Bernard Membe: Nina maadui 11, ikifika 2016 watakimbilia Kenya!

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,919
2,798
Katika kipindi cha Dakika 45 ITV Mh Membe anaonekana kuongea kwa hisia na uwazi sana kuhusu maisha yake ya kisiasa pamoja na mvutano uliopo kati yake na mahasimu wake.

Anasema iko siku atawataja peupe kwa majina na sura zao. Nauona undani wa Membe hapa.

He seems to be innocent amidst wolves. Tuombe siku ifike na yeye afunguke.
 
Ni leo katika ITV...

Mheshimiwa Membe ameahidi kuwa wale wote wanaomzushia kashfa, wako 11 na kati yao wawili ni waandishi...siku yao ikifika, atawataja hadharani peupeeee!!!!

Kwa sasa anakusanya data za kila mmoja wao, kisha atatengeneza dosier ya kila mmoja wao na finally atawataja kweupeee.

It is interesting..sijui wanarudia lini hiki kipindi...please don't miss it if you can.
 
akiongea kwa machungu sana kwenye kipindi cha dk 45, waziri wa mambo ya nje, Bwana B Membe amesema kuna watu wanamuandama sana, lakini ameapa kwamba wakae tayari, kama ataoteshwa basi 2016 watakimbilia kenya.

amesema anafanya kazi ya kukusanya data ili akiwaanika kwenye vyombo vya habari wakose cha kufanya.

akiongelea zile pesa za libya ameongea kwa ukali sana, amesema ni pesa iliyopatikana kihalali kabisa, kesi ilipelekwa mahakamani na meis wakashinda!
 
Vilaza siku zote wanawaza maadui wao kama watu.

Vipanga siku zote wanawaza maadui zao kama ideas.

Ndiyo maana ukimsikia mtu kama Nyerere akiongelea maadui anaongelea umaskini, magonjwa na ujinga. Wengine wanakwambia maadui watakimbilia Kenya.

Kama huu ndio uongozi wenyewe, basi tunarudi nyuma.
 
nilipo bold mkuu umenikumbusha mbali sana wakati tunasoma shule ya msingi somo la Uraia hayo maneno yalikua kwenye syllabus za enzi hizo
 
If Hon Member you would have been a President, I would have never ever missed your speech. I tend to like you more as I keep on listening to number of your talks and presentations including your arguments in the past on the media on various issues. I do admire you ability to argue issues without necessarily reading, but talking your mind, carefully choosing your words, identifying strong points and picking out important wisdoms to present and yet you make a lot of sense.
 
akiongea kwa machungu sana kwenye kipindi cha dk 45, waziri wa mambo ya nje, Bwana B Membe amesema kuna watu wanamuandama sana, lakini ameapa kwamba wakae tayari, kama ataoteshwa basi 2016 watakimbilia kenya.

amesema anafanya kazi ya kukusanya data ili akiwaanika kwenye vyombo vya habari wakose cha kufanya.

akiongelea zile pesa za libya ameongea kwa ukali sana, amesema ni pesa iliyopatikana kihalali kabisa, kesi ilipelekwa mahakamani na meis wakashinda!
meis wakashinda nini?maana ni pesa za kujenga kiwanda cha cement lindi,jee kiwanda kimejengwa?mimi nina ushahidi membe na meis wamegawana pesa hiyo!atueleze pesa zipo wapi kwa sasa?zinafanya nini?
 
Mh anasema wabunge wapinzani ni wasemaji hodari wa kusema bungeni lakini kwenye majimbo yao hawajafanya chochote?
 
Vilaza siku zote wanawaza maadui wao kama watu.

Vipanga siku zote wanawaza maadui zao kama ideas.

Ndiyo maana ukimsikia mtu kama Nyerere akiongelea maadui anaongelea umaskini, magonjwa na ujinga. Wengine wanakwambia maadui watakimbilia Kenya.

Kama huu ndio uongozi wenyewe, basi tunarudi nyuma.
Kiranga,'
Umesahau kitu kimoja. CCM ya sasa si CCM ya ideas. Ni CCM ya personalities na kuwindana. Imekuwa hivi tangu 2005, ukikumbuka jinsi Kikwete alivyopata urais kwa kuwapaka tope akina Salim. Watajinasuaje na hili? That is a million dollar question
 
jamaa anasema mgomo wa madokta hauna impact kimataifa na anasema madokta wawe na moyo kama wa viongozi wa dini wanaotegemea sadaka... naona leo leo yupo kiitikadi zaidi naona kama hapendwezi na tabia ya upinzani.,.... forms kama za vijembe maana alimesheni kuwa mtu anayemuita rais ni dhaifu hapaswi kuvumiliwa... anasema watu waheshimu mamlaka... lazima mamlaka iheshimiwe
 
Back
Top Bottom