ContentCreator
Senior Member
- Sep 2, 2020
- 151
- 233
Jana Waziri wa Viwanda na Biashara ametunga amri inayozuia wageni kutoka mataifa ya kigeni kufanya baadhi ya biashara kama zilivyoainishwa kwenye amri hiyo. Amri hiyo imetungwa kupitia kifungu Cha 14A(2) Cha Sheria ya Leseni za Biashara yaani Business Licencing (Prohibition of Business Activities For Non-Citizens) Order GN No. 487A 2025 ambayo imeanza kutumika kuanzia tarehe 28 Julai 2025.
Baadhi ya biashara zilizozuiwa kufanywa na wageni ni pamoja na Biashara ya uwakala wa mitandao ya simu, biashara ya kuongoza watalii, kununua mazao shambani, biashara za mashine za kubashiri, udalali wa nyumba, clearing and forwarding, Viwanda vidogo, uchimbaji mdogo wa madini n.k
Aidha amri hiyo imeweka adhabu kwa atakayekiuka mashariti ya amri hiyo ambapo mfanyabiashara wa kigeni atatozwa faini isiyopungua Sh. Millioni 10 au kifungo cha miezi 6 na kunyanganywa kibali cha ukaazi na Visa yake kutenguliwa.
Mtanzania atakayemsaidia raia wa kigeni adhabu yake ni faini ya Sh. Millioni 5 au kifungo cha miezi mitatu jela.
Kwa upande mwingine wafanyabiashara wa wageni waliokuwa wanafanya biashara zilizozuiwa na amri hii wataendelea kufanya biashara hizo Hadi pale Leseni zao zitakapoisha muda wake. Baada ya hapo hawataruhusiwa kuhuisha (renew) leseni hizo.
Amri hiyo inatokana malalamiko na kukithiri wafanyabiashara wa kigeni wanaofanya biashara mbalimbali ambazo zingeweza kufanywa na wazawa na pia ripoti ya wafanyabiashara wa kigeni iliyokabidhiwa kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Selemani Saidi Jafo Machi 18, 2025 jijini Dar es Salaam.
Je maoni yako ni yapi unadhani amri hii itafuta kabisa utitiri wa wafanyabiashara wa kigeni wanaofanya biashara zinazopaswa kufanywa na wazawa?