Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,817
- 71,266
Akiwa anahudhuria kumuaga mwana habari nguli Marehemu Dilunga, Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Bwana Bernard Membe amesema Serikali inayozuia Uhuru wa habari itakuwa Serikali dumavu.
Hilo ni Jiwe gizani, tusubiri atakaye twangwa na hilo Jiwe lazima atapiga ukelele wa nywiiii!
Lakini pamoja na maji kuhorojeka Membe amedhibitisha ni chuma tofauti na hawa vibenten Nape na January.
Mh Benard Membe Waziri wa Mambo ya nje Mstaafu wa serikali ya wamu ya nne akizungumza Jambo na Mbunge wa Mtama Mh Nape Nnauye Mara baada ya ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Jamhuri Godfrey Dilunga jijini Dar es Salaam leo
---
Membe amesema, Uhuru wa vyombo vya habari ni sawa na mbolea inayowekwa kwenye mche. Bila uhuru wa vyombo vya habari serikali inakuwa serikali dumavu. Afya ya serikali zote duniani inatoka kwa waandishi wa habari.
Waandishi wa habari nawaomba muwe huru kufanya kazi zenu bila uoga , mseme ukweli ili nchi hii iende inapotakiwa kufika bila uoga
======
Dar es salaam. Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Bernard Membe amesema Serikali inaweza kuwa dumavu endapo haitaruhusu uhuru wa vyombo vya habari Tanzania.
Membe ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 19, 2019 wakati shughuli ya kuaga mwili wa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Godfrey Dilunga (43) katika viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanahabari, viongozi wa serikali, pamoja na wanasiasa mbalimbali.
Dilunga aliyefariki dunia Septemba 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu ya homa ya tumbo.
Akitoa salamu zake za rambirambi mbele ya wanahabari hao, Membe amesema Dilunga ameondoka akiwa anastahili heshima ya Taifa kupitia kazi yake ya uandishi wa habari.
"Siku hii tunapomuaga Dilunga, itukumbushe uhuru wa vyombo vya habari, kazi ya uandishi wa habari ni sawa na mbolea, unapoiweka katika mche inachipua."
"Bila kazi ya vyombo vya habari, serikali itakuwa dumavu, vyama vya siasa havitakuwa na afya," amesema Membe
Mwananchi