Biashara hii ihalalishwe ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara hii ihalalishwe ??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Mar 20, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Mar 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu zanguni
  Jana Usiku kuna maeneo nilipata nafasi ya kutembelea baada ya kusikia habari za kutatanisha kuhusu maeneo haya kwanza nilifika kimboka by night pale Buguruni Sheli , Nilipotia mguuu tu upande wangu wa kushoti mbele niliona wasichana umri kuanzia miaka 16 mpaka 20 wakija mbele yangu wamevaa nusu uchi wananiuliza kama nahitaji huduma ya msichana pale , niliposema ndio nikaulizwa nataka aina gani ya msichana baada ya hapo nikaulizwa nataka kwenda nae wapi manake wote wako pale , swali la mwisho ni kama nataka wale wa kinga au si kinga yote haya ni maamuzi yangu mimi mwenyewe kama nataka kinga au la .
  Kilichoendelea hapo siwezi kuendelea kuandika hapa kwa sasa lakini wahusika watilie macho eneo lile baada ya hapo nikaenda zangu kinondoni karibu na makaburini hapo nilikutana hata na wakina mama wako wanajiuza wanauliza kijana unataka huduma gani una bei gani gesti ziko jirani tu ukiwa na pesa zako twende kama hutaki jimama basi wana vitoto vyao navyo viko mjini kwa biashara hiyo .
  Nikaamua kwenda kabisa makaburudi kule napo ni balaa tupu utazikuta kuna watu wenye heshima zao tu wanapaki magari wanashuka kwenda kuokota msichana pale wanamwingiza ndani ya gari lake ana maliza haja zake basi msichana Yule anashuka wengine huwachukuwa kwenda nao starehe sehemu mbali mbali kasha wanawarudisha mahali pale usiku ule ule au kesho yake inategemea na makubaliano yao .
  Safari yangu ya mwisho ilikuwa ni mitaa ya sinza katika bar moja inaitwa kona kuna wasichana pale warembo nao wako katika biashara hiyo wengi wao ni wanafunzi toka chuo cha ustawi wa jamii kijitonyama , hawa ni wasichana ambao baadaye wanaweza kuajiriwa kushika nafasi nyeti katika serikali , makampuni binafsi na mashirika ya ummah hawa hawa ndio customer care wetu katika makampuni ya simu wako kule wanajiuza .
  Nyumba nyingi sana za wageni mitaa ya sinza zimegeuzwa madanguro kwa siri haiwezekani ukute wasichana wamekaa tu mbele ya nyumba hizi bila kazi maalumu na muda mwingi wako hapo hapo , utaweza kujiuliza wanafanya kazi hapo ? kama ndio hawana muda wa kupumzika ? au kama ni wageni tu wanapesa za kuweza kuishi kuishi miezi katika nyumba hizo nani ana wafadhili chanzo cha pesa hizo ni wapi kama sio biashara hii ya kujiuza ?
  Najiuliza mfano unapokutana na customer care wa kampuni kubwa pale anajiuza unawaza huyu analipwa bei gani katika kampuni yake – au katika kampuni hizo hakuna vitengo vya kusimamia maadili ya watu hawa kuwafunza na kuwaonya kuhusu mambo mengine ya kidunia hawa ni vijana size yetu lazima kampuni hizi , wizara hizi na mashirika haya yawe na njia za kuhakikisha wanalelewa vizuri haswa katika maisha yao banafsi tunapokutana na wadada hawa sehemu hizi tunatilia hata mashaka utendaji wao wa kazi katika sehemu husika .
  Kuna wakati wanaofanya biashara hizi kukamatwa na jeshi la polisi lakini inapofikia wakati wa kupelekwa mahakamani basi ndio mwisho wa kesi baadhi ya askari hao wanaundugu na wasichana hawa wanapesa pesa basi wanafuta kesi zao au kufanya hujuma zingine kuhakikisha hawapelekwi mbali zaidi ya vituo hivyo vya polisi
  Kama kweli huwa wanapelekwa na kufungwa kungekuwa na mifano hai ya wasichana hawa au wanaume hawa wanaojihusisha na biashara haya , kama jeshi la polisi limeshindwa kupambana na biashara hii , kama wazazi na walezi wameshindwa kudhibiti watoto hawa kufanyike kitu mbadala basi kuhakikisha jamii yetu inakuwa salama dhidi ya biashara hii .
  Katika nchi zilizoendelea biashara hii imehalalishwa , wanatambulika na wanalipa kodi kuongeza mapato ya serikali , hata huku kwetu tunaweza kuhalilisha lakini kwa sharti la umri na kuhakikisha afya zao ziko salama pamoja na mambo mengine ya kisheria
  Nasema ihalalishwe kwa sababu mitaani watu wameshahalalisha watunga sheria wetu ndio wateja wakuu katika biashara hizi , wafanyakazi wetu ndio wateja pia , walimu , na watu mbali mbali kwanini wasitambulike basi wakishatambulika wapimwe kuw ana umri Fulani wa kufanya biashara hii na wawe na maeneo maalumu ya kufanya biashara hiii

