Benki ya Exim inatarajia kupiga mnada hoteli ya kifahari ya Slim Slim pamoja na samani za kumbi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,281
Benki ya Exim inatarajia kupiga mnada hoteli ya kifahari ya Slim Slim pamoja na samani za kumbi za mikutano vilivyopo Bagamoyo mkoani Pwani baada ya mmiliki huyo kushindwa kurejesha mkopo wa TZS 920 milioni.

Benki ya Exim inatarajia kufanya mnada wa hoteli hiyo maarufu ya Green Park Village siku ya Jumamosi Aprili 22 mwaka huu ambapo watahitaji TZS 2.5 bilioni lakini mmiliki wa hoteli hiyo amesema kuwa thamani ya hoteli hiyo ni TZS 5 bilioni na si bei iliyotajwa na benki. Wakazi wa eneo hilo wanaombea hoteli hiyo iuzwe kwa thamani halisi ili mmiliki huyo aweze kupata fedha za kuendeshea maisha yake kwani hatobakiwa na kitu kingine. Gazeti la The Citizen limemnukuu Slim Slim mmiliki wa hoteli hiyo akisema kuwa, anaamini Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itaingilia sakata hilo ili kuweza kunusuru hali ngumu anayopitia yeye kama mwekezaji kwani serikali iliwaahidi wawekezaji mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

Alisema Hoteli ya Green Park Village ni ndoto yake aliyokuwa nayo siku nyingi tangu alipokuwa akiishi nchini Norway. Hoteli hiyo ina vyumba vya kulala 20, vyumba 7 vya mikutano, na sehemu mbili za mapumziko.“Niliuza kila kitu nilichokuwa nikimiliki nchi Norway na kuamua kurejea nchini mwangu baada ya serikali kutushawishi wazawa tuliopo nje ya nchi tushiriki katika maendeleo ya nchi yetu.” Amesema.
tmp_9856-FB_IMG_1492607239980-750452642.jpg

tmp_9856-FB_IMG_1492607237749-57720638.jpg

tmp_9856-FB_IMG_14926072422702146312859.jpg

tmp_9856-FB_IMG_14926072469872092683380.jpg

tmp_9856-FB_IMG_1492607244597-1372610975.jpg
 
Thamani ya hotel bilioni 5 yeye alikopa sh bilioni 2.5
kama aliuza kila kitu alikopa tena benk ya nini? ila namuombea Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi ni vizuri pia akakaa na benk aendelee na operation za hotel ili arejeshe kidogo kidogo.au kama vipi atafute mjeja amuuzie hyo b 5 awape benk yakwao abakiwe na zingine .
H
 
huyu ni mwekezaji mzawa asaidiwe kwa kuwa hotel inafanya kazi mapungufu yaliyopo yarekebishwa kwani hii si habari nzur kwa benki zetu hapa nchini ,ipo minongono kuwa benki zetu si rafiki wa biashara zetu .pengine ndo haya riba ni kikwazo kikubwa na muda wa kulipa .
 
Leo nimesoma kutoka gazeti la Citizen kuwa Hoteli ya Slim iliyopo Bagamoyo ya Ndugu Slim karibuni itapigwa mnada na Exim Bank.

Inasemekana kuwa tamani ya Hoteli hiyo kwa sasa ni 5bn/= lakini inawezekana ikauzwa kwa 2.5bn/= tu. Madai ya Exim Bank kwa Mr. Slim ni Tshs.900m/=. Huyu Ndugu ni Jamaa aliyekuwa diaspora (Norway) akifanya kazi za ujenzi na akashawishiwa na wakubwa kuja kuwekeza Tanzania na akawekekeza kwenye Hoteli akitegea ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambayo alihahidiwa kuwa ingejengwa kwa haraka na kutokana na Bandari hiyo Hoteli yake isingekosa wateja.Mpaka leo hii Bandari haijajengwa na hata ndoto ya kuijenga ilikwisha yeyuka.

Kwa kweli inasikitisha kwa mtu kumaliza hela zote alizokuwa nazo kwa kuwekeza halafu hoteli inapigwa mnada.

Naishauri Benki Kuu iingilie kati hili suala angalau Exim wamuongezee tena hata miaka miwili ili awarudishie fedha yao.

Mimi pia namshauri Mr. Slim arudi tena Norway akafanye kazi hata kwa miaka miwili ili apate hizo hela kuliko kuuza hoteli yenye thamani kama hiyo.

Pole sana Ndugu yangu Slim.
 
Back
Top Bottom