gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Katika mambo ambayo hayahitaji siasa basi ni chakula.Kimsingi hali ya chakula nchini inatishia uhai wa mtanzania masikini kwani bei za nafaka zimekua zikipanda mno.
Leo ni takribani kama wiki hivi bei ya 1kg ya mahindi sokoni Tandale imefika 1350 record ambayo haijawahi kufikiwa tangu biashara hii ilipoanza kufanyika katika soko hili.
Kutokana ba mlipuko huu wa bei za mahindi ndipo bei za unga nazo zimepanda maradufu kutoka tsh37000/25kg hadi tsh48000/25kg mabadiliko ya bei ndani ya wiki moja.Kwakua bei inayouziwa Tandale ni bei ya jumla(viwandani) hivyo mtaani kiroba kimefika tsh50,000 kwa 25kg.
Ukweli ni kwamba chanzo cha tatizo hili ni serikali kufungua mipaka mwaka jana mahindi yakawa yanauzwa nje ya nchi wakati hali ya mavuno kwa mwaka jana haikua nzuri.
Kwaajili yakuweka record sawa niwakumbushe tu mwaka juzi kipindi kama hiki unga kwa 25kg uliuzwa tsh20,000 tu.Mwaka jana nao bei ya juu ilikuwa tsh 25000.
Naishauri serikali kupitia waziri wa kilimo dr Charles Tizeba wasije wakarudia kosa hili tena mwaka huu kwani mahindi sio zao la biashara kama ilivyo korosho hili ni zao la chakula mifumuko ya bei ya kiasi hiki ni hatari kwa usalama wa amani ya nchi yetu.