Biashara: Unamiliki kituo cha Radio?

Biashara: Unamiliki kituo cha Radio?

Radio Producer

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2011
Posts
728
Reaction score
322
Wadau,

Kwa wale wanaomiliki vituo vya radio habari hii inaweza kuwahusu kwa namna moja au nyingine!

Kwa sasa kuna changamoto kubwa sana kutokana na radio nyingi sana kuanzishwa na bado zinaanzishwa hali inayopelekea radio nyingi kushindwa kujiendesha na kuwa radio jina tu.

Kampuni yetu ya Radio Consult LTD tunatoa huduma zifuatazo:-

1. Tunatengeneza mapendekezo ya uboreshaji wa radio yako kuendana na soko la sasa na ushindani wa sasa.

2. Kwa wale wanaotaka kuhire radio zao kwa watu wengine na wao wawe wanapata malipo tu huku radio ikisimamiwa na mtu mwingine, tunawaunganisha na watu muhimu kwa ajili ya suala hili.

Ombi: Usifunge kituo chako cha radio kwa kushindwa kukiendesha kwa vile hakikuzalishii sana. Wasiliana nasisi kwanza tukupe ushauri kabla ya kufikia maamuzi hayo. Gharama zetu daima huwa ni nafuu zaidi.

Email: consultancy@radiotz.com
Mob: 0719970665
 
Leo nataka kuzungumzia hoja kidogo juu ya uendeshaji wa biashara ya radio. Hii itawahusu wanaomiliki radio, au wanaotarajia kumiliki radio hata wanaofanya kazi kwenye radio.

Hali ya sasa.
Tanzania kwa sasa kuna mwamko mkubwa kwa watu mbalimbali kufanya biashara hii ya radio kwa kuanzisha vituo vingi vya radio. Radio kwa sasa zipo zaidi ya 84 hapa Tanzania na bado zingine nyingi zinazidi kufunguliwa. Hali hii inafanya radio nyingi zinashindwa kabisa kujiendesha au kama zinajiendesha ni kwa kusua sua sana ndiyo maana mara nyingi tunasikia watangazaji wakisemwa kuwa wanasotea sana mishahara kwenye ofisi zao na mishahara hiyo ni midogo.

Uchumi wa Radio.
Radio nyingi Tanzania zinategemea uchumi kutoka kwenye
Matangazo
Wadhamini
Kuuza vipindi
Kadi, simu
Maonyesho mbalimbali
Hizi ndiyo njia kuu zinazotumiwa na radio nyingi hapa Tanzania. Mafanikio kwa nyuma yalikuwa mazuri wakati radio zilipokuwa chache. Mauzo kwa baadhi ya radio ndogndogo tu za wilayani na mikoani yalifikia hata mpaka Tshs 50,000,000/= milioni hamsini. Lakini changamoto wamiliki wa radio wakati huo walipata na kutumia pesa bila kuwa na wazo la kupanua biashara zao hizo.

Hali ya sasa imekuwa tofauti kidogo kwa mapato ya radio hizi yameshuka sana na wakati mwingine unakuta radio ndogo za wilayani zinapata mpaka Tshs 2,000,000/= tu kwa mwezi. Sasa kwa pesa hii ni vigumu mno kuendesha radio. Tatizo ni kwamba radio zimekuwa nyingi na kwamba zinagawana tu hayo matangazo na kufanya kipato kiwe kidogo. Pia hakuna ubunifu mwingine zaidi.

Sababu zinazoshusha kipato cha radio.
Kuna mambo mengi yanayoababisha kipato kushuka hapa nitataja machache tu:-

1. Uongozi au utawala. Nimeshuhudia sehemu nyingi sana wamiliki wenye radio wamewapa uongozi watu ambao hawana elimu hata kidogo juu ya masuala ya radio hata ya uongozi. Yaani tu kwa vile ni mtoto wa mjomba basi kapewa uongozi na anaiendesha radio kama anavyopenda. Unatarajia radio kweli izae matunda?

2. Hazina wasikilizaji. Watu wengi siku hizi wanafanya uchunguzi kwanza kugundua kama radio inawasikilizaji wengi ili Tanngazo lake liwafikie watu wengi. Kama una vipindi vibovu huwezi kupata wasikilizaji wengi hata siku moja.

