abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
12th May 2012
Benki ya Taifa ya Vijana inatarajiwa kuzinduliwa wakati wowote mwaka huu.
Uzinduzi utafanyika baada ya mchakato wa kufunguliwa kwa benki ya vijana ya taifa kuingia katika hatua za mwisho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM –(UVCCM) Taifa, Martin Shigela amesema.
Alisema hayo wakati akizindua kikundi cha wajasiliamali wa umoja huo katika kata ya Manyoni mkoani Singida.
Alifahamisha kuwa mchakato wa kuanzishwa benki hiyo kupata usajili wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Alisisitiza kuwa taasisi hiyo itawezesha wajasiriamali wa kati na wadogo yakiwemo makundi ya wanawake kujikwamua kiuchumi.
Aliongeza kuwa ni azma ya serikali ya CCM ya kuwawezesha vijana hasa kuwapatia mtaji. Alisema tayari UVCCM ngazi ya taifa imefanya mazungumzo na mifuko ya hifadhi ya Jamii pamoja na taasisi nyingine za fedha ambazo zimeonyesha nia ya kusaidia vijana wakiwemo waendesha boda boda na vikundi vingine.
Awali akisoma risala ya kikundi hicho cha wajasiriamali, Katibu Uhamasishaji wa Kikundi Bahati Matonya alisema kikundi hicho kinakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi zikiwemo zana za kilimo.
Alisema hali hiyo inakwamishwa maendeleo ya shamba la kikundi lenye hekari zaidi ya 200 na kumuomba Katibu Shigela kusaidia kupata wafadhili.
CHANZO: NIPASHE