666 chata
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 1,700
- 3,919
Wakuu sie ambao tumepata uwezo wa kuingia humu mitandaoni na tukaweza kubadilishana mawili matatu juu ya vitu flani vinavyotokea katika jamii zetu, basi tunauwezo vile vile wa kupigia kelele jambo flani ambalo tunaliona sio la kawaida hili mamlaka husika zifanye kitu chanya kwa manufaa ya jamii.
Sasa hali iko hivi
Mchele kilo moja dukani bei ni 2000
Unga kilo moja dukani bei ni 1800 mpaka 2000
Usukari kilo bei ni 2200-2400
Bidhaa hizi ndio za msingi ktk ustawi wa jamii yetu kuliko jambo lolote lingine, na ndio maana kwa maksudi tu nimeacha kuviorodhesha vitu kama mafuta ya kula, taa na maharage na mboga zingine.
Ni wazi humu duniani hakuna jamii iliyowai kuendelea bila wananchi wake kula na kushiba vizuri, achilia mbali kula tu bali kupata chakula pasipo na shaka yoyote, kula vizuri kunaleta ufikiri mzuri, amani na maendeleo ya nchi.
Je, ni lini nchi hii bei ya unga ikaenda sawa na bei ya mchele? yaani tumefikia hatua ya kuuziwa unga elfu mbili kwa kilo? yaani kwanini yaani? kwamba sasa iv chaguo ni lako tu unga au mchele bei ni ile ile, meanwhile unga ndio chakula kikuu cha maskini kwakua kilijulikana kwa bei yake chee tu, sasa leo et uwauzie unga elf 2 au 1800 kweli?
Naimani kubwa na nguvu ya hii mitandao ya kijamii kua inaweza ikafanya jambo na hali ikalejea atleast kama zamani, kwani hata mwaka jana tu hapo unga ulikua unauzwa kilo 600 mpaka 800!
Sasa bei za vyakula inaweza kushuka sanaa endapo tu serikali itaondoa kodi kwenye sekta za chakula na nafaka kiujumla, yaani ifanye bidhaa zote zenye uhusiano na sekta ya chakula kua zisilipe kodi, ondoa makato yote ya kodi kwenye vyakula visafirishwavyo maeneo mbali mbali, na hata zile pembejeo za kilimo kodi ishushwe ili uzalishwaji wa kilimo uongezeke.
Kwa akili za kawaida tu tufikirie hizi familia maskini maeneo tukaayo, vijijini huko na mitaani je ni wakina nani wanaweza ku afford mchele na unga ambao unauzwa elf 2 kwa milo ya mchana na usiku, ili hali uchumi wa sasa wenyewe ndio huu. Tumezoea kuona wenzetu wakiandamana mabarabarani kisa tu labda mkate uliongezwa bei kwa shiling mia tu na maandamano yakawa makubwa hatari, basi sie hatuwezi kuandamana ila hadi kwenye mitandao yetu hii nayo tushindwe kulipigia kelele hili swala?
Hili tulipigie kelele.