Iman...
Moja Mohamedi na nyingine ya Yesu.
Hiyo ni tofauti kama vile umewekewa Nissan Patrol mbili za muundo mmoja, zinashabihiana sana, moja nyeupe, nyingine nyekundu.
Ukaambiwa tofauti ya kimsingi kati ya hizo mbili, ukataja rangi.
Ni tofauti, lakini katika msingi wa utendaji wa gari hiyo si tofauti ya kimsingi.
Huyu Carson anasema Waislamu hawafai kuiongoza Marekani.
Marekani ni nchi inayoendeshwa kwa secularism (kutofuata dini yoyote). Inaongozwa kwa misingi ya sheria.
Juzi hapa kumekuwa na mzozo Kentucky kwa sababu mama mmoja mkristo kakataa kutoa marriage certificate kwa watu wa jinsia moja wanaotaka kuoana.
Huyo mama anaitwa Kim Davis. Amesema imani yake ya kikristo haimruhusu kuoa hiyo marriage certificate kwa sababu hakubali kwamba ukristo unaruhusu watu wa jinsia moja wanapaswa kuoana.
Yeye kama county clerk ndiye mtu wa kutoa hiyo license. Dini yake haimruhusu. Kawanyima wenzake marriage certificate ambayo kisheria inaruhusiwa eti kwa sababu tu dini yake anaamini hairuhusu.
Ni sawasawa na Tanzania mtu aende kwa mkuu wa Wilaya kama Makonda, aende kuoa mke wa pili au wa tano, halafu ofisi ya mkuu wa wilaya mtu anayetia saini cheti cha ndoa akatae kumuwekea saini kwa sababu yeye karani ni mkristo na katika dini ya kikristo kuoa mwisho mke mmoja.
Kwa hiyo, utaona kwamba, ukitaka kuchunguza sana habari za dini, mtu yeyote anayetaka kuweka dini mbele ya sheria, awe mkristo au muislamu, hawezi kuongoza kazi za serikali.
Lwa sababu serikali kama hizi za Tanzania na Marekani ni secular, hazina dini.
Sasa kuwasema waislamu tu wakati habari hii ina apply hata kwa wakristo ni kuwaonea.
Kinacjotakiwa ni kuhakikisha mtu wa dini yoyote akitaka kuanza kazi ya serikali anakula kiapo cha kufuata aheria na mambo ya dini kuyaweka oembeni mpaka atakapotoka kazini.