Kunasiku nimepiga simu redioni ku-request ngoma. Nikaomba Bongo hiphop ya Fid. Kipind hiko ndo imetokatoka. Jamaa yangu mmoja anajikutaga mjanja wa mjini alisikia ile call.
Nilivokata simu, jamaa akaja. Ananidiss. eti na ujanja wangu woote nachangua ngoma ya Fid Q. Nashindwa kuchagu mapini ya akina flani flani, anantajia rappers wa huko ma mbele.... Nilimshusha vyeo, nikamwangaliaaa, nikanyamaza. Wakati huo Dj redioni akapress-play request yangu. Nika pump up the volume nikaanza kuvibe na chupa la Ngosha.
Kunawatu wanajiona kwa kushabikia ama kufuatilia mziki wa mbele wao ndo wajanja. Sisi tunaopenda mziki wa hapa ndani ndo mafala beyond repair.
Ukimwambia nitajie rappers wakali wa5 unao wakubali, ndo akutajie akina kendrick, kina eminame sijui, yaani hapo sasa ndo mjanja yeye. We ukisema utupie BONTA pale, rapper wako unae mkubuli ndo atakuona booya wakufikia, mshamba huna unajokijua.