Benard Mwakyembe ahamia CCM akitokea CHADEMA

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
227
Reaction score
599
ALIYEKUWA msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, Benard Mwakyembe amejitoza wiki chache baada ya kukihama chama hicho na kueleza mambo 10 yaliyomfanya kuhama kubwa likiwa la serikali ya awamu ya tano kufanyia kazi ajenda za chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwakyembe ambaye pia alikuwa Diwani wa Kata ya Mtoni jimbo la Temeke, amesema ameamua kuzungumza na umma baada ya kuwepo upotoshaji kwamba amenunuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) huku wengine wakidai alilazimishwa kupanda jukwaa la chama hicho Septemba 15 mwaka huu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mbunge wa Ukonga .

Mwakyembe amekanusha vikali tuhuma hizo na kusema, “mimi sikununuliwa kwa gharama yeyote na wala sikuwa na sababu ya kununuliwa kwani kipato change kinanitosheleza mimi na familia yangu…hakuna anayetoka Chadema wala chama chochote kwenda CCM akanunuliwa, labda kama wao wanafanya hizo tabia za kununua watu.”

Amesema kila mtanzania ana haki ya kuwa katika chama anachokipenda na anaweza kuhamia chama chochote huku akitolea mfano wa Mawaziri Wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fedrick Sumaye ambao walihamia Chadema kipindi yeye akiwa katika chama hicho na kwamba waulizwe kama wao walinunuliwa kuhamia chama hicho.

“Chadema na vyama vingine vyote, acheni kupoteza umma na kuwadanganya watanzania kwamba watu wananunuliwa, wanatekwa. Hizo ni propanganda za kitoto na hazina mashiko yoyote,” amesisitiza Mwakyembe.

Akitaja sababu mbalimbali za kuhama Chadema amesema ajenda kuu katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na 2015 endapo chama hicho (Chadema) kingeingia madarakani ilikuwa ni kupambana na ufisadi, elimu bure, ujenzi wa miundombinu, kuboresha usafiri wa anga, kuboresha huduma za afya na kuimarisha uchumi na kwamba zimefanyiwa kazi na Serikali ndani ya kipindi cha miaka mitatu tu.

“Leo Rais John Magufuli anafanya haya, tunaona ujenzi wa barabara nchi nzima unaweza kuzunguka kwa gari ukafika kwa wakati. Kama hilo halitoshi, ujenzi wa flyover ya Tazara (Mfugale Flyover) na ujenzi wa Interchange ya Ubungo, kupanua barabara ya Ubungo-Chalinze na kila wilaya zinajengwa barabara mfano Temeke imetengewa Sh bilioni 246 chini ya mradi wa DMDP, ” amesema Mwakyembe.

Amesema pia serikali chini ya Rais Magufuli imeanza ujenzi wa bwawa kubwa na kufua umeme la Stigler’s Gorge katika mto rufiji lenye uwezo wa kuzalisha MW 2100 ili kuondoa kabisa upungufu wa nishati ya umeme na kushusha gharama za nishati hiyo nchini.

Ameongeza kuwa licha ya Chadema kuahidi kuboresha usafiri wa reli, Rais Magufuli ameenda mbali zaidi na kuamua kujenga reli mpya ya kisasa (SGR) itakayosaidia kusafirisha abiria na mizigo kwa haraka zaidi.

Amesema mwaka 2015 kwenye kampeni, Chadema walikuwa wanaimba suala la kutoa elimu bure na kwamba suala hilo limefanyiwa kazi na Rais Magufuli mara tu alivyoingia madarakani kama alivyoahidi na kwamba serikali inatenga zaidi ya bilioni 20 kila mwezi kwaajili ya kuhakikisha hakuna mwananchi anayelipia elimu kuanzia darasa la awamli hadi kidato cha nne.

Aidha kuhusu ajenda ya ufisadi, Mwakyembe amesema ulikuwa ni ajenda kuu ya chama hicho na kwamba tayari imefanyiwa kazi na serikali kwa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka watu walioisababishia Taifa hasara kwa namna yeyote.

Ameeleza sababu zingine za kumfanya ahamie CCM ni kuona namna serikali ilivyoondoa watumishi hewa waliokuwa wakiisababishia serikali hasara kwa kulipamishara hewa, ununuzi wa ndege mpya na kufufua shirika la ndege, kupunguza matumizi ya serikali na kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya, zahanati na hospitali kubwa akitolea mfano Hospitali ya Rufaa ya Mloganzila.

