF house, duka la pili liko posta mkabala na wizara ya sayansi na taknolojia na duka la tatu liko tazara veterani pale Penye petrol station. Haya. maduka vifaa vyao vinatoka UK, Turkey na baadhi ya nchi za Ulaya.
2. Vifaa vya at least bei rahisi ni kutoka China maduka ni moja liko Kariakoo mtaa wa agreey ukimaliza Bakhresa mbele kuja jengo lina hospitali. Pili ni maduka mawili yanatazamana na kituo cha mafuta Bigborn.
Nakaribisha uwanja wa maswali kwa jambo lolote kuhusiana na bakery.
VIFAA UNAVYOHITAJI NA USHAURIHapo kwenye sehemu ya kufanyia kazi (jengo) itabidi kwanza uwaone TFDA wakague kwanza jengo lako.
TFDA wana regulations zao kuhusu ramani na 'ubora' wa majengo ya bakery.
Waone hao ili watembelee jengo lako kabla hujawekeza. Watakuelekeza vizuri.
Ukianza kabla ya wao kuhakiki jengo lako, wakija na kukuta jengo lako halina 'ubora' watafunga bakery yako na kukuamuru urekebishe jego. Hii itakuwa ni hasara na gharama kubwa sana.
TFDA wakishapita, basi kila kitu ni rahisi kabisa.
Vifaa vya lazima kwenye bakery ni hivi hapa:
1.) Mixer (mashine ya kukandia mikate)
2.) Oven ya kuokea mikate
3.) Slicer (Machine ya kukatia mikate)
4.) Proofer (Machine ya kuumulia mikate)
KUTENGENEZA MAANDAZI
Salute wakuu,
Natumaini wote mko poa.. Leo naomba ni-shee na nyie huu mradi mdogo kama jinsi watu wanavyoweza kuuona lkn kwa kiasi fulani unawaingizia watu mkwanja wa nguvu na wanalisha familia kama kawaida, sio lazima wewe uufanye huu mradi, la hashaa.
Ila unaweza kumshauri mtu akaufanya kupitia mawazo haya ama na wewe ukaboresha zaidi {mwisho wa huu uzi nimekuwekea file unaweza kulipakua na kujisomea ama kumuonesha mtu unayetaka afanye huu mradi} haya twende sasa
MRADI WA KUTENGENEZA MAANDAZI
Mradi huu utahusisha utengenezaji wa vitafunwa aina ya maandazi na kuyasambaza maduka mbali mbali kwa ajili ya kununuliwa na wateja. Hivi ni vitafunwa vinavyojulikana na wengi mijini na vijijni.
Vitafunwa hivi hutengenezwa na ngano inayouzwa madukani pamoja na mchangavyiko wa viungo vingine mahsusi. Ni mradi mdogo sana kwa kuutizama lakini kama ukifanywa kwa umakini unafaida kubwa na inaweza hata kumpatia mtengenezaji pesa nyingi.
Usambazaji
Kama nilivyoainisha awali kuwa hii biashara itafanyika kwa kuweka maandazi haya madukani {maduka ya kawaida kwa kuwaomba marafiki na hata kuwa na makubaliano fulani}. Kwa mfano hapa mtengenezaji atakuwa na madeli {makontena} madogo kumi {10 ama pungufu} ambayo kila moja wapo litakuwa na maadazi 100.
Yote haya yata wekwa maduka tofauti tofauti kwa makubaliano Fulani Fulani na muuzaji. Hapa ujanja wa kuweka maandazi ma2 ama ma3 kwa kila deli ili kumpatia muuzani nae atafute kama ujira wake. ama unaweza kutafuta watu/madogo wakawa wanakuuzia mashuleni hasa shule za msingi n.k
Utengenezaji
Maandazi yatatengenezwa na msambazaji mwenyewe kwa mikono yake ili kuepuka gharama kubwa za uwekezaji huu. Vifaa vitanunuliwa humu humu ndani ya masoko yetu ili kuepuka gharama za uzalishaji na kujihakikishia faida kubwa.
Mbinu za kuyafanya yauzike.
Kwa sababu huu ni ujasiriamali makini, sasa ili kuifanya hii bidhaa iuzike ni muhimu kuwa mbunifu. Nazani inaeleweka kuwa vipo aina nyingi ya vitafunwa madukani vizuri tuu lakini ni vema kuyafanya maandazi haya yakauzika mapema na haraka ili kuufanya mzunguko wa biashara uwe mzuri na wa haraka zaidi.
Kwa mfano size ya andazi iwe ya kuridhisha kulingana na gharama za ununuzi wa bidhaa {kuepuka tamaa}, kuweka viungo ili angalau andazi liwe na harufu na radha ya kuvutia, kuweka tui la nazi, maandazi yakae katika hali ya usafi yaani yakae ndani ya deli linalo yaonesha {transparent} lililofunikwa na pia ili kuepuka mandazi yasiwe na unyevu nyevu ni vema deli likatobolewa matundu kiasi ili kupitisha hewa.
Ifutayo ni mchanganuo wa bajeti na mambo mengineyo ya jinsi ya kuifanya hii biashara kuwa na faida kubwa.
Gharama za awali,mchanganuo, faida na changamoto
Changamoto.
Bithaa hii ikiwa sokoni itakutana na bidhaa nyingine kama hizi, kwa hiyo ni vema ubunifu wa hali ya juu ukatumia ili kuifanya biashara hii kuwa ya kipekee na kupendwa na watu.
Mpango na idadi ya mauzo kwa siku,mwezi,mwaka na FAIDA katika mradi.
{WAKUU HAPA NAOMBA M-DOWNLOAD FILE NIMELIWEKA HAPO CHINI NAONA HAPA MAJEDWALI HAYAKAI VEMA}
MWISHO
Uzuri wa biashara hii ni kuwa haiitaji mtaji mkubwa saaaana yani hata laki nne haifiki kwa kuanzia. lakini pia unaweza kubuni mbinu ya kuyaweka maandazi yako mashuleni ambapo kama yakopoa madogo janja lazima wayanunue sana.
MWISHO KABISA
Ukiangalia kwenye hilo file labda kuna hesabu zimekosewa kwa njia moja ama nyingine lkn napenda kuwafungua macho watu waliokuwa wanaichukulia poa hii biashara, labda niwaambie mama yangu mzazi mimi kwa % Fulani kanilea mimi na ndugu zangu wengine kwa biashara ya maandazi.
Sasa wewe mdau ni kazi yako wewe kusuka ama kunyoa. Ikumbukwe huu mradi unaweza kuufaya na vijana wako home hata kama unafanya kazi kwa {DEREVA WA ROLI} ˂≈≈ Usini-quote tafadhali.
Nakaribisha
*maoni
*marekebisho
*matusi hapana {Sikaribishi}
*chochote
Salute Wakuu
VIFAA VYA MUHIMU KUWA NAVYO1. Anatakiwa awe na oven hii kwa ajili ya kuchomea mikate.
2. Anatakiwa awe na mixer hii kwa ajili ya kuchanganya unga.
3. Anatakiwa awe na bread slicer hii ni kwa ajili ya kukatia mikate slesi.
4. Anatakiwa awe na profer hii ni machine kwa ajili ya kuimulia mikate.
5. Anatakiwa pia awe na hand sealing hii machine kwa ajili ya kufunga vibanio katika mfuko baada ya mkate kuingizwa katika mfuko wake.
6. Anatakiwa awe na vibati kwa ajili ya kuekea mikate katika oven.