Tupige kelele, hali ya bei za vyakula sio shwari

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,818
Wakuu sie ambao tumepata uwezo wa kuingia humu mitandaoni na tukaweza kubadilishana mawili matatu juu ya vitu flani vinavyotokea katika jamii zetu, basi tunauwezo vile vile wa kupigia kelele jambo flani ambalo tunaliona sio la kawaida hili mamlaka husika zifanye kitu chanya kwa manufaa ya jamii.

Sasa hali iko hivi

Mchele kilo moja dukani bei ni 2000

Unga kilo moja dukani bei ni 1800 mpaka 2000

Usukari kilo bei ni 2200-2400

Bidhaa hizi ndio za msingi ktk ustawi wa jamii yetu kuliko jambo lolote lingine, na ndio maana kwa maksudi tu nimeacha kuviorodhesha vitu kama mafuta ya kula, taa na maharage na mboga zingine.

Ni wazi humu duniani hakuna jamii iliyowai kuendelea bila wananchi wake kula na kushiba vizuri, achilia mbali kula tu bali kupata chakula pasipo na shaka yoyote, kula vizuri kunaleta ufikiri mzuri, amani na maendeleo ya nchi.

Je, ni lini nchi hii bei ya unga ikaenda sawa na bei ya mchele? yaani tumefikia hatua ya kuuziwa unga elfu mbili kwa kilo? yaani kwanini yaani? kwamba sasa iv chaguo ni lako tu unga au mchele bei ni ile ile, meanwhile unga ndio chakula kikuu cha maskini kwakua kilijulikana kwa bei yake chee tu, sasa leo et uwauzie unga elf 2 au 1800 kweli?

Naimani kubwa na nguvu ya hii mitandao ya kijamii kua inaweza ikafanya jambo na hali ikalejea atleast kama zamani, kwani hata mwaka jana tu hapo unga ulikua unauzwa kilo 600 mpaka 800!

Sasa bei za vyakula inaweza kushuka sanaa endapo tu serikali itaondoa kodi kwenye sekta za chakula na nafaka kiujumla, yaani ifanye bidhaa zote zenye uhusiano na sekta ya chakula kua zisilipe kodi, ondoa makato yote ya kodi kwenye vyakula visafirishwavyo maeneo mbali mbali, na hata zile pembejeo za kilimo kodi ishushwe ili uzalishwaji wa kilimo uongezeke.

Kwa akili za kawaida tu tufikirie hizi familia maskini maeneo tukaayo, vijijini huko na mitaani je ni wakina nani wanaweza ku afford mchele na unga ambao unauzwa elf 2 kwa milo ya mchana na usiku, ili hali uchumi wa sasa wenyewe ndio huu. Tumezoea kuona wenzetu wakiandamana mabarabarani kisa tu labda mkate uliongezwa bei kwa shiling mia tu na maandamano yakawa makubwa hatari, basi sie hatuwezi kuandamana ila hadi kwenye mitandao yetu hii nayo tushindwe kulipigia kelele hili swala?


Hili tulipigie kelele.
 
Wakati unajiandaa na kuhimiza wananchi kupiga kelele kumbuka hata huku bado kesi inayomkabili mkurugenzi wa JF inaungura. Kwa ufupi hata huo ukumbi au uhuru wakueleza hisia na malalamiko yako nao unazidi kukandamizwa.....

Waziri mkuu bungeni akijibu maswali mubashara amesema ni jukumu la kila kaya kuhakikisha wanauwezo wakujinunulia chakula.
 
Piga kazi acha kupiga kelele hazisaidii, kwani kwa nini bei za vyakula vimepanda bei?
 
Sikio la kufa halisikii dawa watu tunawalisha kwa kodi zetu wanafanya mambo ya hovyo kana kwamba hii nchi ni yao peke yao sababu tu wao ni viongozi watanzania tuamke siasa tusizitegemee hapa tumefika kwa ajili ya siasa za chama kile kiondoeni hiki chama madarakani mwaka 2020 kwa kura nyingi na za kishindo
 
Bei ikishuka chadema mnalalamika kwamba serikali inawaminya wakulima wanashindwa kunufaika na mazao yao,

Bei ikipanda tena ili wakulima wanufaike na mazao yao, chadema mnalalamika tena serikali ishushe bei.

Chadema mpo hapa duniani kumtetea nani??
Hivi hapo ufipa zinawatosha kweli hata za kuvukia barabara??
 
Bei ikishuka chadema mnalalamika kwamba serikali inawaminya wakulima wanashindwa kunufaika na mazao yao,

Bei ikipanda tena ili wakulima wanufaike na mazao yao, chadema mnalalamika tena serikali ishushe bei.

Chadema mpo hapa duniani kumtetea nani??
Hivi hapo ufipa zinawatosha kweli hata za kuvukia barabara??

Hivi wewee ni kichaa? huu uchama unaouleta wewe umeutoa wapi?


acha ubinafsi, ni ujinga sanaa kwa kuzani kila kitu ni lazima kiwe kinatokana na pande mbili either Chadema au CCM!
 
Piga kazi acha kupiga kelele hazisaidii, kwani kwa nini bei za vyakula vimepanda bei?

Acha ubinafsi, kuna familia kibao tu sasa hivi zitakua ktk hali mbaya sanaa, sasa wewe kama unaongea kwa kujiangalia mwenyewe tu ni wazi huu ni ubinafsi mkubwa
 
Acha ubinafsi, kuna familia kibao tu sasa hivi zitakua ktk hali mbaya sanaa, sasa wewe kama unaongea kwa kujiangalia mwenyewe tu ni wazi huu ni ubinafsi mkubwa
Hujajibu swali, kupiga kelele hakutasaidia bei za vyakula kupungua! Unataka serikali ifanye nini? Kwa nini bei za vyakula vimepanda?
 
Ngoja niende ruvu nikatafute shamba nilime.
Maana nimesikia huu ndio muda wa wakulima kutajirika sitaki kumtajirisha mtu, nalima mwenyewe, nakulamwenyewe.
 
Nmekuwa kimnya kwa sababu ya uwoga ila wacha niseme ili km nmekosea bas nipewe oyo,Mh rais nchi hii taabani kweli tumefikaje hapa maharGe 23000 unga kilo. 2500, mchele morogoro unapo limwa 2300?mfumuko Wa bei mkuu timiza wajibu kidgo legeza mkuu
 
Back
Top Bottom