Benki Azania kutoa huduma kuzingatia kanuni za Kiislam

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670


Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa (kulia), akishiriki hafla ya kufuturisha wateja wa Kiislam wa Benki ya Azania ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano baina ya benki hiyo na wateja wake msimu huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kwa ufupi
*."Tunaamini huduma hii itasaidia kuleta ahueni kwa wateja wetu Waislam. Dhamira yetu ni kuhakikisha wanapata huduma zakipekee zitakazokidhi matakwa yao kikamilifu".

Dar es Salaam. Benki ya Azania imejipanga kuanzisha dirisha la kutoa huduma zinazofuata kanuni na misingi ya Kiislam.
Hayo yalielezwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Singili, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Benki ya Azania, Bernard Haule, kwenye hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake Waislam Dar es Salaam juzi.
Tupo kwenye maandalizi kuanzisha huduma za benki kwa wateja wetu ambao ni waumini wa dini ya Kiislam, baada ya kuanza kutoa huduma kupitia mawakala miezi michache iliyopita, alisema Singili na kuongeza:
Tunaamini huduma hii itasaidia kuleta ahueni kwa wateja wetu Waislam. Dhamira yetu ni kuhakikisha wanapata huduma za kipekee zitakazokidhi matakwa yao kikamilifu.
Alisema benki yake imekuwa ikiandaa hafla za kufuturisha wateja wake Dar es Salaam na mikoa mingine, ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kujumuika pamoja na wateja wake hususan wakati wa Ramadhan.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, aliwaasa Waislam nchini kuungana na kufuata misingi ya dini ya Kiislam.
Waislam inatakiwa tutumie Ramadhan kwa kuzidisha upendo miongoni mwetu. Upendo huu usijengeke kwa Waislam pekee balihata kwa wasio Waislam, alisema.


Chanzo: Mwananchi
 
Nilikuwa sijui kama Tanzania ni nchi ya dini fulani!

BS!
 
Haimaanishi ivyo ila kama umeamini hivyo kivyako ndugu yetu ulie mbinafsi na mbaguzi
 
Benki ya Azania imejipanga kuanzisha dirisha la kutoa huduma (Islamic Window) kwa ajili ya kutoa huduma za kibenki zinazofuata kanuni na misingi ya Kiislamu, benki hiyo imetangaza.

Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Benki ya Azania, Bernard Haule, wakati akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles Singili, wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo maalum kwa wateja wake Waislamu jijini Dar es Salaam juzi.

“Tupo katika maandalizi ya kuanzisha huduma za kibenki kwa niaba ya wateja wetu ambao ni waumini wa dini ya Kiislaamu baada ya kuanza kutoa huduma kupitia mawakala miezi michache iliyopita," alisema.

Aliongeza: “Tunaamini huduma hii itasaidia kuleta ahueni kwa wateja wetu Waislamu. Dhamira yetu ni kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma za kipekee zitakazokidhi matakwa yao kikamilifu.”

Haule alisema kuwa benki yake imekuwa ikiandaa hafla za kufuturisha kwa wateja wake jijini Dar es Salaam na mikoa mingine ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kujumuika pamoja na wateja wake hususani wakati huu wa Ramadhan.

Alisema kuwa benki yake imekuwa katika mstari wa mbele wa kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii kupitia mpango wake wa kuisaidia jamii hususani katika masuala ya afya na elimu.

Aidha, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, wakati wa hafla hiyo aliwaasa Waislamu wote nchini kuungana pamoja na kufuata misingi ya dini ya Kiislamu.

“Waislamu inatakiwa watumie mwezi huu wa Ramadhan kwa kuzidisha upendo miongoni mwao. Na upendo huu usijengeke kwa Waislamu pekee bali hata kwa wasio Waislamu," alisema.





CHANZO: NIPASHE

 
Haya tena waisilamu banki zinazofuata taratibu na imani za kiisilamu ndio hizo zinajimwaga zenyewe tuchangamkieni fursa hio adhimu naomba pia bank nyengine zifuate hio
 
Huduma za kibenki zinzofuata sheria za kiisilamu ni nzuri ndugu zangu watanzania maana sisi ni waisilamu na wengine ni wakiristo ambapo dini zote hizi mbili tulizonazo zinakataza kula riba riba ni haramu kwa waisilamu na wakiristo hivyo watanzania tuchangamkie hizo hata na benki ambazo bado hazijaingia kwenye huu utaratibu wafanye haraka sana wasije kukimbiwa na wateja wao wa kiisilamu na kikiristo wanaochukia riba
 
kutengana kwenye huduma za kibenki inawezekana lakini kutengana kwenye huduma za machinjio ni kuligawa taifa......tanzania ni zaidi ya uijuavyo..mateo quares ulinena vema

mix with yours
 
Nilikuwa sijui kama Tanzania ni nchi ya dini fulani!

BS!
Usiumize kichwa hizi bank ziko dunia nzima,hata nchi za America,Uingereza,ufaransa,ujerumani.Islamic banking ni mkombozi kiuchumi.Unapokopa hakuna riba,unalipa ulichokopa.Na ukishirikiana nao kibiashara mwagawana Faida na hasara sawa sawa.
Jana kuna dada mmoja anaduka lake zuri,mda mrefu,kumbe kakopa kwenye tasisi za fedha zenye riba,walimuingilia wakakamata bidhaa zake zote dukani mpaka Mafeni wameondoa juu ya dari.
Huoni hapo ni matatizo ya riba?Riba ni matatizo matupu.
 

good reference katika nchi hizi pia kuna sehemu wanauza nyama imeandikwa HALAL, tusichuje vya kuiga!


mix with yours
 
Nilikuwa sijui kama Tanzania ni nchi ya dini fulani!

BS!

Vijitu Vingine vishamba sana ila vyenyewe havijijui, tembea Duniani uone Mambo, Kwa Taarifa yako hata huko Uingereza walokuletea iyo dini yako wanayo Islamic Bank (Islamic Britain Bank) IBB na mmoja wa wana hisa wakubwa ni Tony Blair, Kajifunze madhara ya Riba kijamii uone jinsi watu wanavofilisika, mataifa ya Africa more than 70% ya deni inayolitesa ni malimbikizo ya Rib
 

"..We agree to disagree"hii si ndio signature yako??

Islamic banking ni kwa ajili ya kufadhili UGAIDI worldwide!
 

Hiyo "hadithi" yako inanifundisha nini?
 
Kwa kuwa huna uwezo wa kufikiri haitakufundisha lolote ahaa ahaa :Cry:[/B]QUOTE=Rapherl;6984891]Hiyo "hadithi" yako inanifundisha nini?[/QUOTE]
 
Kwa kuwa huna uwezo wa kufikiri haitakufundisha lolote ahaa ahaa :Cry:[/B]QUOTE=Rapherl;6984891]Hiyo "hadithi" yako inanifundisha nini?
[/QUOTE]

Kwanini ukope kama hauna uwezo wa kulipa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…