Miaka ya nyuma kulikuwa na mbanano wa biashara hasa mitaa ya libert na rwagasore. Sasa hivi sio pamepooza sana. Maeneo hayo chumba cha duka kodi ilikuwa 10m na kuendelea leo hii mpangaji wa 3m kwa mwaka hapatikani na bado maduka yanazidi kufungwa.
Nimejaribu kufuatilia sababu mojawapo ni makadirio ya kodi yasiyoendana na uhalisia wa biashara wafanyabiashara wameamua kupunguza biashara na wengine kuhama. Mfano mtu alikuwa na duka lake la mke wake na kijana wake anaamua kuvunja na kubaki na duka moja.
kuanzishwa kwa mikoa ya simiyu na geita kumesababisha kukua kwa biashara katika maeneo hayo na hakuna usumbufu wa maofisa wa serikali kama mwanza.
Askari hasa trafik wa mwanza wamekuwa wasumbufu hivyo wafanyabiashara wameamua kuhama mwanza na kuhamia kahama katoro bariadi na geita ambapo hakuna usumbufu huo. Mfano kutoka mwanza mjini hadi kisesa umbali wa km 20 kuna vituo vya trafik zaidi ya vitano na wote huuliza maswali yaleyale. Zipo kaguzi zinazokatisha tamaa mfano unaambiwa urushe maji ya kusafishia kioo yasiporuka unalipa faini ya elfu 30, sehemu kubwa ya mwanza barabara ni mbovu na za vumbi huto tujitu kuziba ni jambo la kawaida.
Kuna mabus mengi yameegeshwa kwa kukosa abiria kwani wasafiri wengi ni wafanyabiashara ambao hawaji tena kuhemea mwanza. Lipo tatizo la mabus kuzidi uzito mizani jiulize bus jipya kama sabuni continental fresta linazidi mizani huku likiwa halina mizigo na abiria wako nusu? Bus hizi zikifika mizani abiria wanaanza kuswagwa kama mbuzi. Likikanyaga tairi za mbele mnakimbilia nyuma likikanyaga za nyuma mnakimbilia mbele basi tabu tupu.
Tanroad sidhani kama wana ujuzi wa upimaji kazi hii bora ingefanywa na wakala wa vipimo hao ndio waliosomea vipimo na wanajua uzito sahihi na kisheria ndio wenye dhamana ya upimaji uzito wa mizigo na bidhaa