Benki ya posta wezi

sebeco

Member
Joined
Apr 18, 2013
Posts
19
Reaction score
1
Kuna tukio moja la ajabu limetokea katika benki ya posta; kuna jamaa amekuta pesa yake wame withdraw katika akaunti yake akawauliza wakampa benki statement ambayo inaonyesha pesa zime tolewa katika benki fulani kupitia umoja switch cha ajabu hakuna transaction iliyo fanyika kwenye ile benki.

Kilicho baki ni kuanza kuona haibu tu ooh! andika barua mara pesa yako ipo.

Rai yangu kwa hii benki ni kwamba itakosa wateja kama mtindo wao wa wizi utaendele kwani si wote wateja ni wajinga.

KAMA ULISHAPATA USUMBUFU WA KAMA HUU CHANGIA
 
Wale ni wezi wakubwa tu,ukiacha 20000 baada ya mwezi mmoja anakuta salio 0
 
Achana nayo hiyo benki, nakushauri kafungue akaunti uswisi kama wenzako walivyofanya. pesa yako itakuwa salama.
 
Wenzio vijsent vyetu tunaweka uswizi kule hakuna kuibiana kamwe
 

Mijitu mingine bwana, heading inavutia nimekimbilia kuona hawa jamaa ambao wanahifadhi vijisent vyangu ni wezi kwa namna gani,lakini nashindwa hata kuelewa uwizi wao uko wapi, unaandika kama unakimbizwa. Tulia rejea mada yako kwenye heading tuelemishe nasi tuelewe au tuangalie namna ya kujihami.

Kuna jamaa amekuta pesa yake wame withdrawal kutoka akaunt yake... hao wezi alipowauliza wakampa Benk statement...ambayo inaonyesha fedha zimetolewa katika benk fulan...kupitia umoja switch...Cha ajabu hakuna transaction iliyofanyka katika benk ile...

Kuna jamaa...kadi yake na namba yake ya siri ana share na nani ? kama kapewa statement ametambua kwamba fedha imechotwa... amethibitisha kuwa kadi yake haikuchukuliwa na yule aliyekuwa anajifanya anampenda sana na kumpana namba ya siri ? zimetolewa katika ATM za umoja switch kwenye benk nyingine,Mmmh sasa mtoaji wa hizo hela ni nani CCTV zinaonesha nani alikuwa anatoa hizo hela ? Hakuna transaction kwenye benk hiyo... akaunti iko benki ya posta,unataka uone transactions za akaunt yako kwenye benk nyingine ?
Acha kukurupuka na kujaza server JF.

Hebu tengeneza vizuri kisa chako kinaweza kuwa msaada kwa wengi wetu, acheni papara...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…