Kwa hali yetu waTZ, vifuatavyo vilivyapaswa angalau kuwa bei hizi ili watu wasiumie mtaani.

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,311
4,019
Ordinary people need ordinary prices.


Sukari 1kg = tsh 1500

Mchele 1kg = ths 1500

Unga ngano 1kg = tsh 1000

Nyama ng'ombe 1kg = 5000

Nyanya za buku = 15 pcs

Vitunguu vya buku = 15pcs

Kuku jike kienyeji = tsh 10,000
Kuku jike kisasa = tsh 8000

Kuku dume kienyeji = tsh 15000
Kuku dume kisasa = tsh 13000

Maziwa ng'ombe litre (not carbonated) =tsh 1000


NOTE: HIZI NI BEI NINAAVYO - WISH ZIWE KUTOKANA NA HALI NGUMU YA WATU KIUCHUMI, SIO KUWA NI PENDEKEZO BILA KUJALI FACTORS HALISIA ZILIZOPO NCHINI.

Ebu tupia vingine ukirekebisha bei ambazo unaona ziko juu out of order.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Thamani ya pesa huwa haishuki ila inapanda.

Jero la zamani ulikuwa unaweza kuilisha familia, ila Jero la sasa hata Soda hununui.

HIZO BEI HAZIWEZI KUWA-APPLIED KWENYE ULIMWENGU WA SASA!

KaziKwelikweli/JobTruTrue
Umeanza kwa kusema thamani ya pesa huwa haishuki ila inapanda, lakini maelezo yako yanaelezea jinsi thamani ya pesa inavyoshuka.

Hebu fikiria tena thamani ya pesa kushuka ni nini na kupanda ni nini.
 
Mkulima wa hayo mazao atauza kwa bei gani ili aweze kujipatia mahitaji yake? Watu wa mijini tusiendelee kuwaonea wakulima. Vitu vya viwandani vinapangwa bei na watengenezaji, ila wakulima unataka kuwapangia bei! "Ordinary people " wanatakiwa kufanya kazi saa 18 kila siku ili wajipatie mahitaji yao. Kazi ni kazi - yoyote ile!
Wanapewa ruzuku kwenye pembejeo lakini wao hawajawahi kutangaza kushusha bei.Hawana tofauti na wamiliki wa vituo vya mafuta ya magari/mitambo.Kila siku ulalamishi tu.
 
Hata hapo kweny Nyama umeweka Bei Juu sana walau iwe elf 3,000/-

Na Huduma za Kijamii napo bei ziwe chini kama Huduma ya Upatikanaji wa Umeme na maji.

Miaka ya Nyuma ilizoeleka Mafuta ya Taa(Kerosin) ndo yalikuwa Bei Ndogo Kuliko Deseal na Petrol ila kwa sasa Bei yake ni Juu mara Dufu ya nishati hiyo. Nayo inabidi yashuke ili kuepusha uvunaji wa miti kama nishati ya kupikia. Mafuta ya Taa pamoja Na Gesi zitaweza kuwa msaada kutunza mazingira ili kupelekea kuwe na Hali nzuri ya Afya na Hewa ili tupate vyakula kutoka mashambani kwa Bei njema.
 
Mkulima wa hayo mazao atauza kwa bei gani ili aweze kujipatia mahitaji yake? Watu wa mijini tusiendelee kuwaonea wakulima. Vitu vya viwandani vinapangwa bei na watengenezaji, ila wakulima unataka kuwapangia bei! "Ordinary people " wanatakiwa kufanya kazi saa 18 kila siku ili wajipatie mahitaji yao. Kazi ni kazi - yoyote ile!
Nimeshangaa sana, et mchele uuzwe 1500kg, manake mkulima wa ubaruku auze 900/kg,

Nyanya 15 sh 500,
Mkulima auze 200/15,

Cha kumshauri mleta mada, mapori yapo mengi, akalime yeye aje na hio bei, yan ng'ombe afugwe miaka 2 yeye anataka ale kg 1 kwa 5k, kwa hio mkulima auze 3k/kg,
Watu wa mjini wanaona wana haki ya kula chakula cheap,

Aende akalime yeye aje auze hivyo vyakula kwa hio bei,

Halafu sukari ni just overrated stuff, haina umuhimu wowote hata ikiuzwa 10k/kg
 
Nchi hii ni ya kununua parachichi 2k kweli matunda yalitakiwa watu wanunue kwa senti
Kitu kimoja naona watu wanapata changamoto kuelewa ni kwamba, bei za chini za vitu hazitengenezi uchumi mzuri automatically.

Uchumi mzuri wenye ufanisi ndio unaotengeneza bei nzuri za vitu.

Kwa mfano.

Mnataka bei za chini za vitu.

Serikali leo inaweza kusema inaondoa sifuri mbili katika shilingi ya Tanzania.

Kwamba kitu kilichokuwa kinauzwa shilingi 100 kiuzwe shilingi 1.

Bia hiyo mnayoisema ya sh 4500 iuzwe sh 45.

Lakini, kama uzalishaji hautabadilika, kama ufanisi katika maisha haujabadilika, mambo yatarudi palepale, hiyo shilingi 1 mpya thamani yake na upatikanaji wake utakuwa sawa na ile shilingi 100 ya zamani.

Baada ya muda mfupi tu wa mambo ku adjust, watu watarudi kulia vilevile.

Nafikiri Zambia walishawahi kufanya kitu kama hiki.
Zambia waliondoa sifuri tatu kwenye Kwacha yao, lakini haikusaidia kitu.


Hivyo, badala ya kujikita kwenye kupanga bei za vitu, tujikite zaidi kwenye kuboresha ufanisi katika uchumi, kuzalisha zaidi, kusafirisha bidhaa kwa ufanisi na gharama nafuu, kupunguza gharama za uzalishaji, kuzalisha nchini vitu vyote tunavyoweza kuzalisha nchini kwa ufanisi zaidi, kuondoa "imported inflation" kutoka kwenye bidhaa tunazoagiza nje as much as possible, kujiongeza kwenye innovation, kuongeza terms and balance of trade, kuweka a fair and incentive building tax system etc.

Tukifanya hivi, bei zita balance kwenye equilibrium kwa forces za demand and supply.

Watu wengi hawaelewi kwamba, bei za bidhaa kuwa ndogo sana kupita equilibrium ya supply and demand si kitu kizuri.

Kwa sababu zitatengeneza disinflation na halafu deflation, haya mambo yatakuja kuleta disincentive kwa producers ku produce, na kutakuwa nanihaba wa bidhaa.

Ni vigumu sana kwa muuza mkate kutengeneza mkate huku akijua mkate utatoka shilingi 1,000 wiki hii, kufika shilingi 750 wiki ijayo na kufikia sh 500 wiki itakayofuata.

Anaweza kuona ni bora asubiri upepo huu upite kwanza ndiyo arejee kwenye uzalishaji.

So, badala ya kuangalia bei zikoje, na zinatakiwa kuwa wapi ili watu wawe na nafuu, tuangalie mifumo yetu ya uzalishaji na ugavi ina inefficiencies wapi na tunaweza vipi kuziondoa ili kutengeneza uchumi wenye ufanisi zaidi.
 
Back
Top Bottom