Ben Kiko yu wapi jamani?

Watangazaji wa sasa hata hawana mvuto kama huyu jamaa!

kwani sasa hivi kuna mtangazaji. mtu hawezi kutofautisha "R" and "L" lakini anatangaza. Zamani RTD upuuzi huu haukuwepo, qualification ya kwanza ni sauti yako halafu matamshi ya kiswahili fasha.. sio unapenda kutangaza lakini sauti linakwaruza kama chura. Mnawakumbuka akina Jacob Tesha, David Wakati, wakitangaza taarifa ya habari, hata kama hakuna la maana utasikiliza tu zile sauti. Akina Enock Ngombale akitangaza kipindi cha salam, utapenda, akina Abisai Steven, Julius Nyaisanga, Halima Kihemba, sauti zilitulia, na wengine wengi. Sasa hivi hata kama kuna la maana linatangazwa, ile sauti tu inakufanya hata hamu ya kusikiliza huna, mtu ana accent ya kichaga au kisukuma eti ni mtangazaji. Upuuzi mtupu!
 
Ben Kiko kuna kipindi alinifanya nisipende kumiss kipindi cha MAJIRA cha RTD enzi hizo hasa akiwa stesheni ya Dodoma na kisha akahamia Tabora. Taarifa zake zilikuwa na misisimko sana hata watu wengi walifika mahala akimaliza kuongea yeye wanafunga redio kuashiria kipindi kimekwisha siku hiyo. Sijamsikia muda mrefu sana, yuko wapi?????

Ben Kiko alijaliwa kipaji cha kuwavuta wasikilizaji wake na kuwapa haja ya mioyo yao kusikiliza habari. Wakati huo huo kuna mtu ambaye sikutamani hata kusikia sauti yake redioni kwa sababu ya kutangaza habari hasi tu kutokea vituo vya polisi kwa RPC Mbeya (Martha Ngwira) naye hasikiki tena. Au ......??? Tusiseme sana huenda walisharudisha mafaili...... (Mungu anisamehe).
Ameshatangulia mbele ya haki
 
Benjamin Kikoroma apumzike pema peponi huko aliko. Alikuwa na talent sana katika kipindi ambacho talents zilikuwa hazilipi kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom