Benki ya CRDB na huduma mbovu za utoaji wa mikopo

Benki ya CRDB na huduma mbovu za utoaji wa mikopo

kishapu boy

Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
40
Reaction score
85
Ndugu wanabodi,

Mimi ni mtumishi katika Taasisi mojawapo ya Serikali hapa TZ,kama mnavyojua mtu anapoamua kukopa anakuwa na malengo juu huo mkopo ,lakini imekuwa tofauti Kwa benki ya CRDB hasa mtu unapoenda kukopa, leo mie binafsi nimemaliza wiki ya tatu tangu nisubmit documents zangu za kuomba mkopo na nimekuwa napigwa danadana tu oooh subiri mkopo wako unashughulikiwa!!

Kwa wanaojua labda watusaidie ni nn hasa kimeikuta hii benki hadi imekuwa na huduma mbovu namna hii??

Nawasilisha
 
Mimi mwenyewe nilisubirishwa Kwa miezi 3 ili kupata mkopo.Hawa jamaa siyo kabisa.
 
CRDB Kwisha habar Yao hata hiyo 13%ni uongo mtupu wamepandisha pro fee 1% to 2% na kiwango Cha bima
 
Mimi mwenyewe nilisubirishwa Kwa miezi 3 ili kupata mkopo.Hawa jamaa siyo kabisa.
Duh! miezi mitatu si mchezo, kuendana na malengo ya mkopaji ni bora wazingatie tu muda wa masaa 48 au ndani ya wiki moja, maana asilimia kubwa ya watu huwa wana ishu za dharura za kuwafanya ku process mkopo.
 
Crdb yashindwa kutoa mkopo. Hawana mtonyo aka liquidity. Wamekiuka kitu muhm sana kwenye biashara ya pesa.

Kifuatacho
Wataongeza mashart,
Watapandisha riba kama walivofanya kwenye bima na ada

Pia muda mzuri wa kukmnpa ni sep to may.

Jun, july na aug kunakuwa na watumish kibao wa uma wanataka mikopo kwa sabb madaraja yamepanda au nyongeza ya serikali.

Tukutane 2029 december ili feb 2030 nikavute mkogo wa m15 kwa rate ya leo. Itakuwa imefika T XYZ FCK
 
Ndugu wanabodi,

Mimi ni mtumishi katika Taasisi mojawapo ya Serikali hapa TZ,kama mnavyojua mtu anapoamua kukopa anakuwa na malengo juu huo mkopo ,lakini imekuwa tofauti Kwa benki ya CRDB hasa mtu unapoenda kukopa, leo mie binafsi nimemaliza wiki ya tatu tangu nisubmit documents zangu za kuomba mkopo na nimekuwa napigwa danadana tu oooh subiri mkopo wako unashughulikiwa!!

Kwa wanaojua labda watusaidie ni nn hasa kimeikuta hii benki hadi imekuwa na huduma mbovu namna hii??

Nawasilisha
Walikuwa busy na primary business yao ya Marathon ingawa nayo waliboronga kwenye Tshirts....!!!
 
Hebu ungetaja majina yako matatu na ni mwalimu nani pia uliombea tawi gani ili nione nakusaidiaje.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Arusha Branch kuna jamaa jina linaannza na
E kushia na Er ni shida sana Yule. CRDB imulike hyo Branch.
 
Back
Top Bottom