3. Vipindi vibovu na ratiba mbovu.
Radio nyingi zimecopy vipindi kutoka radio zingine jambo ambalo hufanya kusiwe na tofuaiti kati ya radio na radio. Kawaida na kitalaamu huwezi kuanzisha kipindi bila kuwa na andalio la kipindi maalum ambalo linamaeleezo ya wasikilizaji na uhitaji wa kipindi hicho.

4. Hakuna ubunifu katika utengenezaji wa matangazo. Tumekalia kutafuta watu maarufu kama wachekeshaji na kuwapa matangazo watuandalie hali ambayo hupelekea matangazo yetu pia kuwa ya utani hivyohivyo.

5. Coverage ndogo ya radio.
Makampuni makubwa yanayotoa matangazo hupenda kufikia watu wengi kwa wakati mmoja, sasa unakuta radio yako inasikika kilomita 40 tu, ni ngumu kuyashawishi makampuni haya.

Pamoja na mambo mengine mbalimbali.

Nini kifanyike sasa?
Radio nyingi zenye matatizo haya zinahitaji upgrade kwa ajili ya kushughulika na mambo hayo mbalimbali. Kampuni yetu ya Radio Consult LTD inatoa oprtion mbili:-

1. Tunaweza kukurekebishia radio yako na kuiweka kwenye chart nzuri kabisa kwa gharama nafuu ndani ya miezi mitatu.
2. Unaweza kutupa dhamana ya kuendesha radio yako kwa makubaliano maalum tukaisimamia wenyewe kwa kila kitu.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa PM, au email: consultancy@radiotz.com au simu 0719970665

Asanteni kwa leo.
 
Ninayo interest kufungua radio ya burani mkoani sgd. Vp naweza kupata estmated budget ya vifaa na tcra? Nashukuru
 
Estmated budget inategemea na malengo yako unataka radio yenye ubora gani! Ni sawa na kujenga nyumba, mwingine anaweza jenga ya mil 5 na mwingine ya mil50, hapa ni uwezo wa mtu!

rahisi sana niandikie matarajio yako na budget yako kwenye consultancy@radiotz.com halafu mi nitakujibu!
 
Radio Producer inaonekana ni mdau mkubwa kwenye hiyo sector tupe bio ya kazi ulizowahi kufanya kwenye hiyo sector!
 
Last edited by a moderator:
Wadau,

Watu wengi sana kwasasa wanataka kuanzisha radio, mwamko huu ukiendelea hivihivi kwakweli frequency zitajaa sana katika miji mikubwa! Ninachotaka kuzungumzia leo ni hoja ndogo tu kwamba ni nini kinatakiwa kuanza unapokuwa unataka kufungua kituo cha radio:-

1. Kuandaa utaratibu wa kuomba leseni.
Hapa kuna mambo makubwa mawili, 1. Kufanya upembuzi yakinifu (Feasibility Study), na 2. Ni kuandika documents zote zinazotakiwa kwa ajili ya kuambatanisha kwenye maombi ya leseni.

Feasibility Study ni muhimu sana japo radio nyingi hazikufanya. Hii ndiyo itaelezea uhalisia wa mradi wako kwa 100%. Na hii ndiyo itatoa bajeti halisi itakayotakiwa, masuala ya vipindi na wasikilizaji na mambo mengine yote muhimu.

Ukishamaliza hatua hii sasa mengine ni hatua za baadaye zinazofuata. Mnaotaka kuomba leseni kwa ajili ya kuanzisha radio hii hatua ni muhimu sana wakati unaweka sawa mambo mengine. gharama za maombi ya leseni TCRA ni $1000. Na gharama za kuandikiwa maandiko haya na kufanyiwa feasibility study ni Tshs 2,000,000/=

Asanteni.
 
Duuu hizo dola ni nyingi kumbe kwa usajili tu.???

Yeah ni nzuri maana watu walikuwa wanatuma maombi tu ovyoovyo hata kama hawana nia ya dhati ya kufungua radio, walivyopandisha hapa wamebaki wenye nia tu hahahaha (joke)
 
Hiyo $1000 ni kwa ajili ya maombi tu au pamoja na leseni?
 
Nina ndoto hiyo na ni nia yangu tangu mwaka 2010 ya kumiliki Radio Station yenye usikivu wa kiwango cha Radio Free Afrika.

Na kwa kuanza ninatamani covarage yake ijekuwa ni ya mkoa mzima (kama Mkoa wa Mara wote na wilaya zake hivi).

Ninamuomba Mungu mwaka huu kabla haujaisha anifungulie njia za pesa.
 
Back
Top Bottom