  Sio kama sasa mtoto miaka 15 nae yuko na dada yake miaka 18 wote wanajiuza , mama zao nao wanajuza lazima kuwe na utofauti Fulani
   
 2. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu Shy, mbona utachoka ukiamua kufuatilia haya mambo? Muulize Makamba yaliyomkuta alipojaribu kuwafukuza mitaani, mbona walimbadilshia kibao kwamba na yeye ni mteja wao tu tena wa siku nyingi? Akili zako kichwani, kama ni kuhalalishwa mbona ni kama tayari kwa hao wanaowachukua kwenye magari yao tena ya fahari kila usiku unapojiri! Kwanza wa kuhalalisha ni yupi kati ya anayehitaji hiyo huduma na asiye hitaji? Kwa mtazamo wangu ni kama imehalalishwa kwa wanachama wahusika.
   
 3. A

  Audax JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  inasikitisha,serikali na ile wizara ya utamaduni na michezo ipo wapi?
   
 4. S

  Sra Member

  #4
  Mar 20, 2009
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  biashara hii ni tatizo kubwa sanaaa katika jamii, maana huzalisha yatima wengi sana siku hadi siku. Ombi langu ni kutolewa kwa elimu kwa wanaume juu ya athari zake kwa maana wao ndio wahusika wakuu.
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ngoja na sisi tukafanye "independent review" ya data zako, umesema ulianzia Buguruni Sheli sio?....
   
 6. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inaleta matatizo kwa sababu ipo ipo tuu...

  Holland biashara hii ni halali na imewekewa mazingira mazuri kabisa.Yapo maeneo maalum.Wafanya biashara wanapimwa afya zao mara kadhaa kila mwaka(kama kumbu kumbu zangu ziko sawa ni once in three months).Wanatozwa kodi na hakuna kudhulumiana malipo.Makahaba wanalindwa na sheria kama wanavyolindwa walipa kodi wengine.No gloves,no ride!

  Kwa Tanzania,ni bora mazingira mazuri yawekwe halafu ihalalishwe.Hata tukijifanya hatuioni,ukweli ni kwamba ipo sana na inafaanyika kiholela(Shy anasema aliambiwa achague kavukavu au kutumia mpira!What the hell?!)

  Usiri na unafiki huu wa wimbo wa maadili maadili umetugharimu(angalia jinsi AIDS ilivyoingia na sasa hali ikoje),unatugharimu na utatugharimu hadi hapo tutakapo amua kuwa wa kweli kwa nafsi zetu na wenzetu.

  Wala kufanya jitihada za kuiua ni kupoteza muda.Yawekwe mazingira mazuri:minimum age,afya,minimum payment,maeneo maalum,....yote yawe kwa mujibu wa sheria.

  Ha ha haaa wanaume ndio wahusika wakuu..ajabu kabisa.Mjadala huo hautatusaidia.Nafikiri tujikite kwenye 'issue' yenyewe:biashara ya ngono na mazingira yake.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Rafiki Shy,
  Bila shaka pale uliposema siwezi kusimulia yote nimekuelewa. Je ulifaidi? naamini kuzunguka kote kule ukutoka bure lazima na wewe ulikuwa victim wao LOL maneno yako mwenyewe yamekukaanga:D:-D:-D
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tupo pamoja mkubwa. Kimsingi kunanjia nyingi za kupambana na matatizo. Serikari zote duniani hutumia kodi (tax) kama njia ya kuzuia matumizi makubwa ya huduma fulani. Pamoja na imani zetu nzuri, na maadili yetu mazuri katika swala hili naunga mkono liwe legalized. Hii ni underground economy na kama alivyosema BabaJ, Holland wanamitaa safi ''Red Street''. Na kuna mwaka sector hii Holland iliongoza kwa mapato ya kodi. Hivyo basi kwakuwa hatujafanikiwa kuikomesha ihalalishwe na serikari iweke kodi na watu hawa wapewe leseni na walazimishwe kufanya biashara hii katika maeneo husika ''ofisini kwao'' nadhani hili watalifurahia zaidi. Nchi nyingi tu swal hili ni legal, hapa UK kuna makampuni yanaitwa ''Escots Agencies'', vilevile independent escots, na normal prostitute centres maarufu kama ''massage centres''. Tanzania, may think of legalizing it.
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Umasikini na kuharibika kwa maadili katika jamii ndio sababu,ukitatua hayo utapunguza tatizo,bila hivyo ni kujisumbua maana huwezi kumfukuza mwenye njaa asitafute chakula bila wewe kumpa chakula.
   
Loading...