Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 5,581
- 10,110
#UPDATES Kodi ya michezo ya kubahatisha imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 131.99 kwa mwaka 2020/21 kufikia Shilingi bilioni 260.21 mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 97.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma , GBT, Daniel Ole Sumayan ambaye ameongeza kuwa kupitia ukuaji huo fursa za ajira katika sekta ya michezo ya kubahatisha zimekuwa zikiongezeka kila mwaka. Hadi kufikia mwezi Juni 2025, ajira zilifīkia zaidi ya 30,000 ikijumuisha ajira rasmi na zisizo rasmi.
Kwa upande wa uwekezaji wa nje (Foreign Direct Investment) umefikia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 66.7 kimeingizwa nchini kutoka kwa wawekezaji wapya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
"Moja ya faida za Sekta ya Michezo ya kubahatisha ni namna ilivyoratibiwa vema na kustawi na hivyo kuchangia ipasavyo katika maendeleo nchini”, amesema.
Ametaja faida ambazo zimepatikana ni pamoja na makusanyo ya kodi yanayofikia Sh.Bilioni 922.95, na kuanzishwa kwa Bahati Nasibu ya Taifa ambayo inatarajia kuongeza mapato ya Serikali. Sekta hiyo pia imechangia Sh. Bilioni 53.8 kuendeleza michezo nchini sambamba na wawekezaji kutoka nje wa Sh.Bilioni 66.7.