BIANCONELLI 0-3 ROSONELLI...forza Dinho

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
8,790
Likes
842
Points
280

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
8,790 842 280
Torino - Italy...

Kiungo anayeaminika kusakata kabumbu la mbinguni Ronaldo Assis de Moreirra almaaruf kama Ronaldinho Gaucho alifanikiwa kuifungia klabu yake kipenzi ya AC Milan magoli mawili kati ya matatu dhidi ya wajukuu wa Bibi Laverchia Signorra klabu ya Juventus.

Alikuwa ni beki wa kati anayeaminika kuwa bora zaidi duniani Alesandro Nesta aliyeipatia klabu yake bao la kuongoza.
Hadi mapumziko ubao ulisomeka 0-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila upande kupeleka mashambulizi langoni mwa wapinzani na ndipo Ronaldinho alipopata nafasi ya kufunga kwa kichwa cha ajabu.

Ronaldinho aliyeonekana mwenye kujiamini zaidi alifunga goli la 3 na kupeleka msiba kwa klabu ya Juve ambayo ilionekana wazi kuzidiwa na watoto wa waziri mkuu.

Katika mechi hiyo tulishudia kiungo anayeaminika kumimina majalo yenye upako zaidi duniani yaani David Beckham akicheza dk zote 90.
Huku mashabiki wa Juve wakihangaika kuchoma viti vya uwanja wao kwa hasira.

FORZA MILAN.
 

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
8,790
Likes
842
Points
280

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
8,790 842 280
Ina maana bibi kizee kagaragazwa Stadio Del Alpi ?? Scudetto ambitions naona zinaota mbawa.
Kapigwa 3 kwake na kwa hasira washabiki wakaanza kuchoma moto siti.
Teh teh baada ya goli la 3 star Dinho akamkumbatia na kumbeba star Becks...hakika Milan ni nyumba ya nyota
 

Belo

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2007
Messages
11,718
Likes
4,908
Points
280

Belo

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2007
11,718 4,908 280
Naona Milan wanaanza kurudia enzi zao ,Tusubiri tu Ferara kutimuliwa
 

Forum statistics

Threads 1,190,580
Members 451,229
Posts 27,675,890