Biashara retail shop - groceries, reja reja kama mini supermarket | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara retail shop - groceries, reja reja kama mini supermarket

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ashangedere, Jul 19, 2011.

 1. A

  Ashangedere Senior Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wangudu,

  Nimeona niweke hapa business idea yangu ya kufungua retail shop in one on the medium populated areas hapa dar.

  Nataka kufungua duka ambalo litakuwa na groceries (eg mafuta ya kupaka&kupika, unga, nido kahawa pampers,maziwa fresh, soda mikate, nk)

  Maeneo ambayo nimepanga kufungua ni kwenye barabara kuu katika sehemu ambazo zimejengwa karibuni au zinaelekea maneneo

  yaliyojengeka karibuni, kama mbezi, kimara, afrikana, tank bovu njia ya goba etc..

  mara nyingi wanaishi watu ambao ni proffessionals, unakuta wana kausafiri na familia na wanaishi katika nyumba zao binafsi, watu hawa kwa

  mtazamo wangu ni wateja wazuri wa groceries wakati wakiwa wanarudi kutoka kazini wanaweza pita na kununua mahitaji, vipi great thinkers

  mnaonaje kuhusu hii idea yangu? mimi pia ni muajiriwa na ni mteja mzuri wa aina hiyo ya maduka na nimefanya kasurvey kangu

  nimeshagundua eneo zuri. Mnaonaje kuhusu hii business na kwamba nitaweka watu na sio mimi nitakuwa dukani, mimi nitakaa siku za weekend

  tu. Nawakilisha.
   
 2. A

  Ashangedere Senior Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sorry I meant wandugu.
   
 3. u

  ureni JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu biashara hiyo ni nzuri lakini faida yake ni ndogo sana hata siku moja huwezi kutoka kwa biashara hiyo,hapo sanasana utapata hela ya kula tu, kama utaweka na vivywaji kama bia unaweza kupatapata kidogo,halafu kitu ulichoharibu kabisa uliposema utaweka watu ndio nimesita kidogo manake biashara za sasa hivi kama uko siriaz unahitaji kusimamia mwenyewe na familia yako manake kama unasema kuweka watu baki basi utakua unataka kutajirisha watu wengine,ndio maana unakuta wahindi wanatajirika sana manake hata siku moja hawafungui biashara na kuacha watu hapo wao wakaendelea na shughuli nyingine,wanafungua biashara baba,mama watoto wote wanakua madirector wanasimamia biashara zao,lakin ukisema unafungua duka halafu unaachia watu unakwenda kazini utakua unatajirisha wengine na biashara hiyo itaqkufa mara moja.
   
 4. u

  ureni JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu biashara hiyo ni nzuri lakini faida yake ni ndogo sana hata siku moja huwezi kutoka kwa biashara hiyo,hapo sanasana utapata hela ya kula tu, kama utaweka na vivywaji kama bia unaweza kupatapata kidogo,halafu kitu ulichoharibu kabisa uliposema utaweka watu ndio nimesita kidogo manake biashara za sasa hivi kama uko siriaz unahitaji kusimamia mwenyewe na familia yako manake kama unasema kuweka watu baki basi utakua unataka kutajirisha watu wengine,ndio maana unakuta wahindi wanatajirika sana manake hata siku moja hawafungui biashara na kuacha watu hapo wao wakaendelea na shughuli nyingine,wanafungua biashara baba,mama watoto wote wanakua madirector wanasimamia biashara zao,lakin ukisema unafungua duka halafu unaachia watu unakwenda kazini utakua unatajirisha wengine na biashara hiyo itakufa mara moja.
   
 5. A

  Ashangedere Senior Member

  #5
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa mawazo ndugu yangu, hilo nalo neno...
   
 6. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Asha,

  Nafikiri biashara yako lazima iende na vitu kama soda na bia au pombe ambazo zinanunulika sana kwa Tanzania. Pia vyakula vinakwenda sana ila sema upate sehemu utakaponunua kwa bei nafuu na wewe bado uuze kwa bei nafuu. Ila si lazima uige wengine wanafanyaje. Unaweza kuja na mipango mipya na ukaanzisha biashara ya aina ya pekee. Labda tu itabidi ukae sana na kufikiria. Nenda kwenye maduka angalia wengine wanafanya makosa wapi na wewe unaweza wapo kurekebisha.

  Wauza duka wana nafuu zaidi Wanawake. Wanaume watakuliza sana kwani wengi hao hasa vijana huwa kasheshe. Labda uweke vyombo vya kusoma kila bidhaa inayotoka dukani inabidi kuifuta SUMAKU yake vinginevyo inapiga kelele. Nguo wanakuwa na miblastic ambayo inaidi kimashine chake kufungua. Ila hivyo vyombo sasa shida ya umeme utalia. Pia kama kuna Camera na vioo. Ila Counter bado wanaweza kukuliza tu. Itabidi kwa hilo ujipange uone wengine wana solve vipi.

  Kama utahitaji PERFUMES basi niye nauza aina kadhaa kwa bei nzuri sana na natafuta wenye maduka. Ukilinganisha ubora na bei, utakuta kwamba bei yake ni rahisi sana. Karibu sana ukitaka kushirikiana na sisi na kila la kheri katika biashara zako.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Aina ya biashara ni nzuri kama iko sehemu yenye wateja wazuri. Tatizo la biashara ya aina hiyo ni gharama za uendeshaji kuwa kubwa na pia parishable food kutupa huleta hasara. Biashara aina hiyo hata nchi za majuu kinachowaingizia pesa ni tobacco, alcohol na soft drink. Lakini chakula tu wengi hupendelea kununua supper market.

  Kumbuka kivutio cha biashara kama hiyo unatakiwa uwe na commercial coolers kwa ajili ya vinywaji, na baadhi ya vyakula ili kuwa na kiwango kinachohitajika kwa stage ya watu ambao wamekuwa umeeleza. Sasa Umeme huu wa mgao MHHHHHHHHHH
   
Loading...