Benki Kuu (BoT) yaendelea kusisitiza kuwa malipo ya huduma zote ndani ya nchi yanapaswa kufanyika kwa Shilingi ya Tanzania

Benki Kuu (BoT) yaendelea kusisitiza kuwa malipo ya huduma zote ndani ya nchi yanapaswa kufanyika kwa Shilingi ya Tanzania

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
980
Reaction score
3,646
KATAZO LA MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI KATIKA KUFANYA MIAMALA YA NCHINI/MALIPO NDANI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kwamba, kulingana na matakwa ya Kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Serikali imetoa Kanuni za Matumizi ya Fedha za Kigeni za Mwaka 2025. Kanuni hizo zimechapishwa katika Gazeti la Serikali na. 198 la tarehe 28 Machi 2025.

Kwa mujibu wa Kanuni hizo, bei na malipo ya bidhaa na huduma zote ndani ya nchi zinapaswa kufanyika kwa Shilingi ya Tanzania. Hivyo, ni kosa kunukuu, kutangaza au kubainisha bei kwa kutumia fedha za kigeni; kulazimisha, kuwezesha au kupokea malipo kwa fedha za kigeni; au kukataa malipo kwa Shilingi ya Tanzania.

Kanuni hizi pia zimeainisha miamala ambayo imeruhusiwa kufanyika kwa fedha za kigeni. Aidha, Kanuni zimeweka ukomo wa muda kwa mikataba inayotekelezwa kwa fedha za kigeni na kuweka katazo la kutokuingia au kuhuisha mikataba inayotaka malipo yafanyike kwa fedha za kigeni kuanzia tarehe 28 Machi 2025.

Wageni kutoka nje ikiwemo watalii watabadili fedha za kigeni kupitia benki za biashara na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni nchini au kuendelea kufanya malipo kwa kutumia kadi za kielektroniki au utaratibu wa kawaida wa kidigitali.

Benki Kuu inawahimiza wananchi kutoa taarifa za ukiukwaji wa Kanuni hizi kupitia barua pepe: fx.regulations@bot.go.tz, Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Jeshi la Polisi, au mamlaka nyingine yoyote ya utekelezaji wa sheria kwa hatua stahiki. Nakala ya Kanuni imeambatishwa kwa urahisi wa rejea.

Pia soma > Serikali yatangaza Kanuni zinazokataza Matumizi ya Fedha za Kigeni kulipia bidhaa au huduma nchini

BoT.jpg
 
This was supposed to have taken effect circa 2006, when the BoT Act was enacted. But again, the state bureaucracy was hijacked and run by greedy-malevolent thugs.​
 
Back
Top Bottom