Benki ya Kiislamu inapataje faida?

Ninachokiona hapa ni baadhi ya watu kutoelewa RIBA/interest ni nini hadi kushindwa kuitofautisha na faida,..
RIBA- Riba ni ada inayolipwa na akopaye mali kwa mmiliki wa mali kama fidia kwa ajili ya matumizi ya mali hiyo.
FAIDA-Ziada inayobaki baada kutoa jumla ya gharama katika mapato.
 
Hiyo bank ni kwa ajili ya waislam tu au? Na mkristo akitaka kupata mkopo au kufungua akaunti anaruhusiwa??
 
Hivi kwa benki za Kikristo/Kiyahudi inakuaje? maana Biblia nayo inakataza riba.

Exodus 22:25 "If you lend money to one of my people among you who is needy, do not be like a moneylender; charge him no interest.

Leviticus 25:35 "'If one of your countrymen becomes poor and is unable to support himself among you, help him as you would an alien or a temporary resident, so he can continue to live among you.

Leviticus 25:36 Do not take interest of any kind from him, but fear your God, so that your countryman may continue to live among you.
 
Mkombozi ina maana wakristo hawaifuati biblia?maana mkombozi bank,efatha bank zinatoza riba kwa wateja
 
Hivyo hidden interest inakubalika maadam isiwe open interest. Unaruhusiwa kuzini mradi umefanya siri, sio kwa vile kuzini ni dhambi hata kama kwenye usiri wa hali ya juu

Lete maandiko, lasivyo wacha uzushi wako!!
 
Chukua hii aya ili ikuweke sawa:
"Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na shetani kwa kumgusa. Hayo ni kwakuwa wamesema; Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba. Qur'an:2:275
" Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba na huzibariki sadaka. Qur'an:2:276

:focus:
 
Ulileta mwenyewe kweli hiyo siyo riba. BUT is this practical. labda kwa wenzetu waarabu, hapa Africa South of sahara, I doubt! Naomba nikuuilze na si kwa mabishano: Mtume (SAW) alikuwa mfanya biashara (biashara means mtaji + riba/faida) sasa kwa nini waislamu wanakataa riba wakati mtume(SAW) alifanya hivyo. nadhani if it were me, ni kutotaka riba ya kuumiza wenzako au wasemaje!

Unalijua unalosema au unaropoka !
Unapata wapi hilo dai la Mtume Muhammad kuchanganya riba na faida.
Biashara ni kununua Gunia la Mahindi kwa Tsh 20,000/- ukaweka gharama zako (Tsh 2,000/-) na kuweka faida (Tsh 3,000) kisha ukauza Tsh 25,000/-
Riba ni kukopesa kwa Mtu (Tsh 20,000/- ) kisha ukatakiwa kurudisha (Tsh 25,000/-) tena kwa muda maalum, ukipita huo, unaongeza pesa zingine !
Mtume alifanya biashara, akitoa bidhaa fulani kutoka Uarabuni hadi Sham na kutoa bidhaa za Sham hadi Uarabuni ! Na ndo maana kulikuwa na misafara (Caravan) hakuwahi kuwa na mafuko ya pesa kukopesha watu !
 
Hii benki ya kiislam ni marketing strategy tu jamani..wanajua kuwa waislam watakuja kuweka pesa basi, kwanza hawana tabia ya kuchunguza sana...lakini wao wanagawana na wewe kile unachopata kama kawaida..hata kama hakiitwi interest

Haya ni mawazo ya kifungwa, kijela jela ! Pole !
 
Mkuu Ally Kombo tafadhali fafanua jinsi bank hiyo itakavyokuwa ina run kupata profit, achana na wanaokejeli kwanza
Je nikikopa nitalipaje
Je nitakatwa bank charges
Je huduma kama fixed account zinakubalika
je vipi huduma kama kuuza na kukua pesa za nje
Nk nk
 
Last edited by a moderator:
Unalijua unalosema au unaropoka !
Unapata wapi hilo dai la Mtume Muhammad kuchanganya riba na faida.
Biashara ni kununua Gunia la Mahindi kwa Tsh 20,000/- ukaweka gharama zako (Tsh 2,000/-) na kuweka faida (Tsh 3,000) kisha ukauza Tsh 25,000/-
Riba ni kukopesa kwa Mtu (Tsh 20,000/- ) kisha ukatakiwa kurudisha (Tsh 25,000/-) tena kwa muda maalum, ukipita huo, unaongeza pesa zingine !
Mtume alifanya biashara, akitoa bidhaa fulani kutoka Uarabuni hadi Sham na kutoa bidhaa za Sham hadi Uarabuni ! Na ndo maana kulikuwa na misafara (Caravan) hakuwahi kuwa na mafuko ya pesa kukopesha watu !

