Betting na Forex ni kitu kimoja?

Betting na Forex ni kitu kimoja?

Nakubaliana nawe kwamba speculation siyo jambo baya lenyewe, na pia halipo kwenye Forex pekee. Linapatikana kwenye hisa, Crypto na masoko mengine ya kifedha. Hilo halina ubishi.

Hata hivyo, hoja yangu siyo kulaumu speculation wala kusema kwamba kila mtu anayefanya Forex anafanya betting. Ninachojaribu kuonyesha ni kwamba kuna kufanana kwa namna maamuzi yanavyofanywa katika speculative Forex trading na Betting.

Katika mazingira yote mawili, mtu:

1. Hukusanya na kuchambua taarifa zilizopo.
2. Hutumia taarifa hizo kutabiri matokeo ambayo bado hayajatokea.
3. Hufanya uamuzi akiwa na taarifa zisizokamilika.
4. Huweka fedha kwenye hatari akitarajia kupata faida.
5. Anaweza kupata faida au hasara, hata kama amefanya uchambuzi mzuri.

Kuwa strategic ni muhimu, lakini strategy haiwezi kuondoa uncertainty wala kuhakikisha ushindi. Unaweza kufanya uchambuzi sahihi kwa kutumia data zote ulizonazo, lakini matokeo yakawa tofauti na matarajio yako.

Pia, tusisahau kwamba risk management, probability na discipline ni muhimu kuliko kuamini tu kwamba una strategy nzuri. Soko linaweza kubadilika kutokana na taarifa za kiuchumi, kisiasa na matukio ambayo hukuweza kuyatarajia.

Kwa hiyo, sikatai kwamba speculation ni sehemu ya masoko ya fedha. Hoja yangu ni kwamba tunapaswa kutambua kufanana kwa mifumo ya kufanya maamuzi chini ya uncertainty, bila kupuuza tofauti za kisheria, kiutendaji na kiuchumi kati ya Forex na Betting.
Mkuu kwani kuna kitu unaweza fanya bila kufanya analysis na ku predict the future outcome mfano ukitaka kufungua kiband cHa wakala uoni unahitaji kufany both analysis and analytics ili uweze ku predict the unknown does it make to same as betting?
 
kusema Crypto inatabirika kuliko Forex ni hoja ambayo pia inahitaji mjadala.

Kumbuka, Crypto na Forex zote zinahusisha masoko ya kifedha, mabadiliko ya bei (price movements), demand and supply, pamoja na risk.

Kwenye Crypto pia, mtu anaweza kutumia historical data, charts na technical indicators kutabiri kama bei itapanda au kushuka. Lakini hakuna mfumo unaoweza kuhakikisha matokeo hayo kwa asilimia 100.

Kwa hiyo, swali langu ni hili: Kama kwenye Forex tunatumia data kutabiri mwenendo wa bei, na kwenye Crypto tunafanya hivyo hivyo, ni nini kinachofanya Crypto iwe inatabirika zaidi kuliko Forex?
Kwanza crypto kila kitu kipo wazi pia kweli kutabiri kwamba bei itashuka au kupanda inaweza kuwa vigumu kidogo ila kiashiria chenye nguvu zaidi ya kutambua mwelekeo wa bei ni TAARIFA.
Kujua kama bei inashuka au inapanda na wapi bei ikifika inaweza kushuka au kupanda ni rahisi kidogo.
Volume unaiona upande gani imejaa, unaona ni wapi palipo na oda nyingi kubwakubwa(whale orders) hapo mara nyingi bei huwa inageuka, hebu angalia hiyo screenshot....
Screenshot_20261115-090245.png

Hizo ni whale orders, katika maeneo ya bei ya 64,288 inaweza kuwa vigumu bei kuvuka hapo kuelekea chini, na hata ikivuka kuna uwezekano mkubwa bei ikifika pale ita bounce kwanza.

Crypto ni tofauti kabisa na forex ambayo trade yeye anachoona ni bei tu, mengine yote yamefichwa.
 
View attachment 3710249

Kwaio kupitia izo whale orders una make money 100% ?
 
Mkuu kwani kuna kitu unaweza fanya bila kufanya analysis na ku predict the future outcome mfano ukitaka kufungua kiband cHa wakala uoni unahitaji kufany both analysis and analytics ili uweze ku predict the unknown does it make to same as betting?

Mkuu, ni kweli kila biashara inahitaji analysis na forecasting ili kutathmini future outcomes. Lakini kufanya prediction hakumaanishi kila shughuli ni sawa na betting. Tofauti ipo kwenye chanzo cha mapato, thamani unayozalisha na aina ya risk unayobeba. Kwa mfano, kibanda cha uwakala kinatoa huduma halisi na kupata commission, wakati betting inategemea kuweka dau kwenye matokeo yasiyojulikana.
 
Kwa uwakala na upata hela kupitia wateja vipi kama hutapata wateja biashara itaendelea kuwepo si itakua hasara so ni betting na yenyewe
 
Mkuu, ni kweli kila biashara inahitaji analysis na forecasting ili kutathmini future outcomes. Lakini kufanya prediction hakumaanishi kila shughuli ni sawa na betting. Tofauti ipo kwenye chanzo cha mapato, thamani unayozalisha na aina ya risk unayobeba. Kwa mfano, kibanda cha uwakala kinatoa huduma halisi na kupata commission, wakati betting inategemea kuweka dau kwenye matokeo yasiyojulikana.
Kwa wakala kupata wateja ni.matokeo unayoyajua na unahakika nayo kwamb lazima nitapata wateja?
 
Kwaio kupitia izo whale orders una make money 100% ?
Je umesoma maelezo yangu vizuri ukaelewa?
Unajua maana biashara? mfanyabiashara yeyote unamjua wewe hu-make money kwa 100%? jambo lolote katika maisha yako linalokuingizia kipato huwa unafanikiwa kwa 100% sawa na matarajio yako?
 
What is the difference then if there is no certainty in anything
 
Back
Top Bottom