Bendera za CCM zimeng'olewa Arusha

Bendera za CCM zimeng'olewa Arusha

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,227
Reaction score
3,330
Nimetembea maeneo mbambali Arusha, nimegundua kuwa bendera nyingi za CCM zimeondolewa. Ukienda kwenye mashina ya CCM bendera zimeng'olewa.

Nimehoji watu wengi wanasema kuwa CCM ni chama cha waonevu, kinapokonya haki ya wanachama wake na kuwa chama cha familia.

Wanasema Tumechukizwa na jinsi Lowasa na wagombea wenye heshima CCM kukatwa, wanasema "hatukuchukizwa na Lowasa tu kukatwa,bali kuona kijana mdogo kama Makamba alieupata Uwaziri juzi anaweza kuwa na uwezo wa kuingia tano bora kuliko wale walioitumikia CCM miaka mingi kama akina Sitta na wengineo.

Na jambo lingine linalowakasirisha ni kuona kuwa matamko yametimia kama "Rais wa Tanzania hatatoka Kaskazini".
 
Kampeni piga mbizi Makomeo kaanza kampeini mapemaaa.Lubuva mkate kama Lowasa
 
Umbea wako utakutesa sana
Utajuwa wapi wakati mpo busy kumfungia Kingunge,simba, nchimbi na Lowas..mtakuja mwomba ongee kitu very soon.kawafungie na hao watu wa arusha,masai wa monduli na wengine nchini ili wasiwapige chini...
 
Jamani, mbona watu tunajitia wazimu hivi hivi?? Ni nani mmbeya hapa? Kusema Makofuli kaanza kampeni mapema ni umbeya??

Walifanya kampeni ya kufa mtu kwa mbwembwe za kusaka wadhamini na kuchukua form na kurudisha fomu, sasa mzee Lubuva ndo unajifanya kuangalia upande mwingine??

Kama kweli hii ni tume huru, chukua hatua. Mkate huyo Makofuli au mpe hata onyo. Kila kinyume kifanywacho na ccm hakionekani, ila akijaribu kufanya chema, CDM kinaitwa uvunjifu wa amani.

Mkamtandika Lipumba ka Jizi na kumkalisha chini kwenye gari la wazi kuuonesha ulimwengu. Kisa, ati kuandamana kwa amani. Mijizi imeonekana na hatia kabisa kuiba mali za serekali, mnaipa kiti cha kukalia kwenye lile lile gari mlilompakia Lipumba. CCM mna mambo nyiye we acha tu. Nisameheni, nawaza tuuu
 
Watu wa kaskazini mwa Tanzania walishaikataa ccm muda mrefu sana...huo ni muendelezo tu...
 
Arusha ni ndogo sana ukiilinganisha na kijiji nilicho.hasa kwa wapigakula ya ndio kwa ccm
 
Nkobe

nyie wajinga na siasa zenu za ukamda na ukabila,watu wakiwasema mnalalamika mimi mmwenyewe nakaa arusha nasikia wanayoyasema
,naomba na kanda ya ziwa zote za upinzani wazingoe tuone na ukabila wanu,
mungu anapompanga mtu kuwa rais kwake sio ukanda wala ukabila bali mtu sahihi wa kuongoza taifa,
 
Last edited by a moderator:
Unategemea nini wanywa gongo,viroba na banana wanapo kutana? Wao wanacho waza ni kuvunja sheria na kuharibu amani tuu!

Uwezi kutaka kukabidhiwa nchi ikiwa hujakomaa kisiasa na wala huna uvumilivu kwa wengine!
Hii ni moja ya sababu ya nyie kukosa kura za watu wengi...kuna mtu anaweza kufikiri kuwapa kura lakini akasita maana akiona matendo yenu hamna tofauti na vikundi vya waasi au maharamia!

Ikulu mtaisikia kwenye bomba..
 
Watu wa kaskazini mwa Tanzania walishaikataa ccm muda mrefu sana...huo ni muendelezo tu...
Lakini waliikubali chadema kwakuwa ni chama cha kaskazini na ni saccoss ya wachaga! Bora leo umeseme mwenyewe Bavicha! Lakini pamoja na hayo huwa ham affect matokeo ya nafasi ya Urais...
 
Back
Top Bottom