Benjamin Mkapa Stadium. Je mabango ya matangazo ya umeme yameacha kufanya kazi?

sarcomere1

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
305
571
Ni takriban miezi miwili tangu kuzinduliwa wa michuano ya African Football League (AFL) ambapo mabango ya matangazo ya umeme yalianza kufanya kazi kwa mara ya kwanza

Lakini katika hali ya kustaajabisha baada ya mechi chache tu kuchezwa uwanjani hapo, mabango hayo hayafanyi kazi tena na badala yake zimebandikwa stickers

Hivi kitu gani hakipo sawa kwetu sisi watanzania?
 
Kwa umeme gani na kiingilio cha buku 3? Yanatumia umeme yale, Kwa hiyo tunapunguza matumizi.
 
Kuya maintain yake mabanko ukaendelea kuyaona vile sio kazi rahisi, yanahitaji pesa sasa kwa nchi inayonuka ufisadi kama hii si jambo la kushangaza kuona hayapo Tena.
 
Kuya maintain yake mabanko ukaendelea kuyaona vile sio kazi rahisi, yanahitaji pesa sasa kwa nchi inayonuka ufisadi kama hii si jambo la kushangaza kuona hayapo Tena.
Gharama yake inakujaje kwenye kuyamaintain? Umeme? Au ni vipi yani
 
Ile kazi ningepewa mm ya kufunga zile tv panel hapo Huenda zimekunywa maji zimekufaa na ni gharama
Zimekunywa maji zimekufa, inamaana haikujulikana kama zinafikiwa na maji kipindi cha mvua? Vipi Yale ya Azam complex mbona yanafikiwa na maji lakin yanaendelea kufanya kaz?
 
Mbona ulaya kila kiwanja kina hayo mabango na yanafanya kazi hata kipindi cha mvua kali bila ya kuharibika...au walinunua feki?
 
Ata mm nlikua najiuliza sana imekuaje hayafanyi kazi tena inaonekana kama ni shamba tu la maboga
 
Na mvua zile huenda yameungua
Ila mantainance yake si mchezo
Na umeme wa Bongo basiii
 
Hapana...yanafanya KAZI mbona...sema machi hizi za caf mfumo wao ni stick...Yani yake mabango hayatembei..yabakuwa yanaonekana Kwa mpangilio ule ..tazama mechi zote hata za sauzi kwenye viwanja wenye LED tv parameters utaona inavyokuwa...

Plus kingine Yale ni mwekezaji kaweka...sio serikali wala tff...wala uwanja wa taifa kina kampuni iliiingia ubia na serikali kufunga zile LED parameters.....so gharama za matangazo kuwa displayed pale ni hao wadhamini wa klabu wanatakiwa kulipa Kwa hiyo kampuni ili matangazo yao yawe displayed...

Kwenye hili nachoona baadhi ya makampuni ni aidha hawako tayari kwenye kulipa au gharama ni kubwa...maana pale unaweza kutwa tangazo linachajiwa Kwa sekunde ..sasa hesabu kampuni idhamini klabu alafu ilipe tena na pesa ya kufanya matangazo yao yaonekane uwanjani.

Hata hivyo ukisema ni wajibu wa klabu kulipia hayo matangazo Kwa kuwa ni wajibu wao kimkataba na hayo makampuni..nayo ni ngumu...maana klabu zinalipa gharama za mchezo .Kisha zilipe tena gharama za ghafla za kudisply matangazo kwenye LED lights za uwanjani..inakuwa ni kichekeshi.

Hivyo basi...huenda klabu zimekataa kulipia hayo matangazo au huenda kampuni zinazodhamini klabu zikawa zimeukataa huo mtego...

Nadhani kuanzia msimu ujao kutakuwa na Sheria ya lazima ya namna ya kutumia hizo LED lights parameters
 
Back
Top Bottom