Benzi la Daniel Arap Moi lililoibwa Kenya lakamatwa Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benzi la Daniel Arap Moi lililoibwa Kenya lakamatwa Arusha

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by mwanaizaya, Dec 15, 2008.

 1. m

  mwanaizaya Senior Member

  #1
  Dec 15, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Benzi la Daniel Arap Moi lililoibwa Kenya lakamatwa Arusha
  Na Hemed Kivuyo,Arusha

  WIZI wa magari katika ukanda wa Afrika Mashariki, sasa umekithiri baada ya wezi kuiba gari aina ya Mercedes Benz linalomilikiwa na rais mstaafu wa Kenya, Daniel Arap Moi.


  Kuibwa kwa gari hilo ni moja ya matukio makubwa ya aina yake ya wizi hasa kutokana na ukweli kuwa rais huyo mstaafu bado ana ulinzi.


  Duru za habari za kuaminika kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoani hapa zinasema Benz hilo lenye rangi nyeusi ambalo namba zake za usajili zimehifadhiwa, lilipatikana mkoani hapa likiwa limehifadhiwa kwa mmoja wafanyabiashara maarufu.  Kwa mujibu wa duru hizo za habari, gari hilo lilipitishwa mpakani Desemba 10 mwaka huu na watu wasiofahamika na kwamba polisi wa nchini Kenya walikuwa katika jitihada za kulikamata hata hivyo, hawakufanikiwa.


  Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Matei Basilio, alipoulizwa juu ya taarifa hizo, alisema jeshi la polisi halina taarifa za kuibwa benz bali gari liloibwa Kenya na kuingizwa Arusha ni aina ya Toyota Land Cruiser.


  Kamanda Basilio alitaja gari hilo kuwa ni lenye namba za usajili ambazo sio halali akizitaja kuwa ni T118 AVZ, ambalo mmiliki wake bado hajafahamika.  Kamanda huyo alisema gari hilo lilipatikana baada ya kampuni moja maarufu inayojishughulisha na utafiti juu ya magari ya wizi baada ya kugundua kuwa gari hilo lina vifaa vingi ambavyo sio halali hivyo kushikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa uchunguzi zaidi.


  Kamanda huyo alifafanua kwamba watu watatu wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi na kuwataja kwa majina kuwa ni pamoja na Halidi Juma Marik, Abdulnuru Meena, George Munisi na Adrian Mariwa.


  Alisema Mariwa bado anashikiliwa na polisi huku wengine wakiwa nje kwa dhamana.  "Tunamshikilia Mariwa na wenzake waliopata dhamana na uchunguzi ukikamilika watapelekwa mahakamani hapa Tanzania na kisha kupelekwa katika mahakama ya nchini Kenya," alisema Kamanda Matei.


  Habari zimedokeza kwamba gari lililoibiwa ni la Moi na kwamba lipo Dar es Salaam huku mfanyabiashara mmoja maarufu mkoani hapa akitajwa katika wizi huo.


  Habari hizo zinadokeza zaidi kwamba kufichwa kwa taarifa za wizi wa gari hilo kunatokana na

  masuala ya kiusalama na mahusiano kati ya nchi za Kenya na Tanzania na kwamba uchunguzi zaidi unafanyika kuona mbinu zilizotumika kuiba gari la rais mstaafu
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  UUwi
  I see wewe Munisi, Meena na Mariwa mwataka msee wa watu atumie baiskeli kwa sughuli sake? Mnajua kapisa amesoea kuendeswa ndani ya Penzi lake, sasa ataendaje Limuru na amevaa suti?
   
Loading...