Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,411
Kwa wale wote wanaotetea Beting kama BIASHARA HALALI, nasema siyo. Na haijalishi kama serikali imeruhusu au la, swala ni kwamba hii siyo biashara halali kwa sababu zifuatazo;
1. Hakuna thamani inayotengenezwa. Biashara yoyote halali na yenye manufaa kwa kila mtu, kuna thamani ambayo inatengenezwa. Hivyo kuna kubadilishana fedha kwa thamani. Una njaa unakwenda kwa anayeuza chakula, unampa fedha anakupa chakula, hapo kuna thamani imebadilishwa. Sasa niulize thamani gani inatengenezwa kwenye beting?
2. Beting inawadanganya vijana kwamba zoezi la kupata fedha n rahisi sana, ukae tu na kubashiri matokeo halafu unapata fedha nyingi. Fedha haijawahi kuwa rahisi kiasi hicho, na hapa tunatengeneza taifa la watu wavivu, wasio tayari kuweka juhudi kubwa kwenye kazi inayozalisha thamani. Badala yake wanatafuta njia ya mkato ya kupata fedha, ambayo siyo ya uhakika.
3. Hakuna juhudi zozote mtu anaweza kufanya kwenye beting kuongeza uwezekano wa yeye kupata anachotaka. Kwa mfano kama wewe unauza nguo, na biashara siyo nzuri, unaweza kuongeza juhudi zaidi kwa kuwafikia wateja zaidi ili kuuza. Au unaweza kuongeza bidhaa nyingine kuongeza mauzo. Lakini kwenye beting hilo halipo, ukishatabiri timu A itashinda, huwezi kuingia uwanjani kuhakikisha inashinda, unabaki tu kuombea ishinde, na maombi siyo mkakati wa kupata unachotaka.
4. Beting ni wizi wa kihalali. Anayebashiri na kupatia, anapewa fedha, lakini jiulize hizi fedha zinatoka wapi? Zinatoka kwa wengine ambao wameshindwa. Kwa hiyo kwa kifupi, beting ni kukusanya fedha kwa watu wengi, kuwapa wachache na nyingine ikawa faidia kwa anayechezesha hiyo betting.
5. Beting inaleta uteja, mwanzoni watu huanza taratibu na kuona ni kitu kidogo tu, baadaye wanajikuta wamekuwa wategemezi wa beting na hawawezi kuacha. Inafika hatua mtu anaiba ili aende akabet, au anauza vitu vyake cya thamani ili apate fedha ya kubet.
Nimalize kwa kuwashauri vijana wenzangu kwamba betting siyo biashara halali, na wala siyo mkakati wa kupata fedha. Fedha zinapatikana kwa kufanya kazi, inayoongeza thamani kwa wengine. Kuruhusiwa kwa hii beting na serikali hakuifanyi kuwa halali, kwa sababu mara nyingi serikali huwa haioni madhara ya vitu hivi kwa haraka, yenyewe inafurahia kukusanya kodi. Kwenye nchi nyingine beting inafanyika kwenye maeneo maalumu, kwa sababu inachukuliwa kama sehemu ya starehe na siyo mkakati wa kutengeneza fedha. Ila hapa kwetu beting inafanyika kila mahali, mpaka mtaani kabisa, na mpaka watoto nao wanabet. Nasema kwamba biashara hii ina madhara makubwa kwa taifa kuliko faida ambazo watu wanaziona juu juu.
Kwa kijana yeyote mwenye akili timamu, nashauri achana na mchezo huu, na yeyote unayemwona anacheza, mshauri aache. Peleka akili na nguvu zako kutengeneza biashara ambayo itawasaidia wengine na itakuwezesha kutengeneza kipato cha uhakika, unachoweza kuongeza kama ukiweka juhudi. Acha kutumika kuwanufaisha watu wengine.
Kocha Makirita.
www.amkamtanzania.com