Nelson Kileo
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 3,054
- 3,263
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernad Membe, amekitaka Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kutoruhusu mtu yeyote
kununua urais kama njugu.
Alitahadharisha kuwa kama itatokea kada yeyote
wa CCM amepata urais kwa kununua kama
njugu, waandishi wa habari nchini watakuwa wa
kwanza kulaumiwa kwa kuwasaidia kuwaingiza
madarakani watu wa aina hiyo.
Ingawa Waziri Membe hakutaja jina la mtu, lakini
kauli yake ni dhahiri kwamba ilikuwa ikimlenga
Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa, ambaye amekuwa akiandamwa
ndani ya chama chake, kwamba anataka urais
kwa kumwaga fedha katika vikundi mbalimbali
nchini, kikiwemo chama cha waendesha
Bodaboda.
Waziri Membe alitoa kauli hiyo ya fitna jana
mjini Dodoma mara baada ya kumaliza kuhojiwa
na Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM, chini ya
uenyekiti wa Philip Mangula.
Membe ambaye ni miongoni mwa watu
wanaotajwa kuwania urais mwaka 2015, aliitaka
CCM iwe makini kufuatilia nyendo za makada
wake wanaotaka urais kwa kumwaga fedha ili
wachukuliwe hatua.
CCM hakiwezi kuruhusu urais wa nchi
upatikane kwa kununua kama njugu na kama
itatokea hivyo waandishi wa habari mtakuwa
sehemu ya lawama.
Waandishi nawambia mtaona tukiacha suala
hilo litokee hapa nchini kwani hamuwezi
kututengenezea uongozi kwa njia ya fedha,
alisema Waziri Membe.
Alisisitiza kuwa ni mwiko kwa mtu yeyote ndani
ya CCM kutumia fedha kama nguzo ya ushindi
kama wanavyofanya baadhi ya makada ambao
hata hivyo hakuwataja kwa majina.
Akizungumzia mambo yaliyojitokeza kwenye
mahojiano yake na Kamati ya Maadili, Waziri
Membe alieleza mambo makubwa matatu na
kubwa kuliko yote ni kuibuka kwa makundi ya
urais.
Suala la pili alisema ni matumizi ya fedha katika
kuusaka urais kwani alidai kuwa kuna watu
wanatumia mabilioni ya fedha kujiimarisha
kisiasa kwa ajili ya urais mwakani.
Suala la tatu ni ninyi waandishi wa habari. Sijui
mmelishwa nini? Sijui mmemeza mdudu gani
vichwani mwenu mpaka muone kinachosemwa
na mtu fulani ni cha maana kitoke kwenye
magazeti na kingine kikisemwa na fulani hata
kama ni cha maana kisitoke kwenye magazeti,
alisema.
Membe alisema katika majadilino na kamati
hiyo, walijadili uwezekano wa kuwapata
wagombea urais ifikapo Desemba mwaka huu ili
kumaliza fitna na makundi yanayoweza kukimega
chama.
Hayo yalikuwa sehemu ya majibu yangu na
niliitaka kamati hiyo iendelea kufanya kazi hiyo
na bado kuna watu wengine waitwe lengo likiwa
kukifanya chama kiwe imara na kiende kwenye
uchaguzi mwakani kuvishinda vyama vyote
vinavyojitokeza tokeza na vingine ambavyo
vimeanza kufa, alisema Waziri Membe.
Kwa mujibu wa Membe, aliishauri kamati hiyo
kuhakikisha chama kinaandaa midahalo kwa ajili
ya makada wake wanaowania urais ili wananchi
wawajue mapema na hata uwezo wao wa
kujieleza.
Waziri Membe alijigamba kuwa CCM ndiyo
inaweza kuamua muelekeo na hatma ya nchi na
wasipokuwa makini kwa kuwaacha wenye pesa
kuchukua uongozi, chama kitakufa na taifa
litaangamia.
Kamati Ndogo ya Maadili yenye wajumbe sita,
ilianza kuwahoji makada wake wanaodaiwa
kukiuka kanuni za chama hicho Februari 13.
Mbali ya Membe ambaye jana alifunga dimba,
wengine waliowekwa kitimoto na kamati hiyo ni
pamoja na Lowasa, Mbunge wa Sengerema
William Ngeleja, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick
Sumaye, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
(Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira na
Naibu Waziri wa Sayansi na Tecknolojia, Januari
Makamba.
source:Tanzania Daima