Mh. Membe ndani ya ITV ktk kipindi cha dak 45, akilalamika jinsi maadaui wake walivyomsingizia kuwa kaiba pesa za walibya. Amesema ana wabaya wake 11 ambao ndani yake yupo Mohammed Enterprises, wahariri wawili na baadhi ya vigogo wa CCM. Amesema kuwa aliwasaidia chakula vijana wa CHADEMA waliokuwa na njaa, lakini akatafsiriwa vibaya na maadui zake. Kuhusu urais 2015 amemtaka mtangazaji amsalie sana. Ameomba wanachi wasimlalamikie rais kwa hali mbaya ya nchi (ingawa hajasema ni nani wa kulalamikiwa). Anaamini CCM itaimarika baada ya uchaguzi wa Chama mwaka huu. Amewabeza wabunge hasa wa upinzani kwa kusema sana bungeni wakati bajeti bi ya CCM. Amewasifu baadhi ya madaktari kwa kurudi kazini na akasema huo ni wito, na watumikie wito huo walioitiwa na Mungu kwani malipo yao yapo Mbinguni. ndo anamalizia mahojiano kwa kututaka tuheshimu mamlaka ya nchi.