Bernard Membe: Bila uhuru wa vyombo vya habari, Serikali itakuwa dumavu

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,794
71,212
Akiwa anahudhuria kumuaga mwana habari nguli Marehemu Dilunga, Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Bwana Bernard Membe amesema Serikali inayozuia Uhuru wa habari itakuwa Serikali dumavu.

Hilo ni Jiwe gizani, tusubiri atakaye twangwa na hilo Jiwe lazima atapiga ukelele wa nywiiii!

Lakini pamoja na maji kuhorojeka Membe amedhibitisha ni chuma tofauti na hawa vibenten Nape na January.
FB_IMG_1568896198939.jpg

Mh Benard Membe Waziri wa Mambo ya nje Mstaafu wa serikali ya wamu ya nne akizungumza Jambo na Mbunge wa Mtama Mh Nape Nnauye Mara baada ya ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Jamhuri Godfrey Dilunga jijini Dar es Salaam leo

---

Membe amesema, Uhuru wa vyombo vya habari ni sawa na mbolea inayowekwa kwenye mche. Bila uhuru wa vyombo vya habari serikali inakuwa serikali dumavu. Afya ya serikali zote duniani inatoka kwa waandishi wa habari.

Waandishi wa habari nawaomba muwe huru kufanya kazi zenu bila uoga , mseme ukweli ili nchi hii iende inapotakiwa kufika bila uoga

======

Dar es salaam. Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Bernard Membe amesema Serikali inaweza kuwa dumavu endapo haitaruhusu uhuru wa vyombo vya habari Tanzania.

Membe ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 19, 2019 wakati shughuli ya kuaga mwili wa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Godfrey Dilunga (43) katika viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanahabari, viongozi wa serikali, pamoja na wanasiasa mbalimbali.

Dilunga aliyefariki dunia Septemba 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu ya homa ya tumbo.

Akitoa salamu zake za rambirambi mbele ya wanahabari hao, Membe amesema Dilunga ameondoka akiwa anastahili heshima ya Taifa kupitia kazi yake ya uandishi wa habari.

"Siku hii tunapomuaga Dilunga, itukumbushe uhuru wa vyombo vya habari, kazi ya uandishi wa habari ni sawa na mbolea, unapoiweka katika mche inachipua."

"Bila kazi ya vyombo vya habari, serikali itakuwa dumavu, vyama vya siasa havitakuwa na afya," amesema Membe

Mwananchi
 
Akiwa anahudhuria kumuaga mwana habari nguli Marehemu Dilunga, Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Bwana Bernard Membe amesema Serikali inayozuia Uhuru wa habari itakuwa Serikali dumavu.

Hilo ni Jiwe gizani, tusubiri atakaye twangwa na hilo Jiwe lazima atapiga ukelele wa nywiiii!

Lakini pamoja na maji kuhorojeka Membe amedhibitisha ni chuma tofauti na hawa vibenten Nape na January.View attachment 1211532
Mbobezi.....
 
Hakuna kipindi napenda kama kipindi cha kukaribia na uchaguzi kila neno utalisikia wajuvi wa mambo wana sema siasa ni kama upepo CCM ninacho wakubali wana sigana kwenye kampeni usishangae kumuona Membe ana zunguka na chopa kumpigia kampeni Magu apite tunzeni hii comment..
 
Ugomvi wa Vyombo kabatini hauangushi Kabati
 
Horace Kolimba alikuwa Katibu wa Chama tawala Chama cha Mapinduzi akakitukana Chama chake kuwa kimekosa dira na Mwelekeo, Baba wa Taifa pamoja na Rais wa wakati huo Mzee Mkapa walikwazika sana na maneno yale wakamwita Dodoma ajieleze....Story yangu imeishia hapo
......mbobevu akikumbuka hilo akiitwa kwenye kikao atataka iwe Video conference.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
......mbobevu akikumbuka hilo akiitwa kwenye kikao atataka iwe Video conference.

Video conference si sawa na CCTV Camera?

Sept 7 zilisaidia chochote kule Mji mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa watu wa Visiwa vya Fiji?

Ukimaliza kusoma niambie nifute hii comment yangu kwa kuwa Mkojo wangu nauhitaji kwa matumizi yangu binafsi sio ya Jamhuri
 
Horace Kolimba alikuwa Katibu wa Chama tawala Chama cha Mapinduzi akakitukana Chama chake kuwa kimekosa dira na Mwelekeo, Baba wa Taifa pamoja na Rais wa wakati huo Mzee Mkapa walikwazika sana na maneno yale wakamwita Dodoma ajieleze....Story yangu imeishia hapo
Kwa hiyo Membe nae mnataka Kumkolimba?
 
Akiwa anahudhuria kumuaga mwana habari nguli Marehemu Dilunga, Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Bwana Bernard Membe amesema Serikali inayozuia Uhuru wa habari itakuwa Serikali dumavu.

Hilo ni Jiwe gizani, tusubiri atakaye twangwa na hilo Jiwe lazima atapiga ukelele wa nywiiii!

Lakini pamoja na maji kuhorojeka Membe amedhibitisha ni chuma tofauti na hawa vibenten Nape na January.View attachment 1211532

Huyu sijui anajiamini nini wakati ' dossier ' yake ipo ambapo miaka yake Mitano ya mwisho kuna ' Kashfa ' moja anayo kutoka nchi moja ya Kiafrika iliyo jirani sana na Italy ambapo Watu wakiamua tu ' Kumuanzishia ' inakula Kwake na wengi wenu humu ' Wanafiki ' watupu mtamuacha peke yake akitaabika. Namuonea mno huruma kwani ' anatapatapa ' mno huku akitafuta sababu lakini anasahau kwamba Nyumba aliyoiacha siyo ambayo ipo sasa. Atakuja Kujuta na ajitafakari sana na asije Kusahau ' Kiapo ' chake.
 
Video conference si sawa na CCTV Camera?

Sept 7 zilisaidia chochote kule Mji mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa watu wa Visiwa vya Fiji?

Ukimaliza kusoma niambie nifute hii comment yangu kwa kuwa Mkojo wangu nauhitaji kwa matumizi yangu binafsi sio ya Jamhuri

Upo sahihi Mkuu ,wakikutaka kwenye 18 zao hauchomoki.Ila haya yana endelea/endelezwa kwa Sababu ya wanao salia kuwa waoga.
 
Back
Top Bottom