Tungeliweza kuelimishana, lakini nakuona hatutaendana maana umeshasema kuropoka, hilo ni tusi na sidhani kama dini yako imekufundisha hivyo. nakuacha kama ulivyo! Kutukana naweza sana tena sana, lakini kwa heri
 
waislamu tumeharamishiwa riba na 2mehalalishiwa biashara.navyojua mimi all islamic banking wana run inform of business(selling & buying)and not interest basis.wanapataje faida?kwa mfano wewe unaenda kukopa kwajili ya kujenga nyumba yako,unaandika mahitaji yko yote,sasa wao wanande kuvinunua hivo vi2 vyako na wanaweka faida yao kidogo then wanakupatia.kwakifupi wanadeal sana sana na things rather than money.na dini nyingine tafauti ya kiislam wanaruhusiwa kujiunga.nadhani ntakuwa nimeeleweka.
 
Tungeliweza kuelimishana, lakini nakuona hatutaendana maana umeshasema kuropoka, hilo ni tusi na sidhani kama dini yako imekufundisha hivyo. nakuacha kama ulivyo! Kutukana naweza sana tena sana, lakini kwa heri

................nashukuru umeelewa !:whistle::becky:
 
Mkuu Ally Kombo tafadhali fafanua jinsi bank hiyo itakavyokuwa ina run kupata profit, achana na wanaokejeli kwanza
Je nikikopa nitalipaje
Je nitakatwa bank charges
Je huduma kama fixed account zinakubalika
je vipi huduma kama kuuza na kukua pesa za nje
Nk nk

Hii ni elimu kubwa na watu wanasomea mpaka Shahada ya Umahiri (Masters) na Uzamivu (PhD), mie nakupa "basics" tu za Islamic Banking.

Mwenyezi Mungu SWT anasema kupitia Qur'an, 'ameharamisha riba, na amebariki Biashara' ingawa wako watu wasio na Imani wenye kusema, Biashara ni riba !' na Qur'an (Mwenyezi Mungu) ikaongezea kuwa anaekula riba, basi ametangaza vita na Yeye Mwenyezi Mungu pamoja na Mtume wake. (jiulize: inakuwaje Bank ambayo iko "risk free" na inakula riba lakini bado inafilisika ?)

1. Riba ni nini (Interest)!?

Ni kiasi cha juu kinachoongezwa katika kukopeshwa/mtaji, kinacholipwa kwa muda maalum na mtoaji anahakikisha hayuko katika Hatari yoyote ya kupoteza/ au kupata hasara. Mzigo wote wa gharama na uendeshaji (risk) anabeba mkopaji/mpewa mtaji. Mara nyingi hii inahusiana na Pesa Taslim (Cash).

2. Biashara ni nini ?

Biashara (Trading), ni lazima ihusishe kununua na kuuza bidhaa (buying and selling of goods) and reward or difference is profit (margin), hata Biashara ya kubadilisha pesa ina kuwa na profit inayotokana na tofaouti ya mnunuaji au muuzaji anayokubali kuachia !

Bishara ya Bureau De Change ni halali kabisa, kwani muuza pesa ameweka kiwango cha faida (margin) ambacho ni ile tofauti ambayo unakubali kuiachia wakati wa kununua, au unayolipia wakati wa kuuza (Ksh 1,000/= muuza duka ameinunua kwa Tsh 18,000/= na Mtu/Mteja akihitaji hiyo Ksh 1,000/= anaiuza kwa Tsh 20,000/= tofauti ni Tsh 2,000/= sawa na Ksh 100/= ambayo ndiyo ni Faida) Pesa ikishuka thamani ana pata hasara kama Biashara zingine.

Hivyo Bank yenye mfumo wa uendeshaji wa Kiislaam inaweka misingi na kanuni zake katika Biashara,(kutafuta faida) pia inajihusisha na hasara (profit and loss). Wataalamu wake wanajitahidi kuingia na kufanya Biashara kwa faida, ingawa ikipatikana hasara mnakubaliana jinsi ya kuilipa/fidia !

Zipo aina tofauti (products) za kibenki na kanuni na masharti yake kulingana na aina ya Biashara.

" Mwenyezi Mungu huiondolea baraka "riba" na huzibariki sadaka "QUR'AN: 2:276.
 
Chukua hii aya ili ikuweke sawa:
"Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na shetani kwa kumgusa. Hayo ni kwakuwa wamesema; Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba. Qur'an:2:275
" Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba na huzibariki sadaka. Qur'an:2:276

Kiimani upo sahili, lakini uhalisia ni mambo yaleyale, sababu kuna ushauri (ushawishi) wa kidini unaokuomba/kukushauri utoe kiasi fulani cha faida kama zaka. zaka=riba. Na dizaini tu za kuomba hiyo ada ili biashara iendelee.
 
acheni kuwa wavivu wa kufikiri na kuanzisha malumbano yasio na msingi , unapat wapi ujasiri wa kubishiya kitu usichokijuwa wote ambao ufahamu wenu ni mdogo kuhusu islamic finance naomba mtafute material mbalimbali ya islamic finance kwenye internet vinginevyo mtakuwa mavuvuzela ambayo yanapiga kilele .
 
Back
Top Bottom