Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,825
- 3,021
Jasusi Limepiga hodi mbwa wameufayata, hahahaaa..... kumbe Membe ni hatari, yanayosema.huenda yakawa ya kweli.Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya awamu ya nne Bernard Membe amevunja ukimya na kumshangaa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dk. Bashiru Ally kwa kukalia kimya barua yake ya wito.
Akizungumza na RAI nyumbani kwake mwishoni mwa wiki, Membe alisema:
“Nilituhumiwa na Katibu Mkuu Dk. Bashiru Ally kuwa ninaihujumu Serikali ya Awamu ya Tano na kunitaka nifike ofisini kwake kujibu tuhuma baada ya kudai hana namba yangu ya simu.
“Na mimi kwa kumheshimu Katibu wangu wa chama tarehe 7, Desemba mwaka jana nilimpelekea barua kwa dispatch (ushahidi) na kusainiwa nikimuomba kunipangia siku, muda na tarehe ya kufika kwake lakini cha kushangaza ameendelea kukaa kimya.”
Aidha, Mwanadiplomasia huyo amedai kushangaa kusikia kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole kuwa mjadala huo umefungwa rasmi.
“Nimemsikia Polepole kupitia Radio Clouds akisema ‘mjadala wa Membe umefungwa rasmi.’ Sasa ninamhoji ni yeye aliyeuanzisha mjadala huo hadi aufunge? Lakini pia kulikuwa kuna mjadala rasmi wa Membe?”
Akizungumza katika kipindi cha ‘Power Breakfast’ cha kituo cha Radio Clouds cha jijini Dar es salaam, Polepole akizungumzia masuala mbalimbali ya chama hicho alipoulizwa sakata la Membe na Bashiru limefikia wapi alijibu kwa msisitizo, “naomba niwaambie Watanzania na wana CCM kuwa mjadala wa Membe umefungwa rasmi.”
Membe aliendelea kusema: “Nilitegemea baada ya Katibu Mkuu kunitaka nifike kwake angefanya hivyo maana hata nilipotaka mtuhumu wangu mkubwa Bwana Mussiba (Cyprian) naye awepo Katibu Mkuu alinitaka nisimuwekee masharti, nikakubali kukutana naye bila huyo Mussiba ili nijibu mapigo.
“Hata hivyo, huyo mtuhumu wangu tayari nimemfungulia kesi Mahakama Kuu nikimtaka athibitishe kauli yake dhidi yangu kupitia gazeti lake la Tanzanite au anilipe sh 10 Bilioni kama fidia ya kunichafua.”
Aliongeza kuwa; “Baada ya tarehe 7 Desemba kumekuwepo na vikao vya juu kama Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na hata Kamati ya Maadili ambavyo vingetumia nafasi hiyo kujadili suala hili ambalo kwangu mimi na wana CCM wenzangu si dogo maana unapomuona simba anakukimbia usidhani uko salama, jaribu kumpa mgongo uone, utajikuta umeraruriwa vipande vipande, na hivyo kama kuniita kumeshindikana kwa nini nisihisi kuna ‘plan B’ na hivyo nichukue tahadhari?”.
Aidha, RAI lilimtafuta Dk. Bashiru ili kuzungumzia iwapo ameipokea barua hiyo na Membe na lini atampangia kumuhitaji, lakini kila alipotafutwa kwa njia ya simu hakupokea wala kujibu ujumbe mfupi.
Hata hivyo, RAI lilifanikiwa kuzungumzia na Polepole ambaye alisema suala hilo kwa upande wake halifahamu wala hajui kama kuna barua yoyote imeletwa na Membe.
Hata hivyo, katika mazungumzo yake na gazeti hili kuhusu ukimya wake, Membe amesema; “ninajua Watanzania wangependa kusikia ninaongea, nitaongea baada ya kukutana na Katibu wangu Mkuu Dk. Bashiru Ally akinipangia siku na saa ya kukutana.”
Bernard Membe afunguka | Gazeti la Rai
Hahaha eti Membe hajajitokeza hadharani kuunga mkono juhudi za mwenyekiti,.kwani ni lazima??
Jiandae kulipa bilion 10.Kwa hiyo, kwa sasa Membe amekuwa mtu wa kuwashawashwa anapeleka kwenye vyombo vya habari kuwa hajaitwa ili aitwe, siyo?
Mimi nilidhani anajiamini so ya nini kulialia kuwa hujaitwa? Umeshakiweka mchanga kitumbua though.
Tarehe 21 Jan, kuitikia wito ndivyo CAG alivyosema.!!Hivi na yule CAG anaenda lini kwa Subwoofer.?
Vikaragosi kama vile vya mchawi kalaba😂😂😂Nani anataka kumuunga mkono kichaa kwenye udikteta wake, wizi, dhuluma na udhalimu? Hakuna MC bali ni hao vikaragosi vyake.
Sidhani kama JPM anamuogopa huyo Jasusi mstaafu