“Kutokana na mambo hayo yote niliyoyataja sijaona tena sababu ya kuendelea kupinga maendeleo yanayofanywa na Rais Magufuli na serikali yake, bali nipo tayari kupambana na kila anayepinaga maendeleo ya nchi yetu ambayo kwa muda mrefu sana ilikuwa inachezewa na wajanja, ” amesema Mwakyembe.
 
Mi mwenyewe nimeamua kuhama CHADEMA na kumuunga mkono Mh rais maana naogopa naweza nikawa wa mwisho kuhama.Mbowe nae karibia anahama subirini yajayo yanafurahisha
 
Bora madiwani waliopo vyama vya upinzani wote wahame chama ili tujue moja tunaingia kwenye chaguzi za marudio ili tumalize moja hii hama hama nusu nusu inatutia gharama kila siku
 
Huyo nae bado anatapatapa tu.Hata kama umeona rais anafanya kazi unayotaka na njema.Sawa ni vyema.Lakin hata ukiwa nje ya chama still unaweza kutoa ushauri uliobora na rais akautumia kwa manufaa ya nchi yote.Sasa je,kwamba hajaona mapungufu kwenye serikali kana kwamba angeweza kutoa maoni na rais msikivu akasikia?

Hata hivyo amefanya vema sana kwa kutumia haki yake ya kikatiba.Angalau huyu amejitahidi kutoa point japo hazina nguvu.Safari njema huko uendako.L.I.P(left in peace)
 
Hakuna mjadala sisi viona mbali 2015 chadema alikuwa sawa na mtu anayekata roho kwa kupaparika baada ya kulichukua fisadi papa na kulipiga puti na kujifanya ni toleo jipya show-room!
 
Bora madiwani waliopo vyama vya upinzani wote wahame chama ili tujue moja tunaingia kwenye chaguzi za marudio ili tumalize moja hii hama hama nusu nusu inatutia gharama kila siku
Nilipewa takwimu kwa chadema wapi1050 wameondoka 43,ssa ili kurahisisha waitwa tu wakaewe tena kule ccm bila ucjaguzi maana ghrama ni kubwa mbo 1007×300000000=30210000000 ni pesa nyingi sana watangaze tu wamepewa udiwani kule ccm bila uchaguzi
 
We jamaa si ulihama muda tu,una kama wiki tatu umeona hakuna anayekuzungumzia umeona uje ujitangaze jamii forum....HAKUNA ANAYEKUFAHAMU KALALE.
 
Huna lolote ungekuwa unajitoshereza usingegombea udiwani wanachosema Chadema ni ukweli mnafanya biashara
ALIYEKUWA msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, Benard Mwakyembe amejitoza wiki chache baada ya kukihama chama hicho na kueleza mambo 10 yaliyomfanya kuhama kubwa likiwa la serikali ya awamu ya tano kufanyia kazi ajenda za chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwakyembe ambaye pia alikuwa Diwani wa Kata ya Mtoni jimbo la Temeke, amesema ameamua kuzungumza na umma baada ya kuwepo upotoshaji kwamba amenunuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) huku wengine wakidai alilazimishwa kupanda jukwaa la chama hicho Septemba 15 mwaka huu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mbunge wa Ukonga .

Mwakyembe amekanusha vikali tuhuma hizo na kusema, “mimi sikununuliwa kwa gharama yeyote na wala sikuwa na sababu ya kununuliwa kwani kipato change kinanitosheleza mimi na familia yangu…hakuna anayetoka Chadema wala chama chochote kwenda CCM akanunuliwa, labda kama wao wanafanya hizo tabia za kununua watu.”

Amesema kila mtanzania ana haki ya kuwa katika chama anachokipenda na anaweza kuhamia chama chochote huku akitolea mfano wa Mawaziri Wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fedrick Sumaye ambao walihamia Chadema kipindi yeye akiwa katika chama hicho na kwamba waulizwe kama wao walinunuliwa kuhamia chama hicho.

“Chadema na vyama vingine vyote, acheni kupoteza umma na kuwadanganya watanzania kwamba watu wananunuliwa, wanatekwa. Hizo ni propanganda za kitoto na hazina mashiko yoyote,” amesisitiza Mwakyembe.

Akitaja sababu mbalimbali za kuhama Chadema amesema ajenda kuu katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na 2015 endapo chama hicho (Chadema) kingeingia madarakani ilikuwa ni kupambana na ufisadi, elimu bure, ujenzi wa miundombinu, kuboresha usafiri wa anga, kuboresha huduma za afya na kuimarisha uchumi na kwamba zimefanyiwa kazi na Serikali ndani ya kipindi cha miaka mitatu tu.

“Leo Rais John Magufuli anafanya haya, tunaona ujenzi wa barabara nchi nzima unaweza kuzunguka kwa gari ukafika kwa wakati. Kama hilo halitoshi, ujenzi wa flyover ya Tazara (Mfugale Flyover) na ujenzi wa Interchange ya Ubungo, kupanua barabara ya Ubungo-Chalinze na kila wilaya zinajengwa barabara mfano Temeke imetengewa Sh bilioni 246 chini ya mradi wa DMDP, ” amesema Mwakyembe.

Amesema pia serikali chini ya Rais Magufuli imeanza ujenzi wa bwawa kubwa na kufua umeme la Stigler’s Gorge katika mto rufiji lenye uwezo wa kuzalisha MW 2100 ili kuondoa kabisa upungufu wa nishati ya umeme na kushusha gharama za nishati hiyo nchini.

Ameongeza kuwa licha ya Chadema kuahidi kuboresha usafiri wa reli, Rais Magufuli ameenda mbali zaidi na kuamua kujenga reli mpya ya kisasa (SGR) itakayosaidia kusafirisha abiria na mizigo kwa haraka zaidi.

Amesema mwaka 2015 kwenye kampeni, Chadema walikuwa wanaimba suala la kutoa elimu bure na kwamba suala hilo limefanyiwa kazi na Rais Magufuli mara tu alivyoingia madarakani kama alivyoahidi na kwamba serikali inatenga zaidi ya bilioni 20 kila mwezi kwaajili ya kuhakikisha hakuna mwananchi anayelipia elimu kuanzia darasa la awamli hadi kidato cha nne.

Aidha kuhusu ajenda ya ufisadi, Mwakyembe amesema ulikuwa ni ajenda kuu ya chama hicho na kwamba tayari imefanyiwa kazi na serikali kwa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka watu walioisababishia Taifa hasara kwa namna yeyote.

Ameeleza sababu zingine za kumfanya ahamie CCM ni kuona namna serikali ilivyoondoa watumishi hewa waliokuwa wakiisababishia serikali hasara kwa kulipamishara hewa, ununuzi wa ndege mpya na kufufua shirika la ndege, kupunguza matumizi ya serikali na kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya, zahanati na hospitali kubwa akitolea mfano Hospitali ya Rufaa ya Mloganzila.

“Kutokana na mambo hayo yote niliyoyataja sijaona tena sababu ya kuendelea kupinga maendeleo yanayofanywa na Rais Magufuli na serikali yake, bali nipo tayari kupambana na kila anayepinaga maendeleo ya nchi yetu ambayo kwa muda mrefu sana ilikuwa inachezewa na wajanja, ” amesema Mwakyembe.
 
Siyo lazima anunuliwe kwa pesa kuna njia nyingi za kununuliwa anaweza akawaamenunuliwa kwa kuahidiwa kupewa manono nako ni kununuliwa, anaweza akawaameahidiwa kupewa unafuu katika mambo fulanifulani nako ni kununuliwa,vyanzo vyake vya mapato vinaweza vikawa vimetishiwa kuharibiwa kama vya Mbowe na ili vyanzo vyake vya mapato viweze kupona ni kuhamia CCM nako ni kununuliwa.
 
Ndiyo wamegundua mwaka huu kwamba walikuwa wanaongozwa na mr zero ?

Hongereni sana kwa kuendelea kujitambua na kuukataa unyumbu.
 
Ni sawa na kusema nimemuacha mke wangu na kuishi na dada wa nyumba. Sababu
1 Anapika
2 Anafanya usafi nyumbani
Baada ya kujituma na kuleta maendeleo kwa wananchi wanakaa na kuangalia jinsi gani wawavuruge wapinzani. Halafu kutwa wanakwenda kwa wachina na wazungu kuomba misaada lakini hutosikia kuomba misaada ya silaha za kivita bali hununua na waje kuzitumia kuwauwa wapinzani. Trump akituita shithole country tutabaki kununa, kwenye maisha unahitaji mpinzani ndio maana hata Mungu amemueka shetani kuwa mpinzani wake. Kama upinzani hauna maana basi Mungu agelikuwa kisha muangamiza shetani(iblisi) zamani sana.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom