Bei ya sukari yapaa

salehe

Member
Mar 16, 2008
83
30
Siku chache tangu rais azuie uingizwaji wa sukari ya nje. Bei imepaa kutoka sh. 2000 hadi 2500 pia mfuko wa kg 50 ulikuwa 45000 sasa hivi 47000.

Serikali isipoliangalia hili suala vizuri ifikapo mwezi ujao chai hatutakunywa tena. Kingine najiuliza inamaana viwanda vyetu haviproduce au kuna hukuma nyuma yake?

Wenye mamlaka chunguzeni suala hili
 
Siku chache tangu rais azuie uingizwaji wa sukari ya nje. bei imepaa kutoka sh. 2000 hadi 2500 pia mfuko wa kg 50 ulikuwa 45000 sasa hivi 47000 . serikali isipo liangalia hili suala vizuri ifikapo mwezi ujao chai hatutakunywa tena. kingine najiuliza ina maana viwanda vyetu haviproduce au kuna hukuma nyuma yake?wenye mamlaka chunguzeni suala hili

Weka sawa taarifa yako; f.y.i, Mfuko wa KG 50 kwa SH. 47,000= hiyo ina maana KG 1 ni SH. 940= ambapo siyo kweli hata chembe.
 
Weka sawa taarifa yako; f.y.i, Mfuko wa KG 50 kwa SH. 47,000= hiyo ina maana KG 1 ni SH. 940= ambapo siyo kweli hata chembe.
Hawa vijana wanatumwa na wanasiasa uchwara kwa malipo kiduchu...wao ni kuandika habari bila kujua wanachoandika....siku hizi wamepewa column kwenye baadhi ya magazeti kuandika upuuzi.
 
Dawa ikianza kufanya kazi, basi joto la mwili huongezeka.
Mheshimiwa hajafuta utaratibu wa vibali bali kafuta wenye navyo hivi sasa ili waanze kuomba tena na wawe controlled, siyo kama zamani watu wanapiga hela tu kijanjajanja
 
serekali imewaonya wote wanaoficha sukari!/ Ole wao!
HAYA NI MAMBO YA SARBOTAGE YASIYOVUMILIKA KAMWE!/
 
Sukali ndio nini?
Kamuulize dada yako.
Siku chache tangu rais azuie uingizwaji wa sukari ya nje. Bei imepaa kutoka sh. 2000 hadi 2500 pia mfuko wa kg 50 ulikuwa 45000 sasa hivi 47000.

Serikali isipoliangalia hili suala vizuri ifikapo mwezi ujao chai hatutakunywa tena. Kingine najiuliza inamaana viwanda vyetu haviproduce au kuna hukuma nyuma yake?

Wenye mamlaka chunguzeni suala hili
 
Siku chache tangu rais azuie uingizwaji wa sukari ya nje. Bei imepaa kutoka sh. 2000 hadi 2500 pia mfuko wa kg 50 ulikuwa 45000 sasa hivi 47000.

Serikali isipoliangalia hili suala vizuri ifikapo mwezi ujao chai hatutakunywa tena. Kingine najiuliza inamaana viwanda vyetu haviproduce au kuna hukuma nyuma yake?

Wenye mamlaka chunguzeni suala hili
Ngoja niweke sawa kwani huyu aliepost haijuwi hii industry vizuri 50KG YA SUKARI= 93,000-94,000 Kwa bei za jana na 25KG ilikuwa 46,000-48,000 na 1k ilikuwa 2000-2200 kwa Dar es salaam. Mahitaji ya sukari kwa matumizi ya viwanda na brown sugar for domestic use jumla ni Tonne 590,000. Viwanda vyetu vya ndani vinauwezo wa kuzalisha Tonne 320,000 tu brown sugar for domestic use ambapo sukari nyeupe yaani white refined sugar haizalishwi inchi kwa hiyo tunaagiza kutoka inje kiasi cha Tonne 170,000. Jumla ya mahitaji ya brown sugar kwa mwaka ni Tonne 420,000 kwahiyo tunaupungufu wa Tonne 120,000 ambayo lazima iagizwe inje ili kuziba gapu. Mpaka hapo utaona kwamba kuagiza sukari inje haiepukiki. Binafsi naona Rais alikuwa sawa ili kuzisukuma mamlaka zinazohusika kutafuta wawekezaji wanaoweza kuziba gap la Tonne 120,000 brown sugar ambapo siyo jambo la siku moja ni mchakato. Tatizo lililopo ni uingizwaji wa sukari nyingi za magendo kupitia bandari bubu ndiyo linalo asili kwa kiwango kikubwa soko la sukari ya ndani. Niliwahi kutoa mapendekezo humu kuwa ili kukabiliana na tatizo hili lazima serikali iunde kikosi kazi kitakacho husisha vyomba vyote vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kukabiliana na uingizwaji wa bidhaa za magendo kupitia bandari bubu au hata bandari zetu kama tulivyoona kwenye makontena kupita bandarini bila kulipiwa huwezi jua kama na sukari zilikuwemo. Zinahitajika juhudi za kimakusudi kabisa kukabiliana na tatizo hili siyo jambo la siku moja
 
Ni suala lisilo ingia akilini, wiki moja tu toka ipigwe marufuku ya kuingiza sukari kiholela leo hii ipande ghafla. Kuna tatizo la msingi ama kwa wasimamizi au wasambaji. Miaka kadhaa iliyopita, PAC chini ya Zitto ilitoa mapendekezo ya jinsi kupunguza gap la sukari inayozalishwa nchini (tani 300,000 kwa mwaka) na mahitaji halisi(tani 420,000 kwa mwaka), moja ikiwa ni mradi wa RUIPA ambao tunaweza kupata tani Zaidi ya 200,000 kwa mwaka. Tumefikia wapi katika utekelezaji hili?
Tunaweza piga hatua tukiwa makini.
 
Dawa ikianza kufanya kazi, basi joto la mwili huongezeka.
Mheshimiwa hajafuta utaratibu wa vibali bali kafuta wenye navyo hivi sasa ili waanze kuomba tena na wawe controlled, siyo kama zamani watu wanapiga hela tu kijanjajanja
Umesema Kweli Mkuu!! Hata Mtoto Akichoma Chanjo Ya Polio Utaambiwa Hakikisha Una Panadol, Maana Joto Litapanda Tu
 
Back
Top Bottom