Biashara inayolipa

youzam

Member
Apr 9, 2020
15
45
Watu wengi sana wamekuwa wakitafuta huku na huko kujua ni biashara gani inalipa. Yawezekana wengi hatuelewi maana ya biashara inayolipa. Ukweli ni kwamba, biashara inayolipa ni ile ambayo ina uhusiano chanya kati ya kipato unachopata na matokeo ya kile unachokitoa.

Mfano. Kama wewe ni mwalimu na ukafungua twisheni ukapata milioni 6 kwa mwezi, na mwisho wa siku wanafunzi wako wakafeli, basi hujaanzisha biashara inayolipa. Ili iwe biashara inayolipa, ni lazima wanafunzi wako wafahuru, maana kuwa, lazima kuwe na uhusiano chanya wa moja kwa moja kati ya pesa uliyoingiza na matokeo ya kile ulichokifanya.

Kuna mtu atanambia kinachoangaliwa ni pesa. Hapana, pesa si kila kitu. Ukweli ni kwamba, biashara yoyote inayoanzishwa kwa lengo la kuangalia pesa mwisho wake huwa inakufa. Kinyume chake ni kwamba, kama biashara yako ukianzisha kwa kuangalia ni matokeo gani wateja wako watapa kulingana na pesa wanayokupa, basi hapo utakuwa umeanzisha biashara itakayodumu na kukua haraka sana.

Hii ni kwasababu, watu wanahitaji kupata ufumbuzi wa matatizo yao. Mtu akipata ufumbuzi wa tatizo, haoni shida kutoa pesa yoyote ilimradi tu apate bidhaa au huduma inayokidhi mahitaji yake.

Ushahuri wangu ni kwamba, katika biashara unayofanya, hakikisha unaweka mteja wako mbele na pesa nyuma, hapo ndipo utakuwa na biashara inayolipa na haitakufa. Tutajifunza zaidi namna ya kuanzisha biashara inayolipa kwa muktadha wa hii post.
 

youzam

Member
Apr 9, 2020
15
45
biashara bila ubinafsi na ubahili uwezi fanikiwa{inabidi uumize watu wengine ili wewe uwe juu}
najua walio wengi watapinga hii ila huu ndo ukweli
Biashara inayovutia wateja siku zote itadumu kwa muda mrefu na ndiyo biashara pekee tunayosema inalipa. Maana yangu ni kwamba, ili wateja wavutiwe na biashara yako, lazima utoe bidhaa au huduma ambayo wanaihitaji kwa wakati huo na kama wanahitaji.

Basi watakuja wengi tu na biashara yako itafanya vyema. Lakini ukisema uumize wateja wako ili wewe uwe juu basi utasababisha wateja wako wakimbie na utapoea sokoni.
 

youzam

Member
Apr 9, 2020
15
45
Hivi hii biashara ya mashine inalipa?
Inalipa endapo watu wako tayari kulipa ili kupata hiyo bidhaa. Kama ukiona watu hawako tayari kulipia bidhaa yako, basi hiyo biashara hailipi na inaweza ikawa ni kwasababu umeipeleka kwa watu wasio na uwezo wa kuinunua au watu wasio na uhitaji.

Ushahuri wangu ni kwamba, itangaze bidhaa yako kwa watu sahihi unaohisi wanauhitaji wa bidhaa hiyo ili isikae muda mrefu sokoni. Mfano. Kama bidhaa hii ukiipeleka kwa akina mama wenye kipato cha kati au cha juu, uwezekano wa kununuliwa ni mkubwa zaidi kuliko ukipeleka kwa akina baba au wanawake wenye kipato cha chini.
 

Njopino

JF-Expert Member
Apr 8, 2014
3,473
2,000
biashara bila ubinafsi na ubahili uwezi fanikiwa{inabidi uumize watu wengine ili wewe uwe juu}
najua walio wengi watapinga hii ila huu ndo ukweli
Umenena vyema,
Business is all about looking opportunity and exploit it to maximum (James Arthur) otherwise ufungue charity centre.

Ili uuze (knowledge, skill au product) lazima usome customers mind, u presss business in customers centred approach, and use every sh. to invest and save.
All in all, biashara inayolipa ni ile inayokutengenezea pesa nyingi (za kutosha)
 

Sewezymills

Member
Jan 11, 2020
5
45
Biashara inayovutia wateja siku zote itadumu kwa muda mrefu na ndiyo biashara pekee tunayosema inalipa. Maana yangu ni kwamba, ili wateja wavutiwe na biashara yako, lazima utoe bidhaa au huduma ambayo wanaihitaji kwa wakati huo na kama wanahitaji.

Basi watakuja wengi tu na biashara yako itafanya vyema. Lakini ukisema uumize wateja wako ili wewe uwe juu basi utasababisha wateja wako wakimbie na utapoea sokoni.
Hakika
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom