Sal
JF-Expert Member
- Jan 14, 2008
- 498
- 227
Watangazaji wa sasa hata hawana mvuto kama huyu jamaa!
kwani sasa hivi kuna mtangazaji. mtu hawezi kutofautisha "R" and "L" lakini anatangaza. Zamani RTD upuuzi huu haukuwepo, qualification ya kwanza ni sauti yako halafu matamshi ya kiswahili fasha.. sio unapenda kutangaza lakini sauti linakwaruza kama chura. Mnawakumbuka akina Jacob Tesha, David Wakati, wakitangaza taarifa ya habari, hata kama hakuna la maana utasikiliza tu zile sauti. Akina Enock Ngombale akitangaza kipindi cha salam, utapenda, akina Abisai Steven, Julius Nyaisanga, Halima Kihemba, sauti zilitulia, na wengine wengi. Sasa hivi hata kama kuna la maana linatangazwa, ile sauti tu inakufanya hata hamu ya kusikiliza huna, mtu ana accent ya kichaga au kisukuma eti ni mtangazaji. Upuuzi mtupu!