BEIJING OLYMPICS: Haifai kuingiza siasa kwenye michezo

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Caroline Nassoro
VCG111363525857.jpg


Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi imepangwa kufanyika mjini Beijing, China, mwezi Februari, na maandalizi yote kwa ajili ya michezo hiyo yamekamilika.

Lakini baadhi ya nchi ikiwemo Marekani, zimepanga kutoleta maofisa wao katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kwa tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu katika mkoa wa Xinjiang. China mara nyingi imepinga kauli hizi za kupotosha na zisizo na ukweli wowote kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu katika mkoa huo. Hatua kama hiyo ni kuingiza mambo ya kisiasa katika michezo, jambo ambalo linapingwa vikali na jamii ya kimataifa. Wengi tunafahamu kuwa michezo ni moja ya shughuli zinazokusanya watu kutoka tamaduni tofauti, itikadi tofauti, dini tofauti, na tabia tofauti, na haina uhusiano wowote na masuala ya kisiasa. Michezo ni njia nzuri ya kukutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali bila kujali tofuati zao, kwa lengo moja, la kutoa ujumbe wa amani, upendo, uvumilivu, na maelewano, na siasa inapoingia kwenye michezo, inaleta utengano, kukosa maelewano, na kutovumiliana. Hatua zote za kuhakikisha usalama na afya kwa wanariadha zimechukuliwa, na maeneo yote ambapo michezo hiyo itafanyika yako tayari.

Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya, rais wa China Xi Jinping alisema nchi yake itafanya kila linalowezekana kuhakikisha Michezo hiyo inafanikiwa, na kuongeza kuwa, macho ya dunia nzima yameelekea China, na China iko tayari.

Kwa kuzingatia hayo yote, hatua ya Marekani, kususia kuleta maofisa wake katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kwa kisingizio chochote kile haiungwi mkono na jamii ya kimataifa. Nchi nyingine ambayo pia imetangaza kutoleta maofisa wake katika Michezo hiyo ni Canada.

Kususia kuleta maofisa katika Michezo hiyo ni kuonyesha wazi dharau kwa wanariadha, ambao wamefanya mazoezi makali kwa muda wa miaka minne ili kushiriki mashindano hayo. Hatua hii ni kinyume na moyo wa Olimpiki, michezo ambayo imeleta kumbukumbu nyingi kwa karne kadhaa na kukutanisha watu wa jamii mbalimbali pamoja.

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itafanyika kwa mafanikio, licha ya janga la COVID-19 na virusi vya Omicron, kwani China imechukua hatua zote za kiusalama kuhakikisha wanariadha pamoja na ujumbe wao wanashiriki kwenye michezo hiyo bila ya wasiwasi, na kuweka kumbukumbu nyingine muhimu katika michezo hii ya Olimpiki.
 
Back
Top Bottom