Ndugu wamichoso. Nashukuru sana. Kwanza, ni kweli nimesikia kwa wengi uwepo wa tiles zenye nembo za Spain lakini zinatoka China. Binafsi sijathibitisha lakini naamini zipo sokoni. Naomba lakini nijibu points. Bidhaa zetu NI Spanish tiles kwa sababu zinatoka Spain, kutoka viwanda vya Onda na Castellón. Ubora au quality ni za Spain kwa sababu zimetengenezwa Spain. Tena Bidhaa zetu ni za quality ya Kwanza Au daraja la kwanza. Hizo Bidhaa tumezileta kama majaribio ya soko pia kujifunza. Tumewekeza pesa nyingi kuhakikisha ni tiles bora. Kama wewe nachukia Kuziona Bidhaa sokoni za ubora wa chini, sababu wengi wanazinunua na baadaye wanagundua kumbe ni low quality. Wataalamu na mafundi wanajua haraka sana Kupima ubora. Wanaangalia uzito, unene, kama ni rectified au la (za China nyingi hazipo rectified), na Wanaangalia stain, water and slide resistance. Naomba pia nikanushe kabisa sentensi yako "Spain hawatengenezi tiles". Google na utaona tofauti kabisa. Spain wanatengeneza tiles sana, tena takwimu za 2015 inaonyesha uzalishaji wa tiles ni kubwa kuliko za Italy Au Uturuki. Sisi daima tunamshauri mteja kama ni mtu Binafsi (si mkandarasi) aje na fundi mtaalamu wa tiles amhakikishie ananunua tiles za ukweli na si feki. Karibu sana.