Ally Kombo
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 11,429
- 2,645
Kweli kaka, safi sana kwa jitihada zako za kujifunza sayansi. Hata maembe na miwa pia ina madini yanayopatikana katika udongo. Ila sasa uwe makini sana, usikubali kukaririshwa tu sababu kuna watu fulani wana itikadi na elimu kama hiyo, iliyojaa hadithi na hekaya. Wamekomazwa saana kuamini kitu ambacho hakijakuwepo na labda kamwe hakitatokea. Cha kushangaza ndio watu wa mwisho kisayansi/teknolojia, wanatumaini/kuamini bahati/nasibunasibu tu, kutokuwa pia na maendeleo mengine. Badala yake ni wakomavu kwenye ubishi usio na tija, wakakamavu kwa itikadi fulani, vurugu na kuhangaisha wengine n.k.
Kila la heri kaka na nakutakia siku njema.
Hii ni Biology:
" Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asili ya udongo. Kisha tukamjalia awe tone la mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. Kisha tukaliumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivisha nyama, kisha tukamfanya kiumbe mwingine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu, Mbora wa waumbaji. Kisha hakika nyinyio baada ya hayo mtakufa" QUR'AN: 23:12-15.
Hii ni Geography:
"Na tumeteremsha kutoka mbiguni maji kwa kiasi na tukayatuliza ktika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa" QUR'AN: 23:18
Mwenyezi Mungu anaongelea Ishara (Signs) na Mwanadamu anathibitisha kwa Sayansi (Science)