Being called a mom...... [emoji8]

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
613
Reaction score
1,300
I love being called a mom

Wazungu wanasemaga being called a mom is a precious thing ever

Siwezi kuelezea raha ya kuwa mama, ni ufahari, ni utajiri ni kila kitu ambacho naweza kuandika hapa.

Hakuna kumbukumbu nzuri kwa wamama kama pale mtoto wako wa kwanza anapoanza kujua kuita neno mama, huwa najiona kama tajiri fulani najisikia nguvu na fahari isiyoelezeka.

Kuna wamama wanajichukia wanajuta kwa nini walizaa kwa nini hivi ama vile {kosa ulilofanya ni kuzaa bila utaratibu, yaani kuzaa maybe ukiwa bado mwanafunzi, ulizaa kabla ya ndoa n. k } haya yote yanaweza kuwa yanakupa maumivu mno na kila ukimtazama mtoto unailaani siku aliyozaliwa.

Nataka kusema na wewe mama mwenzangu, jisamehe, mwambie mtu wako wa ndani kuwa nilikosea kupanga lakini kuanzia leo najisamehe, kile ulichofanya ndo dhambi lakini matokea yake yaani mtoto ni jambo la heri, mshukuru sana Mungu mana kuna ambao wanatamani waitwe mama ila hawajafanikiwa.

Kuitwa mama si jambo dogo, ni jambo la kujivunia ni jambo la shukrani kwa Mungu na kubwa mno

Kuwa mama ni zaidi ya chochote unachofikiria

Asante mama yangu, naelewa thamani yako baada ya mimi kuwa mama
I love u mom
Sintoichezea hii fursa, ni takuwa mama bora kwa wanangu ili kukuenzi

M a a a a a a a a a a m a

Note:Wale ambao mnatamani kuitwa mama na bado msikate tamaa Sara mkewe Ibrahim aliitwa mama akiwa mzee kabisa Mungu ashindwi kwa wakati wenu na nyie atawapa kicheko kama changu[emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…