Belarus: Kiongozi Mkuu wa Maandamano ahukumiwa miaka 11 jela na mwenzake miaka 10

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Kiongozi wa upinzani Belarus, Maria Kolesnikova amehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela. Vyombo vya habari vya Belarus vinaripoti kuwa hii ni baada ya kuhusika katika maandamano ya mwaka jana kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata nchini humo.

Mshirika wa Kolesnikova ambaye pia ni wakili Maxim Snak amehukumiwa miaka 10 jela. Wote wawili wamehukumiwa kwa jaribio la kuchukua madaraka kinyume cha sheria.

Kolesnikova mwenye umri wa miaka 39, alikuwa nguvu kuu katika maandamano hayo yaliyokuwa yanampinga Rais Alexander Lukashenko.

Aliwahi kumfanyia kazi mgombea wa urais wakati mmoja Viktor Babariko na alitekwa nyara na jeshi la Belarus mjini Minsk mapema mwezi Septemba mwaka jana.
 
Hapo ndio tujifunze kua huwezi kushindana na wenye Nchi

Jiulize miaka 10 jela ukitoka una ramani gani?
 
Hapo ndio tujifunze kua huwezi kushindana na wenye Nchi

Jiulize miaka 10 jela ukitoka una ramani gani?
Hao ni wanaharakati ambao wamejitoa maisha yao, hivyo hawajali kabisa kufungwa.

Kuna aina za watu.
 
Back
Top Bottom