Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

I think watamkumbuka mafisadi wenzake kwani aliwasaidia kuwa mabilione kwa speed ya rocket bila kutumia jasho kwakujimilikisha vitega uchumi vyote vya taifa letu. Sisi tupo katika kulijenga taifa letu tuna imani tunaweza na hatuna haja ya kumkumbuka mtu yeyote baada ya kuwaondoa hawa mamluki tutaanza kazi ya kuileta Tanzania tunayoipenda sote kila mtu akiwa na nafasi ya kuipaka rangi kwa kipaji chake ili iweze kuzidi kuwa mrembo na kuwa fahari yetu sisi watoto wake.
 
Mungu akulinde na akuöngoze mzee Mkapa binafsi nakupenda na nitaendelea kukupenda ulikuwa good president.

Urais wa Mkapa ulianza kuingia dosari pale rafiki yake balozi Ruhinda alipoingia mkenge wa kufanya urafiki na Rostam Aziz ambae alikuwa anatafuta upenyo wa kuwa karibu na Rais. Alipofanikiwa kupelekwa kuwa karibu na Mkapa na wakati Mkapa akiwa nje ya nchi kwa matibabu hapo ndio huyu burushi alipofanya hayo madudu yake ya Kagoda etc!! Kama huyu Ruhinda asingefanya huo ukuwadi wa kumpeleka RA karibu na Mkapa haya madudu yasingefanikiwa. Inasemekana huyo Ruhinda ni mahututi kwa maradhi na yuko kitandani hajiwezi hivyo kwa kuiingiza nchi yetu katika matatizo makubwa nadhani Mungu anamuadhibu hapa hapa duniani ili hata hizo hela walizoiba asizifaidi!!
 
Ndiyo, tutamkumbuka kwa jinsi alivyofisadi nchi yetu na kuwawezesha mafisadi wenzake kuendeleza libeneke. Ni Mkapa huyu huyu aliyekuwa akiapa kila kukicha kuwa "over my dead body," kuhusu Kikwete kuukwaa urais. Sasa atueleze ilikuwakuwaje?

Asante Jasusi umenena tutamkumbuka kwa kutuingiza mkenge na madili ya ufisadi tunayoumia mpaka sasa..... . Pia tutamkumbuka kwa jinsi alivyouza mashirika yetu ya umma kama njugu halafu hela yake isionekane mpaka leo. Ama kweli tutamkumbuka sana tu.
 
Huyu mzee pamoja na tuhuma zote bado namkubali kwa utendaji wake wala huwezi kumlinganisha na hawa playboys na playgirls tulonao kwasasa!


Hapo mkuu umenena huyo mzee wengi tunamkubali huwezi linganisha na hii vuvuzela!! Yaani mimi nashindwa kuelewa huyu jamaa amesoma uchumi gani huo? Au anatudanganya jamaa naye ni Kihiyo?
 
Kifupi ben was a good president however he had som few weakness on some issues,

but now we have big blander and shame to our children they will ask on this.
 
Mimi namkumbuka President Mkapa kwa kurudisha heshima ya watanyakazi Mungu ambariki natuzidi kuomba Mwenyezi Mungu atupatie Rais mchapa kama yeye.
 
Miafrika Ndivyo Tulivyo BY NYANI
HAPA NDO NAMKUMBUKA JAMAA HUYU
 
Big Ben was n still is the greatest Leader of all time compared na hawa majizi wa sasa
 
Ni kweli Mh.B.W.Mkapa hatasaulika kamwa kwakuwa maovu yote yanayohadhiri uchumi wa nchi hii yalianzia katika enzi zake za utawala, hii ikiwa ni pamoja na rushwa kubwa; uuzaji wa mashirika ya umma kwa bei ya kutupwa; uuzaji wa nyumba za serikali kwa bei chee; uporaji wa rasilimali za taifa kama magogo madini, minofu ya samaki na wanyama pori. aidha ni katika enzi za Mkapa ambapo ulianzishwa mfumo wa mgawanyo wa pato la taifa wenye kutoa upendeleo maalum kwa tabaka dogo la wananchi na kuwaacha walio wengi kudidimia katika lindi la umasikini.
 
Ndiyo, tutamkumbuka kwa jinsi alivyofisadi nchi yetu na kuwawezesha mafisadi wenzake kuendeleza libeneke. Ni Mkapa huyu huyu aliyekuwa akiapa kila kukicha kuwa "over my dead body," kuhusu Kikwete kuukwaa urais. Sasa atueleze ilikuwakuwaje?

Maybe he died...or he is living post humously
 
mi naona kukumbuka kitu au mtu sio issue, mbona hata maharage ya shuleni huwa tunayakumbuka?

ajisafishe kwanza na tuhuma za ufisadi zinazomkabili ndiyo apewe heshima anayostahili
 
Ninachoweza kusema ni kwamba Mkapa alikuwa shujaa. Watanzania hatutakuja msahau kamwe.
 
'the courage of leadership'..tutakukumbuka daima Mzee wetu
 
Ben na mkubali sana hata kama alikuwa na maovu yake ktk nchi hii ali2mia akili sana. Kwan effect zake hazikuoneka saaana ukifananisha na awamu hii
 
Ndiyo, tutamkumbuka kwa jinsi alivyofisadi nchi yetu na kuwawezesha mafisadi wenzake kuendeleza libeneke. Ni Mkapa huyu huyu aliyekuwa akiapa kila kukicha kuwa "over my dead body," kuhusu Kikwete kuukwaa urais. Sasa atueleze ilikuwakuwaje?
Aliambiwa hivi Malaika kasema........, na TISS wapo chini ya Malai........, hivyo nchi itayumba endapo hata mpitisha!!
 
Hata JK awe ametenda mabaya kiasi gani, mabaya yake hayawezi kuhalalisha maovu ya msingi ya MKAPA
Mkapa ndiye aliyeutangazia ulimwengu kuwa "MITANZANIA MIVIVU" hata wabotswana walipotutetea kuwa tunaijenga nchi yao,
Kwa imani yake hiyo hakuamini katika utu wa mtanzania hivyo hakuamini kama TANZANIA ni nchi inayostahili kujitegemea akasema "......hatuishi kisiwani"..
Katika mjadala wa kuijenga Tanzania bora, kama taifa lenye hadhi ya watu wanaosimamia mambo yao, taifa lenye kujitegemea.... si Mkapa , si Mwinyi wala Kikwete aliyeweka msingi wowote sanasana wamekuwa busy kila mtu kwa nafasi yake kumomonyoa misingi aliyoijenga Mwalimu Nyerere (sijasema Mwalimu hakuwa na mapungufu)
 

Sisi hatotomsahau kwa kutuletea majeshi kutuua na kufanya vitendo vyengine vya kinyama.

Ndio tutamkumbuka huyu mtu, sana tu
 
Mkapa aliharibu sana baada ya baba wa Taifa kufariki. Huyu jamaa kama angekuwa na msimamo uleule basi nina hakika angetupeleka mbele kama si ombwe la watch dog kutokea baada ya kifo cha nyerere. Ikawa kama vile kipofu kaona mwezi. Tunaweza kumbuka Mkapa kwa kumlinganisha na JK. Kwenye comperative and superative tunaweza sema Mkapa ni worse president but Kikwete is a worst President Tanzania have ever had. Ukiangalia ndani ya miaka mitato tu ya uongozi ameongeza deni la Taifa kwa more than $4Billion to More than $10billion from $6Billion left by Mkapa after 10 years in office. Yaani JK amekuwa extravagant na kundi lake la mtandao utafikiri mchwa wamekabidhiwa ghala la nafaka.

Source: http://allafrica.com/stories/201101270183.html
 
Naye alikuwa na makosa yake,hasa uwekezaji na uuzaji wa mashirika ya umma kwa bei chee,na uwizi wa mali ya umma kwa kutumia nguvu za chama na wafanyabiashara uchwara hasa katika kipindi cha pili ,Lakini ana uwezo mara 100 kuliko wa sasa
 
Pamoja ma mapungufu yake mzee Mkapa lakini inchi ilikuwa pazuri kuliko ilivyo sasa,he is much better kwani inchi ilikuwa na displine ya hali ya juu,leo bei ya sembe na sukari bado iko juu mbali ya mkuu wa kaya kutoa tamko vishuke,then what is this?,sasa hivi kila mtu anatoa matamko na haya fanyiki yanayoogizwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…