Benki gani ni nzuri kwa kufungua akaunti ya mtoto?

The last don

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
989
992
Hello,
Habari marafiki...nadhani nitakuwa sijapotea njia kuomba mchango wenu wa mawazo kupitia jukwaa hili kwani nahisi katika jukwaa hili la mmu ndipo watembeleapo wazazi wengi zaidi kuliko majukwaa mengine.

Ninahitaji kuwawekea akiba watoto wadogo ili ije iwafae katika mambo ya elimu hapo baadae,sasa basi katika kufikia maamuzi haya nahitaji kujua benki yenye kufaa zaidi katika makumi ya mabenki tuliyonayo hivi sasa katika nchi yetu.

Msaada naohitaji ni kuambiwa jina la benki pamoja na aina ya account ambayo napaswa kuwafungulia.

Naomba tafadhali marafiki utajapo jina la benki nijuze walau kwa ufupi faida zipatikanazo katika benki hiyo kwa aina hii ya account ya akiba.

Asanteni sana nawakaribisha kwa mchango wa mawazo na mawazo yenu nitayaheshimu.
 
M' Pesa ayaweee wamekata bora Airtel tehe tehe Castle Milk bwana.Kweli mi pombe ya bure sio mizuri
 
Ina interest kubwa kidogo kuliko savings a/c za kawaida. Haichargiwi chochote, unaweza kuiaccess mara 2 kwa mwaka. Check na watu wa CRDB au tembelea website yao.

Ahsante Kaunga, i will do so. Nataka kuweka akiba ajili ya mwanangu but bado mdogo sana, so nataka bank ambayo inaruhusu mzazi ku access account in case of emergencies. Nitatembelea web as u advised.
 
Ahsante Kaunga, i will do so. Nataka kuweka akiba ajili ya mwanangu but bado mdogo sana, so nataka bank ambayo inaruhusu mzazi ku access account in case of emergencies. Nitatembelea web as u advised.

Mimi niliitumia sana a/c ya mwanangu wakati nafanya saving kwa ajili ya ujenzi. Kwa kuwa huruhusiwi kuchukua pesa zaidi ya mara mbili kwa mwaka ilinisaidia sana. Nilimfungulia alipokuwa ana miezi 6 sasa hivi ana miaka 11 na anajua a/c yake ina sh ngapi.
 
Asante Kaunga na KOKUTONA....vipi kuhusu service charge kwa aina hiyo ya account (CRDB Junior Jumbo) kwani akiba inategemewa kukaa muda mrefu isije ikawa wanakula nusu kwa nusu.
 
Wangu anatimiza 6 pia next month ndo nataka nimfungulie, umenipa mwanga rafiki.
 
@Billie vipi mbona umeogopa na mchango wako mzuri,je udhani kwamba sim banking inaweza kufaa? kwani nadhani hakuna service charge mule hadi utakapo kuwa unataka kutoa pesa.
Hofu yangu katika hizi sim banking ni reliability yake tu kwa kipindi kirefu kijacho.
 
Asante Kaunga na KOKUTONA....vipi kuhusu service charge kwa aina hiyo ya account (CRDB Junior Jumbo) kwani akiba inategemewa kukaa muda mrefu isije ikawa wanakula nusu kwa nusu.

Haina service charges, unaruhusiwa kudraw mara mbili kwa mwaka. Wanapata faida si wanaifanyia biashara kwa miezi 6
 
Haina service charges, unaruhusiwa kudraw mara mbili kwa mwaka. Wanapata faida si wanaifanyia biashara kwa miezi 6
Shukrani kwa mchango wako,nimepata pa kuanzia ngoja niendelee kusikiliza mawazo ya wadau wengine.
 
Nadhani ingekuwa bora kama utafungua account ya forex hivyo thamani ya pesa unayoweka haitaanguka tofauti na madafu yetu ambayo hayako stable
 
Mimi niliitumia sana a/c ya mwanangu wakati nafanya saving kwa ajili ya ujenzi. Kwa kuwa huruhusiwi kuchukua pesa zaidi ya mara mbili kwa mwaka ilinisaidia sana. Nilimfungulia alipokuwa ana miezi 6 sasa hivi ana miaka 11 na anajua a/c yake ina sh ngapi.
kumbe wewe ni mama? aaaaaaaaaaaaaaarg!!!!!
 
Mkuu Kunta Kinte asante kwa mchango wako kiongozi,hebu endelea kufafanua zaidi kuhusu hii account ya forex
 
Last edited by a moderator:
Kiwango cha chini ambacho unaweza kukitumia kufungulia ni kiasi gani? na kiasi gani kinatakiwa kibaki kulea account wakati unapotaka kudraw?

Nimesahau ni long time, huenda ni sh 20,000 kama kianzio. Sijawahi kukwangua hivyo sikumbuki ni kiasi gani unachotakiwa kubakiza.
 
Back
Top Bottom